Ni ajabu hawa watu wana PhDs lakini ni Wapumbavu kabisa

Ni ajabu hawa watu wana PhDs lakini ni Wapumbavu kabisa

Dini ni taratibu walizojiwekea wanadamu wakijaribu kumtafuta Mungu. Huwa wanatumia akili kumtafuta Mungu.

Kristo hakuleta dini duniani, Bali wokovu. Alikuja kutuokoa tuliopotea. Kristo alipokuja alikuta dini duniani za Kiyahudi - Mafarisayo na Masadukayo. Watu Hawa wa dini hawakuwa wanamwelewa Kristo. Hata leo watu wa dini huwa hawamwelewi Kristo.

Fuata hiyo Sala ya mtumishi Setfree hapo juu kwa kumaanisha kisha utapokea Wokovu na Roho wa Mungu atakufunulia mengi ambayo akili yako kamwe haiwezi kuyaelewa!

karibu kwenye ufalme
Great
 
Ungekuwa unasoma Biblia usingekosa majibu ya maswali yako. Biblia inaeleza wazi hizi ni siku za mwisho ndio sababu maadili yameporomoka. Ukisoma 2 Tim 3:1-2 imeandikwa hivi:
"Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. Watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu; watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema; watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo..."

JESUS IS COMING SOON, REPENT OF YOUR SINS BEFORE IT'S TOO LATE.
Ajabu weng wao ni wakristo so church totally fail to play its role.
 
Sidhani kama utakuwa sahihi, mtu kama karl marx aliitendea haki phd yake kwa kujenga hoja ambazo mpka leo zinaesha mashiko yake (marx's theories of life) sasa hapa bongo kuna phd ngapi tumezipa kazi serikalini na hakuna cha maana? Hao una haki ya kuwaita wapumbafu
Inaonekana wewe ulisoma vitabu vya Karl Marx kwa juu juu.

Ngoja nikueleze vizuri jinsi theories zake zisivyo na mashiko:

Theories zake zliondoa uhuru wa dini katika nchi kama USSR, China, na Korea Kaskazini. Hii kwako ni faida?

Theories zake zilichochea Mapinduzi ya umwagaji damu.
Marx alifundisha kuwa mapinduzi ya wafanyakazi dhidi ya matajiri lazima yafanyike kwa nguvu, hata kwa kumwaga damu. Historia imethibitisha kuwa nchi zilizojaribu kufuata falsafa yake (kama USSR, China ya Mao, Cambodia ya Pol Pot) zilishuhudia mauaji ya halaiki (mass killings).

Marx alitaka kuondoa umiliki wa mali binafsi, akidai kila kitu kimilikiwe na serikali kwa manufaa ya wote. Matokeo yake ni kwamba nchi zilizojaribu mfumo wa kikomunisti ziliishia kuangamiza uchumi, kusababisha umasikini na njaa.

Ulisoma "The Communist Manifesto?" Katika hiyo manifesto, Marx aliona familia kama chombo cha mfumo wa unyonyaji. Alipendekeza kulea watoto isiwe jukumu la wazazi bali la serikali. Hii kwako unaona sawa?

Karl Marx alitegemea msaada wa rafiki yake Friedrich Engels ili aishi. Hakuwa na kazi ya maana, alikwepa kulipa madeni, na familia yake iliathirika kwa umasikini.

Kwahiyo, Marx siyo tu kwamba alikuwa na mawazo yanayopingana na maadili ya Kikristo, bali pia falsafa yake imeleta madhara makubwa ulimwenguni. Huyu ni mpumbavu na anapata sasa motoni malipo ya kumkana Mungu.
 
Kuna watu wana elimu ya juu kabisa, wana PhD, lakini ni wapumbavu wa kutupwa. Hebu leo tuangalie baadhi yao:

Richard Dawkins (PhD in Biology). Huyu ameshinda tuzo nyingi kwa kazi zake za sayansi, lakini anatumia muda mwingi kuhubiri kuwa Mungu hayupo. Anasema maisha yalitokea kwa bahati tu!

Lawrence Krauss (PhD in Theoretical Physics) - ameandika kitabu "A Universe from Nothing," akidai eti the universe can originate without a divine creator. Katika kitabu hicho, hana hoja za maana, anazungusha zungusha tu maneno.

Karl Marx (PhD in Philosophy). Huyu alikuwa staunch atheist. Ndiye aliyepandikiza sumu ya Ukomunisti, akifundisha kwamba dini ni "opium ya watu." Matokeo yake? Mamilioni walikufa kwa sababu ya mawazo yake potofu.

Hao watu Mungu anawaita “Wapumbavu”
"Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” – Zaburi 14:1(BHN)

Kumbe mtu anaweza kuwa na PhD, lakini kama anadai kwamba Mungu hayupo, mtu huyo ni MPUMBAVU kabisa mbele za Mungu.

Mungu kama anakuita Mpumbavu, unatarajia nini?
Kwanza jiulize, wewe unayo PhD?
 
Aliyeanza kuwaita hivyo ni Mungu. Mimi nime-quote Neno la Mungu. Ni wapumbavu kwa sababu PhD zao haziwezi hata kuzuia wasizeeke.
hilo neno la mungu unalojua wewe liliandikwa na nani? si na binaadamu? una uhakika gani mungu yupo hadi useme mungu mwenyewe aliwaita watu wapumbavu?

pia ni mungu yupi hasa? wa muslims? wa christians? au wa hinduism? cas wapo wengi na kila mmoja ameandikiwa kitabu chake na binadamu, sasa huyo alieita watu wapumbafu ni yupi exactly?
 
Hebu fikiria, wale wote ambao hawapotezi mda kwa kusali ndio wenye akili duniani. Karibu teknologia yote ya ulimwengu inaendeshwa na "atheists " mwafrika yupo bussy kufunga na kusali ila mchina yupo bussy na teknologia. Nani mwenye maendeleo? Namalizia kusema "dini ni utumwa uliotukuka ".
 
Dini ni taratibu walizojiwekea wanadamu wakijaribu kumtafuta Mungu. Huwa wanatumia akili kumtafuta Mungu.

Kristo hakuleta dini duniani, Bali wokovu. Alikuja kutuokoa tuliopotea. Kristo alipokuja alikuta dini duniani za Kiyahudi - Mafarisayo na Masadukayo. Watu Hawa wa dini hawakuwa wanamwelewa Kristo. Hata leo watu wa dini huwa hawamwelewi Kristo.

Fuata hiyo Sala ya mtumishi Setfree hapo juu kwa kumaanisha kisha utapokea Wokovu na Roho wa Mungu atakufunulia mengi ambayo akili yako kamwe haiwezi kuyaelewa!

karibu kwenye ufalme
sawa sasa kama dini ni utaratibu wa mwanadamu kumtafuta Mungu, je, huo utaratibu unakubalika mbele za Mungu au haukubaliki?
 
Kugundua kuwa hakuna Mungu nayo ni akili ya hali ya juu.
Karl Marx alisema "hakuna Mungu" sasa hivi yuko mavumbini. Angekuwa ana akili nyingi angeweza kuzuia Neno hili alilosema Mungu lisitimie:
Mwanzo 3:19
"Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakaporudi katika ardhi, kwa kuwa katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi, nawe mavumbini utarudi."
 
Binafsi nadhani hatuitaji kumuona Mungu ili tuamini kuwa yupo, the evidence is all around us....
 
Upumbavu halali wa Bertrand Russel na Schellenberg kuhusu uwepo wa Mungu

View attachment 3267441

Setfree, amejenga hoja ifuatayo:
  1. Mtu mwenye PhD, na anayedai kwamba Mungu hayupo, anakuwa ni MPUMBAVU kabisa.
  2. Kuna watu wana elimu ya juu kabisa, wana PhD, wanasema kwamba "Hakuna Mungu," wakiwemo kina Richard Dawkins, Lawrence Krauss, Karl Marx, na Bertrand Russel.
  3. Kwa hiyo, watu hawa ni "wapumbavu wa kutupwa."
Lakini, napendekeza kwamba hoja yake ni batili kwa sababu dokezo la kwanza halikubaliki, maana halina ukweli wowote.

Natumia mfano wa "wapumbavu" wawili, mmojawapo wa Uingereza na mwingine wa Ujerumani, kuonyesha kwamba dokezo lako la kwanza ni batili.

Bertrand Russel (Uingereza) alisema kuwa siku ya kiyama Mungu atajapokuja kuwahukumu watu wote yeye atajitetea hivi:

Bwana Mungu, nilijua haupo maana ushahidi uliokuwa hapa duniani haukuwa unatosha kuthibitisha uwepo wako mahali popote duniani.​

Kisha Russel akaongeza kusema atamwuliza:

Bwana Mungu, kwa nini siku zote umekuwa unajificha kiasi hiki kama wezi, majambazi, wala rushwa, wazinzi na wahalifu awengine ambao hukimbia macho ya watu?

Hoja ya Russel inao muundo wa kimantiki ufuatao:
  1. If God exists, then nonbelief should not occur, meaning that, it would be impossible for people to disbelieve in him (incompatibility premise).
  2. But, nonbelief phenomenon specified in the above premise occurs in the actual world (existential premise).
  3. Therefore, deductively, it follows that, God does not exist.
Hoja hii inaweza kupewa muundo mbadala ufuatao:
  1. If nonbelief exists then, probably, God does not (improbability premise).
  2. Nonbelief probably exists (probability premise).
  3. Therefore, inductively, it follows that, God probably does not exist.
Hoja ya Russel iliungwa mkono na Wlter Schellenberg wa Ujerumani aliyeboresha hoja ya Russel kama ifuatavyo"

  1. Necessarily, if God exists, anyone who is (i) not resisting God and (ii) capable of meaningful conscious relationship with God is also (iii) in a position to participate in such relationship (able to do so just by trying).
  2. Necessarily, one is at a time in a position to participate in meaningful conscious relationship with God only if at that time one believes that God exists.
  3. Necessarily, if God exists, anyone who is (i) not resisting God and (ii) capable of meaningful conscious relationship with God also (iii) believes that God exists. (From 1 and 2)
  4. There are (and often have been) people who are (i) not resisting God and (ii) capable of meaningful conscious relationship with God without also (iii) believing that God exists.
  5. God does not exist
Mpaka hapo ili "upumbavu" wa kina Russel na Schellenberg anaouongelea Setfree ukubalike kwa wasomaji makini inabidi aonyeshe ubovu wa hoja zao hapo juu. Hajafanya hivyo.

Kwa hiyo, Setfree ajue kwamba siku akienda kuwahubiria watu wenye uelewa mkubwa kuliko yeye kama vile kina Russel lazima azabwe vibao kama hiyo jamaa hapo chini.


View attachment 3267240
Kwa Dunia ya Sasa ukisema hakuna MUNGU wewe ni mpumbavu kabisa hatakama ni mwanasayansi mwenyewe professorial, nitakuuliza unipe sayansi ya kiwete kutembea Kwa Maombi ya siku Moja na bubu kuongea Kwa siku Moja bila dawa ya aina yeyote.
 
Kwa Dunia ya Sasa ukisema hakuna MUNGU wewe ni mpumbavu kabisa hatakama ni mwanasayansi mwenyewe professorial, nitakuuliza unipe sayansi ya kiwete kutembea Kwa Maombi ya siku Moja na bubu kuongea Kwa siku Moja bila dawa ya aina yeyote.
Unawaongelea kiwete na kiziwi gani, waliopona lini, wapi na walipona kwa sababu ya kitu gani?
 
Jifunze kutofautisha kati ya mungu na Mungu.
Whether Mungu, MUNGU, muNGU, MUngu, mungu, nk bado maana ni ile ile. Wewe kama unaitwa Juma, mtu akiandika jina lako juma utalikataa kisa hajaweka herufi kubwa nwanzoni? Hapa tunaangalia mantiki, sio uandishi wa herufi.
 
Unawaongelea kiwete na kiziwi gani, waliopona lini, wapi na kwa njia gani?
Mathayo 15:30-31:
"Wakamjia makutano mengi, wenye ulemavu, vipofu, viwete, bubu, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya; hata makutano waliposhangaa walipoona ya kuwa bubu wananena, viwete wanatembea, vipofu wanapata kuona; wakamtukuza Mungu wa Israeli."

Yesu Kristo habadiliki. Ameishawatumia Watumishi wake wengi kutenda miujiza kama hiyo nyakati hizi. Kama hujasikia ina maana wewe hupendi kusikia habari za Injili.
 
Back
Top Bottom