Ni aibu, uchanga, na kukosa weledi kwa wapinzani 'kushadadia' na kutumia taarifa ya CAG kuikosoa Serikali

Ni aibu, uchanga, na kukosa weledi kwa wapinzani 'kushadadia' na kutumia taarifa ya CAG kuikosoa Serikali

Hujaelewa, anamaanisha serikali ndo imegundua haya madudu siyo wapinzani, Ina maana wapinzani wanagonjea hadi serikali igundue tatizo then ndo waanze kuisakama serikali,
CAG ni mtumishi wa serikali na kazi yake ni kugundua matatizo kama hayo,,

Msijifiche kwenye mgongo wa upinzani. Ripoti ya CAG bado mnaidharau ndio Leo wapinzani walete tuhuma zao so mtaanza kuwaita wachonganishi. Wapinzani wamewaacha mpambane na wizi wenu.
 
Soma katiba kwanza ujue kwa nini ofisi ya CAG ilianzishwa, ujue ukomo na mipaka yake. Usiandike jambo kwa pupa. CCM yako inamiliki UVCC, UWT na idara zake si mihimili ya dola kama ofisi ya CAG, TAKUKURU etc
ofisi ya CAG si mali ya chama cho chote cha siasa.
Jiongezee ufahamu kabla ya kukurupuka
Hapana hayo ni mwazo ya kianaharakati
 
Katika demokrasia ya vyama vingi, vyama vya upinzani hutafuta madudu ya serikali na kuyatoa kwa jamii. Hapa Tanzaia vyama vyetu vya upinzani vinatumia taarifa za serikali kuikosoa serikali.

Kwa mfano taarifa ya CAG ni taarifa ya serikali ikionyesha ilivyotengeneza taasisi za kuisaidia kujisahihisha na kuonyesha kuwepo kwa uwazi. Hili la serikali kuonyesha uwazi ni jambo la kupongezwa.

Kwa maana hiyo ni aibu kubwa kwa vyama vya upinzani kuitumia kama msingi kwa kuikosoa serikali. Kwa maana nyingine kama serikali ingeamaua kutoiweka taarifa ya CAG hadharani wapinzani wasingekuwa na cha kusema.

Hii inaonyesha haviko tayari kuwa wapinzani wala kuwa chama tawala.
Kwa maoni yangu naona si jambo baya kama CAG amebaini mapungufu ya Serikali ambayo yanasababishwa na uzembe, tabia za kifisadi na kutokuwajibika na hivyo kusababisha hasara kwa walipa kodi. Wanaweza wakatumia hayo kuseti agenda na kuipeleka kwa jamii maana taarifa ya CAG kuna maeneo hata hawajui kinachoendelea.....kwa maoni yangu narudia sioni tatizo hapo
 
Ni sawa kwa mfano taarifa ya Zitto ya Barrick aliitafuta na alikuwa owner wake. Hii ya kutumia taarifa ya CAG siyo sawa kwani hiyo ni internal control mechanism ya serikali

Ndio maana nashauri hiyo ripoti wawe wanaipeleka kwenye halamshauri kuu ya CCM na sio kutupigia kelele. Unaleta ripoti ya CAG hadharani halafu hutaki CHADEMA waijadili kana kwamba CAG analipwa na pesa za CCM , wakati analipwa kwa Kodi zlna tozo za wafuasi wa Upinzani pia.
 
Katiba ni ya CCM kumbe sikujua. Ndio maana hamtaki ibadilishwe. Umeulizwa swali jepesi umeshindwa kujibu, mmechukua hatua gani Kama CCM kukomesha wizi?. We unarudia tu Yale Yale.

Miaka yote mnaiba hamjawahi kuridhika hata siku moja tangu loliondo gate , Richmond dowans, escrow, 1.5 trillion etc
Wizi na binadamu havitangamani,, Wizi upo na utakuepo tu, hata walete utawala gani,, binadamu kiasiliana ana self interest,
Awamu hii imeamua kupambana na Wizi na kuupunguza na pia kuziba mianya ya Wizi,,
Lakini Wizi utakuepo,
 
Ndio maana nashauri hiyo ripoti wawe wanaipeleka kwenye halamshauri kuu ya CCM na sio kutupigia kelele. Unaleta ripoti ya CAG hadharani halafu hutaki CHADEMA waijadili kana kwamba CAG analipwa na pesa za CCM , wakati analipwa kwa Kodi zlna tozo za wafuasi wa Upinzani pia.
Miaka ya nyuma riport ilikuwa haiwekwi hadharani,, Shida iliyopo ripoti inapoanza kutumika kisiasa,
Ripot inatoka, dakika inayofuata unaambiwa chukua hatua
 
Kiufupi Tanzania Kwa Sasa hatuna wapinzani.

CCM na wapinzani wameungana kulamba asali .

Suala la upotevu wa Fedha za umma halijaanza Leo.

Watu wametajwa Kwa wazi kabisa kuwa wamechepusha pesa za umma na kuzitumia kwenye mambo yao

Mabenki yanajaza form feki yanapiga pesa mabilioni unaambiwa wakopaji walitokea nje ya nchi na kukopa bila dhamana ya kueleweka.

Yaani CCM imeshindwa kuweka mifumo ya Kubaini Mali zinazomilikiwa na viongozi wake kihalali.

Hivi unategemea Mbowe au zito Kabwe akemee ufisadi?

Miaka yote waliokemea ufisadi walikua ni akina Dr. Slaa, Mrema, Lisu ,Heche n.k. Mbowe kwenye Upigaji hua hayupo siriasi kivile.

Sasa hivi Wapinzani na CCM wanasubiri serikali itakachosema ndipo nao watarukia.

Upinzani wa Kweli utatoka ndani ya CCM .
Watu watakaoichachafia serikali ni akina Msukuma mana yeye Kwa kweli hanaga unafiki kwenye Chama chake.
Kwa Sasa Nina Imani na Dr. Msukuma na Tundu Lisu na Heche japo wanapigwa vita kwenye vyama vyao.

Tanzania ni lazima atokee mtu atakayelindanda kile Mungu alichokuwa amaekiweka kwenye maono ya Waasisi wa Taifa hili .
Kuna jambo Mungu alilitaka Kwa Watanzania ndio maana akatupa Kambarage na Karume. Hawa wote walikua ni wajamaa japo Karume alikua mkomunisti halisi na aliyeipenda sana Zanzibar kuliko Muungano wenyewe.

Nyerere hakutaifisha Mali za Mabeberu ili viongozi wa umma wanaolipwa mishahara minono wageuke Tena kuzipora Mali na mashirika ya umma.

Kuna watu wanapeana ulaji TU Kwa ajili ya kuiba na kulindana na kupeana fadhilia.

Mchechu alipewa Shirika la nyumba serikali ya Awamu ya Tano ikaona hatoshi ikamto . Sasa Kuna haja Gani ya kumrudisha mtu yule yule. Tunakua na makundi ya wabadhirifu wanaocheza na fursa za uteuzi ndani ya Serikali. Yaani ni kundi la watu wanapeana zamu ya kufisidi Mali za umma badala ya kuwekwa pembeni na wengine kujifunza na kujitahidi kufanya vizuri ili wasitolewe.

CCM na Serikali yake kwa Sasa hawateui Wala kutengu Kwa sababu ya uadilifu Bali ni kuteuana kimakundi bila kujali sifa . Yaani Mtu kama Sabaya naye anasubiri kabisa kuwa kundi lake litaingia madarakani siku Moja na atateuliwa Tena. Yaani Hana wasiwasi kabisa .
Kuna watu kulingana na ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi walitakiwa wapotee milele kwenye siasa. Hata Kupiga kampeni au kuwa Chawa hawakutakiwa kabisa.

Bila kuwa na mfumo wa kuwapeleka mahakamani Wahalifu wa Mali za umma na kuwafilisi pale inapobainika kuwa wametakatisha fedha hakika tutabaki kuwa na Taifa lenye RASILIMALI nyingi na watu wengi maskini wanaobaki kulimbikiziwa Kodi kubwa ili watawala waishi kwa anasa zilizopitiliza.
Watu wanagawana mabilioni ya umma kama jero vile .
 
Katika demokrasia ya vyama vingi, vyama vya upinzani hutafuta madudu ya serikali na kuyatoa kwa jamii. Hapa Tanzaia vyama vyetu vya upinzani vinatumia taarifa za serikali kuikosoa serikali.

Kwa mfano taarifa ya CAG ni taarifa ya serikali ikionyesha ilivyotengeneza taasisi za kuisaidia kujisahihisha na kuonyesha kuwepo kwa uwazi. Hili la serikali kuonyesha uwazi ni jambo la kupongezwa.

Kwa maana hiyo ni aibu kubwa kwa vyama vya upinzani kuitumia kama msingi kwa kuikosoa serikali. Kwa maana nyingine kama serikali ingeamaua kutoiweka taarifa ya CAG hadharani wapinzani wasingekuwa na cha kusema.

Hii inaonyesha haviko tayari kuwa wapinzani wala kuwa chama tawala.
Hoja dhaifu mno hii. Ni sawa na kusema upinzani haupaswi kuikosoa serikali kwa matendo yake.
 
comment ya kuumbumbumbu kabisa hii...ukijibiwa jambo usilojua unageuzia kwenye uanaharakati au hujui kazi ya ofisi ya CAG unadhani ni kuihabarisha serikali au chama tawala tu?
Unadhani hivyo- sawa. Serikali ni ya nani sasa?
 
Hoja dhaifu mno hii. Ni sawa na kusema upinzani haupaswi kuikosoa serikali kwa matendo yake.
Nimesema na ninasema wapinzani wanayo haki ya kuikosoa serikali lakini hawezi kutumia taarifa za serikali kuikosoa- sijui kwa nini unapata tabu kuelewa
 
Katika demokrasia ya vyama vingi, vyama vya upinzani hutafuta madudu ya serikali na kuyatoa kwa jamii. Hapa Tanzaia vyama vyetu vya upinzani vinatumia taarifa za serikali kuikosoa serikali.

Kwa mfano taarifa ya CAG ni taarifa ya serikali ikionyesha ilivyotengeneza taasisi za kuisaidia kujisahihisha na kuonyesha kuwepo kwa uwazi. Hili la serikali kuonyesha uwazi ni jambo la kupongezwa.

Kwa maana hiyo ni aibu kubwa kwa vyama vya upinzani kuitumia kama msingi kwa kuikosoa serikali. Kwa maana nyingine kama serikali ingeamaua kutoiweka taarifa ya CAG hadharani wapinzani wasingekuwa na cha kusema.

Hii inaonyesha haviko tayari kuwa wapinzani wala kuwa chama tawala.
Kwa hiyo ulitaka wakae kimya?
 
  1. Tumeunda, kuiopa uwezo taasisi ya CAG kikatiba
  2. Tumeifanya taasis ya CAG kutoa taarifa kwa mamlaka na umma
  3. Tumewapa nafasi wahusika kutoa maelezo ya mapungufu yao kwa mjibu wa taarifa ya CAG
  4. Wanaobainika wanachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria
Toa mfano wa mtu aliyechukuliwa hatua. NB. Udsiniambie bodi inevunjwa.
 
Nimesema na ninasema wapinzani wanayo haki ya kuikosoa serikali lakini hawezi kutumia taarifa za serikali kuikosoa- sijui kwa nini unapata tabu kuelewa
Kama hizo taarifa zinawahusu watanzania kwanini upinzani usikosoe?
 
Kama hizo taarifa zinawahusu watanzania kwanini upinzani usikosoe?
unakosoa serikali au taarifa? Ninachosema hapa ni kazi ya upinzani kuikosoa serikali; wanakosoa serikali kwa taarifa walizozipata wenyewe na si kwa kutumia taarifa za serikali
 
Kwa hiyo ulitaka wakae kimya?
Kabisa kwa sababu hawana jipya- If they have something to say and want to tell us, they should tell us what we do not already know.
 
CCM ilitakiwa ijitengenezee mifumo ya kuisaidia ndani ya chama chao, na sio kupitia fedha za umma. Au unadhani fedha za serikali zinatokana na kodi za wañaccm tu? Mmekuwa wajinga hadi miradi ya serikali mnaona kama ni ya CCM. Iko siku utasema wapinzani wanapita kwenye barabara zilizojengwa na CCM na wala sio kodi za wananchi.
Mkuu haina ubishi serikali ni ya CCM
 
Kwa maana hiyo ni aibu kubwa kwa vyama vya upinzani kuitumia kama msingi kwa kuikosoa serikali. Kwa maana nyingine kama serikali ingeamaua kutoiweka taarifa ya CAG hadharani wapinzani wasingekuwa na cha kusema.
Sijui kama ulishirikisha akili yako wakati wa kuandika huu utumbo!
 
Back
Top Bottom