Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Habari hii sijaichakachua. Nairipoti kama nilivyoisikia. Tazama source ujiridhishe.
Habari kutoka Iran zinasema kwamba misikiti mingi sana(kwa maelfu) katika nchi ya Iran imefungwa na mamilioni ya watu wameamua kuacha Uislamu na kumfuata Yesu.
Ripoti hiyo imetolewa na Hooman Khalil, aliyezaliwa Iran katika familia ya Kiislamu.
Khalil anasema kwamba mapinduzi haya ya kiimani hayajawahi kushuhudiwa kwa miaka 40 iliyopita. Ajabu ni kwamba mapinduzi hayo yameanzishwa na wanawake waliosema "Imetosha sasa"(enough is enough).
Khalil anaeleza kwamba hata shirika la habari la All Arab News limetangaza habari hiyo. Shirika hilo likimnukuu kiongozi mmoja wa kidini wa Iran, limesema kwamba, misikiti kati ya 50,000 hadi 75,000 imefungwa.
Khalil anaeleza tena kwamba, kufungwa kwa misikiti hiyo, kulianza wakati wanawake walipokataa kuvaa hijab. Watu walipoona wanawake wakipigwa risasi kichwani, kufunikwa uso na kuchapwa viboko hadharani, kunyongwa na kutundikwa mitaani, kwa kosa la kutokuvaa hijab, waliona haina sababu ya kuendelea na dini hiyo.
Inakadiriwa kwamba kuna Wakristo milioni 10 wanaofanya ibada zao kwa siri nchini Iran, kwa sababu wakijulikana tu wameacha Uislamu, sheria za dini hiyo zinasema lazima wauawe.
Source: CBN News
View: https://www.youtube.com/watch?v=dDAMvTWZseo