SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Sitawapotezea muda wenu kuwaelezea umuhimu wa taasisi ya Mahakama katika jamii na nchi yoyote ile. Hii taasisi ina heshma yake ambayo haitakiwi mtu au taasisi yoyote kuichezea, kuidhihaki, kuidharau wala kuitukana.
Kwa hiki kinachoendelea siku hizi mbili na kauli za viongozi wa Yanga akiwemo msemaji wake Ally Kamwe, ni jambo litakaloshangaza sana umma kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mahakama yenyewe haitaingilia kati haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha heshima ya Mahakama ya Tanzania inalindwa.
Hatuwezi kuruhusu Mahakama inachezewa hivi waziwazi kwa kivuli eti klabu ina mashabiki milioni 40. Kwanza hao mashabiki uliwahesabu lini wakati wanachama wenyewe tu hawafiki 50,000 na unashindwa kufikia mapato ya milangoni ya mwaka na timu ambayo mashabiki wake waliisusia timu yao.