Ni aidha Wenje au Lissu waenguliwe CHADEMA kama chama kipo Makini, vinginevyo ni utapeli

Niambie Lisu ameshinda,
Wenje kashinda.
Wanafanyaje Kazi ili CHADEMA iendelee na isipasuke?
lolote linaweza tokea ila approach ipi wanachadema wangetumia kuimaliza hii kirusi ni ipi? nani apite kama kiongozi kuinusuru chadema? kimtazamo chadema wakiweza tegua huu mtego ndo kutatathimini uhai na kukua chama kikubwa au kifo kama chama kikubwa
 

Mkuu sijasema Abdul alikuwa na mabulungutu ya pesa wala Lisu hajasema hivyo. Ulichoeleza ndicho Lisu alichoeleza. Kuwa alifuatwa kwaajili ya kushawishiwa.

Maelezo ya Lisu yanasema aliambiwa kuwa viongozi wengine wa CHADEMA wamepewa pia. Ingawaje kauli hii yaweza kutumika kama Njia ya kumshawishi mtu hata kama hakuna wengine waliopewa.
 

Lisu hawezi kushirikiana na Wala rushwa Akiwa Mwenyekiti hilo lipo wazi. Na kama ni hivyo inatarajiwa migogoro Mikubwa Mikubwa kuzuka ndani ya CHADEMA na wengi kukimbia ikiwa Lisu atakuwa Mwenyekiti.

Ni kama vile JPM tuu ingawaje kwa Lisu utofauti wake yeye anapenda ukweli na kufuata Sheria
 
Uko sahihi
Kuna mmoja lazima a drop
 
kumbe ni fununu ngoja tupate uhakika, hivi mtu akimsindikiza mtu kupokea au kutoa rushwa ni jinai? wenje hakuwa muhongwaji wala mhongaji na labda hakujua dhumuni la huyo mgeni,
 
hizi naona ni kama amsha amsha tu za diamond kutoa single
 
yaani fununu za chuki na uzushi wa mzushi wa kimataifa ziwakoseshe chadema kiongozi bora na makini kama wenje, kweli?

yaani kweli tumuamini mtu mzushi na mwenye tamaa kama huyo, ambae ni hodari wa kuomba kuchangiwa mara kwa mara, eti amekataa billions of money? thubutu wewe, na shida zote zilizomzonga aache pesa huyo?

uzushi hauwezi kumkosesha muungwana wenje fursa ya kutimiza ndoto zake hata siku moja.


Huyu Lisu ni kiongozi wa ajabu sana,
aliwahi kuulizwa juu ya masuala haya ya rushwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha television,

cha kushangaza,
eti akawa anamtishia tu yule mwanahabari kuwataja wala rushwa waliompelekea rushwa.

sasa,
huyo ni kiongozi wa aina gani anaionea aibu rushwa kama sio unafiki tu?

Wenje atakua makamu mwenyekiti wa Chadema Taifa bila mbambamba yoyote gentleman 🐒
 
Kwani unajua Billion 1 ya Kibongo ni sawa na Vibunda vingapi vya Dollar 100 zikiwa 100?kwa mana zikiwa kama kawaida bunda la dollar 10,000?Mbona zina bebeka tu.
 
Ndio kazi imeanzia hapo sasa mkuu
 
Aaaa!
Kwani Bwashee
Alishakubali kumwachia Lau Masha ubunge wa Nyamagana ingawa alishinda, wananchi wakakataa kwa kutishia kutowesha amani pale Mwanza,Siro wakati huo akiwa RPC alihakikisha mshindi halali anatangazwa kwa gharama za kumtosa bosi wake Masha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.Mwisho wa Siku Wilson Kabwe akamtangaza Wenje kwa shingo upande
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…