Tanzania tuko na Engineers wa kila aina, aina zote za Engineers wanapatikana Tanzania. Ni kawaida sana sana kuwasifia Engineers as individuals wanaoibuka na Tuzo mbali mbali au wanakua recognized duniani.
Mfano, kuna Electrical Engineer mkubwa sana mtanzania mweusi kabisa ana miliki Kampuni kubwa sana ya Umeme hapo Dubai, tuna Software Enginer mwingine anatajwa kwenye media kubwa tu yuko Finland, tuna yule Mnyakyusa was kwenye Boeing huko USA, tuna Engineers wengi wengi hadi kwenye ujenzi kila mahali. Hawa ni mfano tu wa aina za Engineers tulionao. Bila kumsahau Mzee wetu wa kisasa ambaye ni Professor wa Telecommunications, Professor Mark
Kichekesho, Tanzania haina kampuni yake ya ujenzi, nazungumzia ujenzi kwa Leo maana kwenye ujenzi was nyumba na miundo mbinu Tanzania inajenga sana. .
Tunapoteza pesa nyingi sana kwenda nchi ambazo zinaenda kwenye nchi za wajenzi hao. Tanzania tuna kampuni kadhaa kubwa za ujenzi was miundo mbinu na kadhalika ambazo zinamilikiwa na serikali za nchi nyingine kwahio Leo ukisikia Tanzania imepigwa penalty ya mabilioni na mkandarasi ujue hio pesa inaenda kwenye serikali za wenzetu.
Madarasa yetu, vyuo vikuu vilivyojengwa Leo hii vingekuwa vimejengwa kwa kutumia Makampuni yetu tungekua tumeokoa fedha nyingi.
Sioni sababu ya kuwa na Wahandisi Washauri ambao ni Local na kuwa na Wahandisi ambao ni Wageni, kwangu Mimi Consultant Engineers ndio wangekua Wageni yaani watushauri when necessary! Sasa hivi wanajenga wao kisha sisi tuna washauri.
Pili, kuna baadhi ya makampuni hayo ya Wageni wanategemea perse Local Engineers meaning kwamba wala hawaji na hao "Competent, Experienced, recognized Engineers" then tunalipa hizo kampuni mabilioni.
Kwa wale Foreign Engineers wengi wao, SIO WOTE ila wengi wao huwa na ujuzi was kawaida sana.
Tunashindwaje kuanzusha Makampuni yetu? Usiniambie kuhusu mitambo maana kila mradi unakua na mitambo mipya .
Usiniambie kuhusu Capital, maana baadhi ya miradi tunakopa pesa, wananunua mitambo ndio wanaleta, sisi tunakwama wapi? Hatujui viwanda vinavyotengeneza hio mitambo tukaenda kuchukua na sisi?/
Waendesha mitambo wote ni Watanzania tena wazuri sana sana! Tunashindwa wapi?
Maabara zote ziko Tanzania, testing zote zinafanyiwa Tanzania, sasa tunakwama wapi??
Kwanini tunalipa billions kwa nchi nyingine kwa mambo ambayo tungeweza kufanya wenyewe?
SIKUBALIANI 100% na Kauli ya RAIS kuwa foreign Investors waje na Wataalam wao 100% huku ni kuua vyuo vyetu na kuwafanya wataakam wetu wawe vibarua kwenye nchi yao.
Hivi CRB wao ni kusajili na kukusanya ada kila mwaka tu? Ifutwe au iboreshwe, ni Aibu kubwa kwa miaka 60 hatuna cha kujivunia kwa upande ambao ungetokana na Uwekezaji wetu kwenye elimu.
Tujadiliane na tupingane kwa hoja sio matusi na kebehi! Tanzania tunashindwa nini???