Ni ajabu na kweli: Mamilioni ya watu wa Iran wamgeukia Yesu!

Ni ajabu na kweli: Mamilioni ya watu wa Iran wamgeukia Yesu!

Kwa hio wewe unaenda peponi kwa kusema Yesu ni Mungu au hahaha, wewe ni mshirikina una mfananisha Mungu na Yesu mtoto wa Mariam.

We vaa shangaa za kiunoni tu zitakupeleka kwenye pepo unayo itaka, lakini.pepo ya Mungu sahau.
Soma uzi huu upate ufahamu zaidi kwa nini Yesu anaitwa Mungu
 
Al Jazeera utafananisha na hizo habari zako hazina source
Kazi kwelikweli. Source ni CBN News, mkuu, nimekuwekea link na video.
By the way huyo Hooman amekuambia kwamba mambo mazito aliyoyatenda Esther wa kwenye Biblia yalifanyikia Iran, wakati huo ikiitwa Persia. Esther ni mwanamke shujaa sana katika Biblia. Kwahiyo yamkini historia inajirudia sasa ndio sababu kinamama wengi huko wamesema "enough is enough"
 
Soma uzi huu upate ufahamu zaidi kwa nini Yesu anaitwa Mungu
Twende taratibu Hapo mwanzo kulikuwa Neno naye Neno alikuwa kwa Mungu mpaa hapo Neno alikuwepo kwa Mungu safi sana OK Neno alikuwa kwa Mungu.

Tuendelee naye Neno alikuwa Mungu.

Sa tueleze Neno alikuwa kwa Mungu.
Afu huyo huyo Neno ni Mungu.

Hapo hata kichaa lazima atasema kuna vitu viwili tofouti kati ya Neno alikuwepo kwa Mungu na Neno ni Mungu.

Hebu kazipime alili zako hapo lazima haziko sawa. Neno alikuwa kwa Mungu hapo ni vitu viwili tofouti. Afu Neno ni Mungu hapo ni kitu kimoja. Sa lipi nilipi Neno lilikuwa kwa Mungu au Neno ni Mungu.

Kama Neno ni Mungu kwa hio Mungu anaitwa Neno sio hahaha.

Kama Neno alikuwa Kwa Mungu huyo neno ni nani? Na alikuwa anafanya nini kwa Mungu? Mfanya kazi au
 
Kazi kwelikweli. Source ni CBN News, mkuu, nimekuwekea link na video.
By the way huyo Hooman amekuambia kwamba mambo mazito aliyoyatenda Esther wa kwenye Biblia yalifanyikia Iran, wakati huo ikiitwa Persia. Esther ni mwanamke shujaa sana katika Biblia. Kwahiyo yamkini historia inajirudia sasa ndio sababu kinamama wengi huko wamesema "enough is enough"
CBN hizo Story pia waliziongea 2024 bado unawamini tu hahaha hakuna lolote.

Habari hii sijaichakachua. Nairipoti kama nilivyoisikia. Tazama source ujiridhishe.

Habari kutoka Iran zinasema kwamba misikiti mingi sana(kwa maelfu) katika nchi ya Iran imefungwa na mamilioni ya watu wameamua kuacha Uislamu na kumfuata Yesu.

Ripoti hiyo imetolewa na Hooman Khalil, aliyezaliwa Iran katika familia ya Kiislamu.

Khalil anasema kwamba mapinduzi haya ya kiimani hayajawahi kushuhudiwa kwa miaka 40 iliyopita. Ajabu ni kwamba mapinduzi hayo yameanzishwa na wanawake waliosema "Imetosha sasa"(enough is enough).

Khalil anaeleza kwamba hata shirika la habari la All Arab News limetangaza habari hiyo. Shirika hilo likimnukuu kiongozi mmoja wa kidini wa Iran, limesema kwamba, misikiti kati ya 50,000 hadi 75,000 imefungwa.

Khalil anaeleza tena kwamba, kufungwa kwa misikiti hiyo, kulianza wakati wanawake walipokataa kuvaa hijab. Watu walipoona wanawake wakipigwa risasi kichwani, kufunikwa uso na kuchapwa viboko hadharani, kunyongwa na kutundikwa mitaani, kwa kosa la kutokuvaa hijab, waliona haina sababu ya kuendelea na dini hiyo.

Inakadiriwa kwamba kuna Wakristo milioni 10 wanaofanya ibada zao kwa siri nchini Iran, kwa sababu wakijulikana tu wameacha Uislamu, sheria za dini hiyo zinasema lazima wauawe.

Source: CBN News

View: https://www.youtube.com/watch?v=dDAMvTWZseo

Hawauawi tena wakibadili dini!?.. maana huko nyuma mlidai wakibadili dini huuawa, hakuna aliyewahi pigwa risasi ya kichwa Iran kisa hajavaa hijab
 
Hii dunia ina maajabu sana! unaweza kushangaa zile sehemu ngumu ukristo kupenya zikageuka kuwa za kikristo na dola la kiislam kuanguka! naam ndivyo ilivyo
Mtu akishakua muislam,akaujua uislam,atakua radhi kuwa mpagani kuliko kuwa mkristo,imani ya kikristo inachekesha kwa muislam anayeujua uislam
 
Mtu akishakua muislam,akaujua uislam,atakua radhi kuwa mpagani kuliko kuwa mkristo,imani ya kikristo inachekesha kwa muislam anayeujua uislam
na kinyume chake pia mkristo aliyeujua ukristo hawezi kuwa muislam
 
Twende taratibu Hapo mwanzo kulikuwa Neno naye Neno alikuwa kwa Mungu mpaa hapo Neno alikuwepo kwa Mungu safi sana OK Neno alikuwa kwa Mungu.

Tuendelee naye Neno alikuwa Mungu.

Sa tueleze Neno alikuwa kwa Mungu.
Afu huyo huyo Neno ni Mungu.

Hapo hata kichaa lazima atasema kuna vitu viwili tofouti kati ya Neno alikuwepo kwa Mungu na Neno ni Mungu.

Hebu kazipime alili zako hapo lazima haziko sawa. Neno alikuwa kwa Mungu hapo ni vitu viwili tofouti. Afu Neno ni Mungu hapo ni kitu kimoja. Sa lipi nilipi Neno lilikuwa kwa Mungu au Neno ni Mungu.

Kama Neno ni Mungu kwa hio Mungu anaitwa Neno sio hahaha.

Kama Neno alikuwa Kwa Mungu huyo neno ni nani? Na alikuwa anafanya nini kwa Mungu? Mfanya kazi au
Unaenda nje ya mada Adiosamigo. Kwa kukusaidia ngoja nikupe majibu kwa ufupi tu:

Yohana 1:1 haina mkanganyiko kama unavyofikiri wewe
"Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu."
Maneno "alikuwa kwa Mungu" yanaonyesha uhusiano wa karibu, sio kwamba ni mtu tofauti kwa asili. Maneno "alikuwa Mungu" yanaonyesha asili yake ya uungu. Hii inaonyesha kuwa Neno (Yesu) ni Mungu kwa kiini, lakini tofauti na Baba kwa nafsi.

Hoja kwamba "Neno alikuwa kwa Mungu, kwa hiyo ni viumbe viwili tofauti" haina mashiko. Hizo ni nafsi mbili za Mungu mmoja. Katika fundisho la Utatu, Mungu ni mmoja kwa asili, lakini anajifunua katika nafsi tatu: Baba, Mwana (Neno), na Roho Mtakatifu.

Umeuliza "Kama Neno ni Mungu, basi Mungu anaitwa Neno?"
"Neno" ni jina la nafsi ya Pili ya Utatu Mtakatifu (Yesu Kristo).

"Naye Neno alifanyika mwili..." (Yohana 1:14)
Yesu alikuwepo milele kama Neno kabla hajazaliwa duniani. Sasa ni Mungu Mwana, yaani Neno aliyefanyika mwili.

Umeuliza tena kama "Neno alikuwa kwa Mungu, alikuwa anafanya nini? Mfanyakazi au?" Neno hakuwa mfanyakazi, bali Mungu mwenyewe anayeshiriki utendaji wa uumbaji:
"Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika." (Yohana 1:3)

Hivyo, Neno ni Mshiriki wa uumbaji, sio kiumbe wala mfanyakazi wa Mungu.

Naomba tuishie hapa, tusitoke nje ya mada, please.
 
Sawa sawa bora tubaki kwenye mada, kule Iran hakuna kabisa hizo Story za Wairan wanaingia ukristo na Masajid yamefungwa.
 
Maodre,maaskofu,wachungaji wengi tu wamesilimu
Kabisa kabisa.

Mtoa mada anakuambia Mungu ni neno na anajigeuza mara tatu sijui hazisomi bibilia zao au Biblia inasema kwamba Mungu alisema hivi: “Mimi ni Yehova; sikubadilika.” (Malaki 3:6) Vivyo hivyo, Biblia inasema kwamba Mungu “habadiliki, kama kugeuka kwa kivuli

Biblia inajipinga inaposema kwamba “hakuna mwanadamu ambaye amemwona Mungu,” na wakati uleule inasema mahali pengine kwamba Musa ‘alimwona Mungu wa Israeli’? Pia wangapi wamemuona Yesu ambaye wanasema ni Mungu 1=3 nakuambia ukanisa ni kwaya tupu hahaha

Any way tubaki kwenye mada
 
Hata China watu wanaoongoka na kuwa wakristo, idadi yao imekuwa ikiongezeka kwa kasi kubwa.

Hata Indonesia pia idadi ya wakristo inaongezeka kwa kasi.

Haya mataifa yakimkubali na kumkiri Kristo kuwa ndiyo masiha, yatapata ushindi mkubwa katika kila lililo jema dhidi ya wanaomkana Kristo.

"Mtu hafiki kwa Babangu isipokuwa kwa kupitia mimi"

"Mimi ndimi njia na ufufuo"

"Ukiniona mimi umemwona Baba, maana mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu. Ukiniona Mimi umemwona Baba"

"Mtu asipozaliwa kwa mara ya pili, kwa maji na kwa Roho mtakatifu, kamwe hawezi kuokoka"
 
Hii dunia ina maajabu sana! unaweza kushangaa zile sehemu ngumu ukristo kupenya zikageuka kuwa za kikristo na dola la kiislam kuanguka! naam ndivyo ilivyo

Siyo ajabu. Kwanza baya maeneo ya mashariki ya kati ambayo yana waislam wengi, ndiyo yaliyokuwa na wakristo wengi wengi hapo mwanzo. Ndiyo kanisa la kwanza. Kanisa kubwa baada ya Jerusalem, lilikuwa kanisa la Damascus.

Haiwezi kushangaza mataifa haya yakashuhudia yakichukua nafasi zao za kale, na tunaojiona ni wakristo wa mbele, tukawa nyuma yao, maana kuna mashahidi wengi kutoka mataifa haya walikubali kufa kwaajili ya imani.

Fahamuni kuwa waefeso na wagalatia ni waturuki wa leo.
 
1752185302384.png
 
Yesu ni maji ya uzima, usipoyanywa utayaogea, in short hayakwepeki
 
Back
Top Bottom