Ni ajabu hawa watu wana PhDs lakini ni Wapumbavu kabisa

Great
 
Ajabu weng wao ni wakristo so church totally fail to play its role.
 
Inaonekana wewe ulisoma vitabu vya Karl Marx kwa juu juu.

Ngoja nikueleze vizuri jinsi theories zake zisivyo na mashiko:

Theories zake zliondoa uhuru wa dini katika nchi kama USSR, China, na Korea Kaskazini. Hii kwako ni faida?

Theories zake zilichochea Mapinduzi ya umwagaji damu.
Marx alifundisha kuwa mapinduzi ya wafanyakazi dhidi ya matajiri lazima yafanyike kwa nguvu, hata kwa kumwaga damu. Historia imethibitisha kuwa nchi zilizojaribu kufuata falsafa yake (kama USSR, China ya Mao, Cambodia ya Pol Pot) zilishuhudia mauaji ya halaiki (mass killings).

Marx alitaka kuondoa umiliki wa mali binafsi, akidai kila kitu kimilikiwe na serikali kwa manufaa ya wote. Matokeo yake ni kwamba nchi zilizojaribu mfumo wa kikomunisti ziliishia kuangamiza uchumi, kusababisha umasikini na njaa.

Ulisoma "The Communist Manifesto?" Katika hiyo manifesto, Marx aliona familia kama chombo cha mfumo wa unyonyaji. Alipendekeza kulea watoto isiwe jukumu la wazazi bali la serikali. Hii kwako unaona sawa?

Karl Marx alitegemea msaada wa rafiki yake Friedrich Engels ili aishi. Hakuwa na kazi ya maana, alikwepa kulipa madeni, na familia yake iliathirika kwa umasikini.

Kwahiyo, Marx siyo tu kwamba alikuwa na mawazo yanayopingana na maadili ya Kikristo, bali pia falsafa yake imeleta madhara makubwa ulimwenguni. Huyu ni mpumbavu na anapata sasa motoni malipo ya kumkana Mungu.
 
Kwanza jiulize, wewe unayo PhD?
 
Aliyeanza kuwaita hivyo ni Mungu. Mimi nime-quote Neno la Mungu. Ni wapumbavu kwa sababu PhD zao haziwezi hata kuzuia wasizeeke.
hilo neno la mungu unalojua wewe liliandikwa na nani? si na binaadamu? una uhakika gani mungu yupo hadi useme mungu mwenyewe aliwaita watu wapumbavu?

pia ni mungu yupi hasa? wa muslims? wa christians? au wa hinduism? cas wapo wengi na kila mmoja ameandikiwa kitabu chake na binadamu, sasa huyo alieita watu wapumbafu ni yupi exactly?
 
Hebu fikiria, wale wote ambao hawapotezi mda kwa kusali ndio wenye akili duniani. Karibu teknologia yote ya ulimwengu inaendeshwa na "atheists " mwafrika yupo bussy kufunga na kusali ila mchina yupo bussy na teknologia. Nani mwenye maendeleo? Namalizia kusema "dini ni utumwa uliotukuka ".
 
sawa sasa kama dini ni utaratibu wa mwanadamu kumtafuta Mungu, je, huo utaratibu unakubalika mbele za Mungu au haukubaliki?
 
Kugundua kuwa hakuna Mungu nayo ni akili ya hali ya juu.
Karl Marx alisema "hakuna Mungu" sasa hivi yuko mavumbini. Angekuwa ana akili nyingi angeweza kuzuia Neno hili alilosema Mungu lisitimie:
Mwanzo 3:19
"Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakaporudi katika ardhi, kwa kuwa katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi, nawe mavumbini utarudi."
 
Binafsi nadhani hatuitaji kumuona Mungu ili tuamini kuwa yupo, the evidence is all around us....
 
Kwa Dunia ya Sasa ukisema hakuna MUNGU wewe ni mpumbavu kabisa hatakama ni mwanasayansi mwenyewe professorial, nitakuuliza unipe sayansi ya kiwete kutembea Kwa Maombi ya siku Moja na bubu kuongea Kwa siku Moja bila dawa ya aina yeyote.
 
Kwa Dunia ya Sasa ukisema hakuna MUNGU wewe ni mpumbavu kabisa hatakama ni mwanasayansi mwenyewe professorial, nitakuuliza unipe sayansi ya kiwete kutembea Kwa Maombi ya siku Moja na bubu kuongea Kwa siku Moja bila dawa ya aina yeyote.
Unawaongelea kiwete na kiziwi gani, waliopona lini, wapi na walipona kwa sababu ya kitu gani?
 
Jifunze kutofautisha kati ya mungu na Mungu.
Whether Mungu, MUNGU, muNGU, MUngu, mungu, nk bado maana ni ile ile. Wewe kama unaitwa Juma, mtu akiandika jina lako juma utalikataa kisa hajaweka herufi kubwa nwanzoni? Hapa tunaangalia mantiki, sio uandishi wa herufi.
 
Unawaongelea kiwete na kiziwi gani, waliopona lini, wapi na kwa njia gani?
Mathayo 15:30-31:
"Wakamjia makutano mengi, wenye ulemavu, vipofu, viwete, bubu, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya; hata makutano waliposhangaa walipoona ya kuwa bubu wananena, viwete wanatembea, vipofu wanapata kuona; wakamtukuza Mungu wa Israeli."

Yesu Kristo habadiliki. Ameishawatumia Watumishi wake wengi kutenda miujiza kama hiyo nyakati hizi. Kama hujasikia ina maana wewe hupendi kusikia habari za Injili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…