Leo hii tunasikia makelele mengi kuhusu reform. Reform ya mifumo ya uchaguzi nk. Lakini jambo la kushangaza na la kusikitisha ni hili: watu wanaodai reform ya nje, wao wenyewe hawajawahi kuruhusu Mungu awafanyie reform ya ndani. Ni ajabu sana mtu anapigania mabadiliko ya nje wakati moyo wake umejaa chuki, hasira, uongo, uasherati na uzinzi, ulevi, uchawi na kutotubu!
Reform ya kweli huanza ndani ya mtu, si kwenye mabango mitaani. Mungu anafurahia zaidi mtu ambaye yuko tayari moyo wake uwe reformed:
Luka 15:7
"Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu."
Watu wanataka viongozi waadilifu, lakini wao wenyewe ni wadanganyifu kazini na majumbani. Wanapiga wake zao. Maongezi yao yamejaa tamaa za mwili. Midomo yao imejaa maneno yasiyo na heshima kwa wazazi na wanaowazidi umri.
Mathayo 7:4-5
"Wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako? Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako."
Wengine wanapaza sauti dhidi ya rushwa, lakini wao wenyewe wanalipa 'kitu kidogo' ili wapate huduma wasizostahili. Wanatoa rushwa ili magari yao yasikamatwe barabarani.
Warumi 2:21
Basi, wewe unawafundisha wengine; kwa nini hujifundishi wewe mwenyewe? Unawahubiria wengine wasiibe, lakini kumbe wewe mwenyewe unaiba.
So while others are busy chanting “No reform, no election,” I’m over here praying: “Lord, reform my heart and count me among Your elect!” Because one day, all earthly elections will fade, but only those whose names are written in the Lamb’s Book of Life will reign forever and ever. Amen.