Ni ajabu hawa watu wana PhDs lakini ni Wapumbavu kabisa

Ni ajabu hawa watu wana PhDs lakini ni Wapumbavu kabisa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
Kuna watu wana elimu ya juu kabisa, wana PhD, lakini ni wapumbavu wa kutupwa. Hebu leo tuangalie baadhi yao:

Richard Dawkins (PhD in Biology). Huyu ameshinda tuzo nyingi kwa kazi zake za sayansi, lakini anatumia muda mwingi kuhubiri kuwa Mungu hayupo. Anasema maisha yalitokea kwa bahati tu!

Lawrence Krauss (PhD in Theoretical Physics) - ameandika kitabu "A Universe from Nothing," akidai eti the universe can originate without a divine creator. Katika kitabu hicho, hana hoja za maana, anazungusha zungusha tu maneno.

Karl Marx (PhD in Philosophy). Huyu alikuwa staunch atheist. Ndiye aliyepandikiza sumu ya Ukomunisti, akifundisha kwamba dini ni "opium ya watu." Matokeo yake? Mamilioni walikufa kwa sababu ya mawazo yake potofu.

Hao watu Mungu anawaita “Wapumbavu”
"Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” – Zaburi 14:1(BHN)

Kumbe mtu anaweza kuwa na PhD, lakini kama anadai kwamba Mungu hayupo, mtu huyo ni MPUMBAVU kabisa mbele za Mungu.

Mungu kama anakuita Mpumbavu, unatarajia nini?
 
Ume msahau Stephen hawking, alisema uwezekano wa kuwepo na mungu kwenye ulimwengu ni mdogo sana.

Ukweli unaweza kuwaita unavyoweza kuwaita kwamba wajinga au wapumbavu ila wana hoja kuliko maaskofu na wanazuoni wengi.
 
Kuna watu wana elimu ya juu kabisa, wana PhD, lakini ni wapumbavu wa kutupwa. Hebu leo tuangalie baadhi yao:

Richard Dawkins (PhD in Biology). Huyu ameshinda tuzo nyingi kwa kazi zake za sayansi, lakini anatumia muda mwingi kuhubiri kuwa Mungu hayupo. Anasema maisha yalitokea kwa bahati tu!

Lawrence Krauss (PhD in Theoretical Physics) - ameandika kitabu "A Universe from Nothing," akidai eti the universe can originate without a divine creator. Katika kitabu hicho, hana hoja za maana, anazungusha zungusha tu maneno.

Karl Marx (PhD in Philosophy). Huyu alikuwa staunch atheist. Ndiye aliyepandikiza sumu ya Ukomunisti, akifundisha kwamba dini ni "opium ya watu." Matokeo yake? Mamilioni walikufa kwa sababu ya mawazo yake potofu.

Hao watu Mungu anawaita “Wapumbavu”
"Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” – Zaburi 14:1(BHN)

Kumbe mtu anaweza kuwa na PhD, lakini kama anadai kwamba Mungu hayupo, mtu huyo ni MPUMBAVU kabisa mbele za Mungu.

Mungu kama anakuita Mpumbavu, unatarajia nini?
Elimu ya dunia haiwezi kuyaelewa mambo ya Rohoni.
Mtume Paulo anasema, "Mtu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake ni upuzi" (1 Wakorintho 2:14)
 
Kuna watu wana elimu ya juu kabisa, wana PhD, lakini ni wapumbavu wa kutupwa. Hebu leo tuangalie baadhi yao:

Richard Dawkins (PhD in Biology). Huyu ameshinda tuzo nyingi kwa kazi zake za sayansi, lakini anatumia muda mwingi kuhubiri kuwa Mungu hayupo. Anasema maisha yalitokea kwa bahati tu!

Lawrence Krauss (PhD in Theoretical Physics) - ameandika kitabu "A Universe from Nothing," akidai eti the universe can originate without a divine creator. Katika kitabu hicho, hana hoja za maana, anazungusha zungusha tu maneno.

Karl Marx (PhD in Philosophy). Huyu alikuwa staunch atheist. Ndiye aliyepandikiza sumu ya Ukomunisti, akifundisha kwamba dini ni "opium ya watu." Matokeo yake? Mamilioni walikufa kwa sababu ya mawazo yake potofu.

Hao watu Mungu anawaita “Wapumbavu”
"Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” – Zaburi 14:1(BHN)

Kumbe mtu anaweza kuwa na PhD, lakini kama anadai kwamba Mungu hayupo, mtu huyo ni MPUMBAVU kabisa mbele za Mungu.

Mungu kama anakuita Mpumbavu, unatarajia nini?

Werevu wa Setfree na Upumbavu wa kina Bertrand Russel na John Schellenberg

1741758628547.png

Prof. Bertrand Russel

Setfree, amejenga hoja ifuatayo:
  1. Mtu yeyote mwenye PhD na anayedai kwamba Mungu hayupo, anakuwa ni "MPUMBAVU kabisa."
  2. Kuna watu wana PhD na wanasema kwamba "Hakuna Mungu," wakiwemo kina Richard Dawkins, Lawrence Krauss, Karl Marx, na Bertrand Russel.
  3. Kwa hiyo, watu hawa wenye PhD ni "wapumbavu wa kutupwa."
Lakini, napendekeza kwamba hoja yake ni batili kwa sababu dokezo la kwanza halikubaliki, maana halina ukweli wowote.

Natumia mfano wa "wapumbavu" wawili, mmojawapo wa Uingereza na mwingine wa Ujerumani, kuonyesha kwamba dokezo lake la kwanza ni batili.

Bertrand Russel (Mwingereza) alisema kuwa, kama ikitokea, siku ya kiyama Mungu akaja kutoa hukumu kwa watu wote yeye atajitetea kwa kusema hivi:

Bwana Mungu, nilijua haupo maana ushahidi uliokuwa hapa duniani haukuwa unatosha kuthibitisha uwepo wako mahali popote duniani.​

Kisha Russel akaongeza kusema kwamba atauliza tena:

Bwana Mungu, kwa nini siku zote umekuwa unajificha kiasi hiki kama wezi, majambazi, wala rushwa, wazinzi na wahalifu wengine ambao hukimbia macho ya watu?

Hoja ya Russel ambayo hujulikana kama "the argument from divine hiddenness against the existence of a God" inao muundo wa kimantiki ufuatao:
  1. If God exists, then nonbelief should not occur, meaning that, it would be impossible for people to disbelieve in him (incompatibility premise).
  2. But, nonbelief phenomenon specified in the above premise occurs in the actual world (existential premise).
  3. Therefore, deductively, it follows that, God does not exist.
Hoja hii inaweza kupewa muundo mbadala ufuatao:
  1. If nonbelief exists then, probably, God does not (improbability premise).
  2. Nonbelief probably exists (probability premise).
  3. Therefore, inductively, it follows that, God probably does not exist.
1741868215892.png

Dr. John L. Schellenberg

Hoja ya Russel iliungwa mkono na John L. Schellenberg (Mjerumani) aliyeboresha hoja ya Russel kama ifuatavyo"

  1. Necessarily, if God exists, anyone who is (i) not resisting God and (ii) capable of meaningful conscious relationship with God is also (iii) in a position to participate in such relationship (able to do so just by trying).
  2. Necessarily, one is at a time in a position to participate in meaningful conscious relationship with God only if at that time one believes that God exists.
  3. Necessarily, if God exists, anyone who is (i) not resisting God and (ii) capable of meaningful conscious relationship with God also (iii) believes that God exists. (From 1 and 2)
  4. There are (and often have been) people who are (i) not resisting God and (ii) capable of meaningful conscious relationship with God without also (iii) believing that God exists.
  5. God does not exist
Mpaka hapo ili "upumbavu" wa kina Russel na Schellenberg anaouongelea Setfree ukubalike kwa wasomaji makini inabidi aonyeshe ubovu wa hoja zao hapo juu. Hajafanya hivyo.

Kwa hiyo, Setfree ajue kwamba siku akienda kuwahubiria watu wenye uelewa mkubwa kuliko yeye kama vile kina Russel lazima azabwe vibao kama huyu jamaa hapa chini.

Mmoja alisema anataka kujiua ili akahakikishe kama kuna maisha mengine baada ya kifo.
 
Natamani unihubiri labda naweza kuamini aisee
Ndugu yangu, umesema labda unaweza kuamini. Hii ina maana kwamba huamini kuwa Mungu yupo. Lakini hebu fikiria uhai wako, hewa unayovuta, ulimwengu wenye utaratibu kamili—unafikiri vyote hivi vilitokea kwa bahati tu kama huyo jamaa anavyodai? La hasha! Hata Waswahili wanasema "Ukiona vyaelea, vimeundwa"

Kila kitu kinachotuzunguka ni ushahidi kuwa kuna Mungu aliye hai na ndiye aliyetuumba. “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake.” (Zaburi 19:1)

Mungu alipoiumba dunia, wanadamu wa kwanza Adam na Hawa walitenda dhambi kwa kula tunda la mti waliokatazwa. Mungu akasema, kwakuwa wamefanya dhambi hiyo watakufa. Kuanzia wakati huo, kifo, dhambi na uovu viliingia duniani. Ndiyo sababu kila mtu anayezaliwa anakuwa katika hali ya dhambi. Jiulize kwanini mtoto mchanga akinyimwa titi na mamaye anampiga, nani amemfundisha kupiga? Ni asili ya dhambi iliyomo ndani yake.

Dhambi hii ilitutenganisha na Mungu. Ila kwakuwa Mungu ana upendo, alichukua hatua ya kumtuma Yesu Kristo duniani ili aje atuokoe. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16)

Ilibidi damu yake Yesu imwagike msalabani ndio tuweze kupatanishwa na Mungu na kusamehewa dhambi zetu. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu—ikiwa ni pamoja na dhambi ya kutoamini. “Bali Mungu aonyesha pendo lake mwenyewe kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Warumi 5:8)

Ili uupate msamaha huo, unahitaji kufanya haya yafuatayo:

Amini na kukiri moyoni mwako kuwa Yesu alikufa na kufufuka kwa ajili yako. Warumi 10:9-10 –
“Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”

Tubu dhambi zako zote na uziache kabisa. Matendo 3:19 – “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.”

Mpokee Yesu moyoni mwako kwa imani awe Bwana na Mwokozi wako. Yohana 1:12 – “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake."

Ukifanya hayo tu utakuwa umeokoka. Utakuwa umeokoka hukumu ya moto wa milele na utakuwa umepata "tiketi" ya kuingia mbinguni siku Yesu atakaporudi. Wasioamini wote watatupwa katika moto wa milele. Ufunuo 21:8 –"Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na waabudu sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."

Kwahiyo nakusihi, usikubali moyo wako uendelee kutoamini. Usikubali shetani akudanganye eti Mungu hayupo. Shetani ameishahukumiwa kutupwa katika ziwa liwakalo moto.

Mpokee Yesu sasa na utaona nguvu yake na uwepo wake maishani mwako.

Kama uko tayari kufanya hayo niliyokuambia, omba(fuatisha sala hii ya toba) kwa moyo wako wa dhati, Mungu atakusamehe na kukuhesabu kuwa mtoto wake sasa hivi:

Omba hivi:
"Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kukua kiroho.

Karibu kwenye familia ya wanaoamini kuwa Mungu yupo na wanaokwenda kwake mbinguni kwenye raha ya milele!
 
Kuna watu wana elimu ya juu kabisa, wana PhD, lakini ni wapumbavu wa kutupwa. Hebu leo tuangalie baadhi yao:

Richard Dawkins (PhD in Biology). Huyu ameshinda tuzo nyingi kwa kazi zake za sayansi, lakini anatumia muda mwingi kuhubiri kuwa Mungu hayupo. Anasema maisha yalitokea kwa bahati tu!

Lawrence Krauss (PhD in Theoretical Physics) - ameandika kitabu "A Universe from Nothing," akidai eti the universe can originate without a divine creator. Katika kitabu hicho, hana hoja za maana, anazungusha zungusha tu maneno.

Karl Marx (PhD in Philosophy). Huyu alikuwa staunch atheist. Ndiye aliyepandikiza sumu ya Ukomunisti, akifundisha kwamba dini ni "opium ya watu." Matokeo yake? Mamilioni walikufa kwa sababu ya mawazo yake potofu.

Hao watu Mungu anawaita “Wapumbavu”
"Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” – Zaburi 14:1(BHN)

Kumbe mtu anaweza kuwa na PhD, lakini kama anadai kwamba Mungu hayupo, mtu huyo ni MPUMBAVU kabisa mbele za Mungu.

Mungu kama anakuita Mpumbavu, unatarajia nini?
Kujiona mwenye hekima ndiyo upumbavu wenyewe.
"...msijione wenye hekima sana..." (Warumi 12:16). Dawkins na wenzake wanajifanya wana akili na hekima kuliko Mungu!
 
Ume msahau Stephen Hawking,
Yeah, huyu naye ingawa alipata PhD alikuwa mpumbavu sana. Stephen Hawking alikuwa haamini kwamba kuna maisha baada ya kifo. Kama hakutubu kabla ya kifo chake, saa hizi atakuwa anaungua motoni na kusema maneno kama ya yule tajiri: "Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.(Luka 16:22-24)
 
Back
Top Bottom