Umesahau mwingine anaitwa Prof Betrand Russel.
Yeye alisema kuwa siku ya kiyama Mungu atajapokuja kuwahukumu watu wote yeye atajitetea hivi:
Bwani Mungu, nilijua haupo maana ushahidi ulioko hapa duniani hautoshi kuthibitisha uwepo wako mahali popote duniani.
Kisha Russel akasema atamwuliza:
Bwana Mungu, kwa nini unajificha kiasi hiki kama mhalifu anayekimbia macho ya watu?
Hoja ya Russel inao muundo wa kimantiki ufuatao:
1. If God exists, then nonbelief does not occur.
2. Nonbelief occurs.
3. Therefore, God does not exist.
Mpaka hapo upumbavu wa kina Russel uko wapi?
Na ujue siku ukienda kuwahubiria watu wenye uelewa mkubwa kama wa Russel lazima uzabwe vibao kama hiyo jamaa hapo chini.
View attachment 3267240
Bertrand Russell, hoja zake hazina mashiko. Zina makosa ya kimantiki.
1. Makosa ya Kuhusisha Matokeo(False Implication)
Russell anadai kwamba kama Mungu yupo, basi hakuna mtu atakayekosa kuamini. Hii sio sahihi kwa sababu Mungu amewapa wanadamu uhuru wa kuchagua(free will), hivyo watu wanaweza kuamua kumkataa.
Kutokuamini hakumaanishi kwamba kitu hakipo. Kuna watu hawaamini kwamba sayari ya Pluto ipo, lakini hilo halifanyi Pluto isiwepo.
Biblia inasema wazi kuwa kuna watu wasioamini kwa sababu shetani amepofusha akili zao (2 Wakorintho 4:4).
2. Makosa ya Kutoa Hitimisho Lisilo Sahihi(Non Sequitur)
Hata kama kuna watu wasioamini, hiyo haiwezi kuthibitisha kwamba Mungu hayupo. Kuna watu hawaamini kwamba kuna gravity, lakini wakiruka juu bado wanaanguka!
Kuhusu Kauli ya Russell "Kwa nini Mungu anajificha kama mhalifu?"
Jibu ni kwamba Mungu hajajificha, bali amejifunua kwa njia mbalimbali:
- Kwa njia ya Uumbaji – Dunia na viumbe vyote vinaonyesha utukufu wa Mungu (Zaburi 19:1).
- Kwa njia ya Dhamiri ya Binadamu – Kila mtu anayo dhamiri inayomwezesha kutofautisha mema na mabaya(Warumi 2:15).
- Kwa njia ya Yesu Kristo – Mungu alijifunua kikamilifu kwa mwanadamu kupitia Yesu Kristo (Yohana 14:9).
- Kwa njia ya Biblia – Neno la Mungu linafunua mpango wa Mungu kwa mwanadamu.
Kwahiyo tatizo sio kwamba Mungu anajificha, bali watu wenyewe ndio wanaokataa kumuona Mungu.
Mtu anaweza kuona mwanga wa jua, lakini akiamua kufumba macho, jua halitaonekana kwake. Vivyo hivyo, Mungu yupo wazi kwa wote wanaotaka kumuona kwa imani.
Yeremia 29:13 –
"Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote."
Upumbavu wa Russel ndio huo. Ukweli umefunuliwa lakini yeye anazidi kupinga tu kwa kiburi.
Umesema mhubiri akiwahubiri watu wenye akili kama Russell atazabwa vibao. Ni sawa. Sio tu kuzabwa vibao hata kupigwa kwa mawe kama Stefano alivyofanyiwa. Yesu alijua hayo yatawapata wanafunzi wake ndio sababu aliwaambia:
"Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua roho; mwogopeni yeye awezaye kuangamiza mwili na roho katika jehanum." (Mathayo 10:28)
Yesu alipigwa mijeledi, sembuse sisi?
Wanaowapiga wahubiri, siku ya mwisho watajitetea lakini utetezi wao hautakubaliwa na Mungu.
Mt 7:22-23.
Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana,...
Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’
Nimejibu maswali yako yote?