Ni aina gani ya maswali ambayo siyo busara kuuliza ovyo ovyo?

Ni aina gani ya maswali ambayo siyo busara kuuliza ovyo ovyo?

Nakumbuka kuna usiku mmoja nilikuwa maeneo na washkaji japo sio kivile maana huwa tunakutana kwenye kijiwe cha pombe...

Ilipotimu saa sita kamili usiku nikapata notification kwenye simu kuwa hongera Leo ni siku yako ya kuzaliwa...nilifurahi Ila nilijiona mzembe maana nilikuwa nimesahau kabisa,Kwa furaha niliyokuwa nayo nikaamua kuzungusha round moja ya kinywaji katika Ile meza huku nikiwaambia Leo ni siku yangu ya kuzaliwa....

Basi washkaji wakanitakia maisha marefu na baraka tele,tukafurahi tukiendelea kupiga mambo,miongoni mwa watu tuliokaa pale akaniuliza umetimiza miaka mingapi?nikamtajia miaka yangu,ikawa mada kuu sasa kila mmoja akataja miaka yake,Kwa ujumla katika Ile meza nikagundua washkaji wanne walikuwa wamenizidi umri,wawili nilikuwa nimewazidi kiumri....

Sasa ikawa mambo yamekuwa tofauti kila mada ikijadiliwa ukichangia unahukumiwa kutokana na umri wako...linaweza likaongelewa Jambo ukasikia mtu anakuambia"kaa kimya wewe,bado bwana mdogo utashindana na mm nilietangulia kuliona jua"

Kiukweli pale nilijifunza Kwa nn watu huwa hawapendi kuweka wazi umri wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unaishi ili 'ule' au unakula ili "uishi" swali la kipuuzi kweli yaani kutoka kwa mpuuzi fulani.
 
Back
Top Bottom