Ni baraka kwa introvert kujifahamu kuwa ni introvert na kuamua kuutumia uintrovert wake kwa manufaa!

Ni baraka kwa introvert kujifahamu kuwa ni introvert na kuamua kuutumia uintrovert wake kwa manufaa!

Introverts wako vizuri zaidi kwenye kuandika kuliko kuongea mkuu usisahau hilo na huko ndiko uwezo wao wa kujenga hoja unakoonekana

Wewe ndio unawaona wajinga kwa sababu ya chuki zako ulizonazo juu yao, ila wataalam wengi wa saikolojia wanasema introverts ndio wana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko extroverts, kundi la extroverts ndio lina wajinga wengi kuliko la introverts

Kuna mambo lazima tujifunze kuishi nayo na kukubaliana nayo, ukizingatia kwenye hii dunia kila character ina opposite yake dunia ina watu zaidi ya 8 Billion, hakuna character ambayo ni common kwa binadamu wote hawa na haitakuja kuwepo
Well said mkuu
 
Ktk jamii za watanzania, introvert anapitia wakati mgumu Sana
Tangu akiwa mtoto wazazi wanamnyanyasa kwa kumuita lofa, zoba, kiburi na majina mengine

Shuleni wanafunzi wenzake wanamdharau Sana
Waalimu wanamdharau pia, wanamuona mtu aliyezubaa Sana!
Waalimu na wazazi wanampa pressure Sana,, "We vipi acha kuzubaa, changamka"

Kwenye kupendekeza uongozi, introvert ananyimwa kila posti,

Ila pamoja na hulka zao za upole, anapoonewa ikifika zaidi ya uvumilivu wake, Hawa jamaa wako vizuri kwenye kutoa vipigo kwa maextrovert!
Kuna ule msemo, watu wakimya usiwachokoze!

Hawanaga uwezo wa kujitetea kwa maneno!

Inapofika wakati wa kupata mke, Hawa jamaa wanapata tabu Sana, kwakuwa wanawake wengi hawawapendi watu wakimya,
Mara nyingi huishia kupata wanawake second class au third class

Hawa jamaa wanajua Sana kuvumilia maisha ya ndoa! Ni ngumu Sana kuwatupa wapenzi wao! Kwa mantiki hio Hawa si wazalishaji wa single mamaz!

Kwenye issue za kazi Hawa Ni wachapa kazi! Ingawa wanapigwa bao Sana na maextrovert kwenye interviews
Hawa wanatoboa vizuri kwenye issue za ufundi, kilimo, Sanaa, uandishi, sayansi na utafiti, kuliko maextrovert
Ukienda hospitali ukamkuta doctor Hana maneno mengi furahia
Ukienda garage ukamkuta fundi Hana maneno mengi furahia

Kiukweli Introvert Ni mtu na nusu Ila maisha yao yanapitia changamoto Sana hususani za kudharauliwa!
Wewe NI introvert?
 
Back
Top Bottom