Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Inasikitisha sana,ni aibu kubwa ,inafedhehesha,inaleta maswali mengi sana juu ya umakini na akili za chama hiki cha CHADEMA. Hii ni baada ya kusikika kwa taarifa kuwa Lissu alikuwa hana gari la kutumia katika shughuli za chama, na kwamba gari alilokuwa akitumia lilikuwa ni gari la kukodi ambalo lilikuwa likikodiwa kwa gharama kubwa sana. Na kwamba sasa imeanzishwa kampeni na harambee mitandaoni ya kuomba watu wamchangie pesa ili aweze kununua gari mpya.
Swali nalojiuliza mimi Mwashambwa ni kuwa ina maana CHADEMA ilishindwa kumpatia gari makamu mwenyekiti wake? CHADEMA katika mamilioni kwa mamilioni iliyopokea na ambayo imekuwa ikiyapata kama Ruzuku ilishindwa na imeshindwa kununua gari rasmi kwa ajili ya ofisi ya makamu Mwenyekiti wa chama Taifa? Sasa ofisi inaendeshwaje na kujiendesha vipi?
Majuzi juzi tu hapa si chama kilipokea Billion 2 na millioni mia saba? Pesa zote hizo kimepeleka wapi ikiwa hata tu gari la kumsaidia makamu wake kufanyia ziara na shughuli za chama imeshindikana kununuliwa? Hivi CHADEMA kwanini inaendeshwa kijanja janja kiasi hiki? Kwanini chama kinakosa ,mipango, mikakati na vipaombele? Kwanini chama hakijiweki katika mazingira na taswira ya chama kikuu cha upinzani na chenye viongozi wenye maono? Kwanini chama kinakuwa kama kinaongozwa na vipofu na kwenda mzobemzobe.
Hii ndio maana kuna wakati unakuta viongozi wakuu wake wamekwenda mahali kufanya ziara za kichama , halafu unasikia taarifa kuwa wanakosa mahali pa kulala kwa kisingizio kuwa eti vyumba vyote vya kulala wageni vilikuwa vimelipiwa na kuchukuliwa na watu au mtu ambaye wanasema ni adui wao kisiasa. Swali unalojiuliza ina maana chama na viongozi wake huwa wanashindwa kujuwa na kuweka mipango na mikakati mapema ya walau hata wiki moja nyuma kuwa ni wapi viongozi wake wakuu ngazi ya Taifa watalala na kufikia na kufanyia vikao vya ndani na siri? Au wao wakimaliza mikutano na kushuka jukwaani ndio wanaanza kupuyanga mitaani kutafuta vyumba vya kulala viongozi wao?
CHADEMA inatia aibu kubwa sana tena sana. Hii ndio sababu hata ukienda mikoani unakuta chama hakina hata ofisi wala pagala lililojengwa kwa ajili ya kuja kuwa ofisi. Ukiwauliza utasikia sisi tunajenga na tumejenga ofisi zetu mioyoni mwa watanzania. Kana kwamba huko mioyoni ndiko watafanyia vikao vyao,kutolea kadi za chama,kufanyia na kupanga mikakati ,kukutania kuweka misimamo ya kichama na mambo mengine mengi. CHADEMA ni chama ambacho kimekaa kizembe kizembe tu muda wote. Ni chama ambacho hakina utayari wala maandalizi ya chochote na hakiwezi kikaweka mipango hata ya nusu mwaka mbele. Ndio maana hakinaga ajenda na sera ya kueleweka kinayoisimamia zaidi ya kurukia matukio yanayojitokeza na yanayopita kama mvuke.
Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa kwa leo. Ila nimesikia watu mitaani pia wanauliza kuwa ina maana Lissu hakukatia Bima Gari lake? Kama kuna mwenye Elimu zaidi ya suala hili la Bima anaweza eleza hapa ili niwajibu huku mitaani.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.