Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Hakuna kitu sipendi kama mtu kujisifu yeye ni introvent.
Like, who cares? Wewe endelea kuwa hivyo kwanini utuambie?
Introvert ni Watu wasiojiamini na mara nyingi wanaroho mbaya.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna kitu sipendi kama mtu kujisifu yeye ni introvent.
Like, who cares? Wewe endelea kuwa hivyo kwanini utuambie?
Mbona jina la Ally Kiba sijaliona hapo kwenye list ya introvert. Maana tunaambiwaga yeye hapendagi masifa na makiki!Introvert wa JF mpoo! Unafahamu thamani ya uintrovert wako?
Kuwa introvert si ugonjwa. Nibaraka, lakini ukijitambua na kujikubali. Vinginevyo, unaweza ukawa sawa na mtu anayetaka kubadilishana kilo kumi za dhahabu kwa kuku kumi wa mayai! Hasara iliyoje!
Jamii yetu, kwa kutokufahamu, wamekuwa wakiwalaumu introvert kwa kutokuwa extrovert. Kuna wanaofikiria wana viburi,, wengine wanafikiri ni waoga, wengine wanawaona kama ni watu wanaojisikia, n.k. Hawajui kuwa wao ndiyo "wajinga", kwa kushindwa kujua utofauti wa maintrovert an extrovert.
Mungu, kwa nia njema kabisa, kaona vyema watu wawe na "personality" tofauti. Wewe unafikiri ingekuwaje kama dunia nzima ingekuwa ni ya maextrovert pekee? Au unafikiri ingekuwaje kama watu wote wangekuwa ni maintrovert?
Kama ambavyo Mungu kaamua kututofautisha, tuzikubali hizo tofauti na tuzitumie kwa manufaa. Wazazi wenye watoto maintrovert waache kuwalazamisha kuwa extrovert, badala yake wawasaidie kuvuna manufaa ya kuwa introvert.
Kwa wasiofahamu, kuwa introvert si ugonjwa. Ni namna ubongo unavyochakata taarifa zinazotumwa kwake. Kwamba, kiwango cha "dopamine" na muundo wa "dopamine receptors" kwenye ubongo ndiyo humtofautisha Introvert na Extrovert.
Tafiti za Kisayansi zinaonesha kuwa mtu anaweza kubainika kama ni introvert au extrovert akiwa na umri wa kuanzia miezi minne.
Kwa wasiojua, hizi ni baadhi ya tabia za Introverts:
~ Wakiamya
~ Wanapenda mazingira ya kuwa peke yao - hawafurahii mazingira ya mchanganyikeni
~ Wanapenda mazingira ya ukimya
~ Hufikiri kabla ya kuongea
~ Wana kawaida ya kuwa na marafiki wachache
~ Ni wasiri sana, n.k. (wengine wataongezea).
Baadhi ya watu maarufu ambao ni Introverts:
1. Warren Buffett
2. Mark Zuckerberg
3. Bill Gates
4. Steve Wozniak
5. Larry Page
6. Michael Jordan
7. Elon Musk
8. Charles Darwin
9. Mahtma Gandhi
10. Al Gore
11. Sir Isaac Newton
12. Rosa Parks
13. Eleanor Roosevelt
14. Abraham Lincoln
15. Barack Obama
16. Marissa Mayer
17. Guy Kuwasaki
18. Hilary Clinton
19.Michael Jackson
20. Brenda Barnes, e.t.c.
Nafikiri, na hawa Watanzania nao ni introvert: Dr. Mohammed Gharib Bilal, Dr. Ally Mohammed Shein, Dr. Philip Mpango, n.k.
Introvert, umebarikiwa kuwa introvert! Usitamani kuwa extrovert!
Extrovert, hakuna hasara kuwa Extrovert! Usiigize kuwa introvert!
Kila mmoja akae kwenye nafasi yake!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mimi mtu akishaanza “Mimi ni introvent” & blahblah… he/she is cancelled!
Umeandika kweli kabisaa,V
Vitu vingine tuwaachie wazungu, asili yetu ni kujichanganya hao wanaoiga uzungu wanajipa stress bure tu.
Ni kweli kuna kasumba ya kuwachukia watu wanaojiita introverts hata kama wengine wanasema ukweli, ni kwa sababu introverts wengi husemekana wana akili sana na uwezo mkubwa wa kujenga hoja, kwahiyo tukiona mtu anajiita introvert moja kwa moja huwa tunahisi huyu anajaribu kutuambia kwamba ana akili na wabongo hatupendi kuona mtu anajisifia maana mtu wa aina hii tunamuona ni mjuaji
Introverts wako vizuri zaidi kwenye kuandika kuliko kuongea mkuu usisahau hilo na huko ndiko uwezo wao wa kujenga hoja unakoonekanaMara nyingi wanaoitwa introvert ninawaonaga wajinga. Wasio na maarifa, wasiojua kujenga hoja, wasiojiamini,
Kwa sababu introvert Tabia yao kuu ni Ukimya.
👏👏👏🙏Introverts wako vizuri zaidi kwenye kuandika kuliko kuongea mkuu usisahau hilo na huko ndiko uwezo wao wa kujenga hoja unakoonekana
Wewe ndio unawaona wajinga kwa sababu ya chuki zako ulizonazo juu yao, ila wataalam wengi wa saikolojia wanasema introverts ndio wana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko extroverts, kundi la extroverts ndio lina wajinga wengi kuliko la introverts
Kuna mambo lazima tujifunze kuishi nayo na kukubaliana nayo, ukizingatia kwenye hii dunia kila character ina opposite yake dunia ina watu zaidi ya 8 Billion, hakuna character ambayo ni common kwa binadamu wote hawa na haitakuja kuwepo
Ulichokosea ni kuishia kwenye mtazamo wako bila kufanya utafiti.Mara nyingi wanaoitwa introvert ninawaonaga wajinga. Wasio na maarifa, wasiojua kujenga hoja, wasiojiamini,
Kwa sababu introvert Tabia yao kuu ni Ukimya.
Kuwa introvert au extrovert ni hali ya kiasili kabisa kama ilivyo kawaida kwa mwanaume kuota ndevu na mwanamke kuota maziwa.Umeandika kweli kabisaa,
1. Ninajisifia kwa lipi? Kuripoti kile wasomi wenye akili walichobaini kwenye tafiti zao? Mimi siyo neurosurgeon wala mwanasaikolojia, na wala sikushiriki kwa namna yo yote kwenye hizo tafiti zao, nina kipi cha kujisifia? Unaweza kuonesha chembe yo yote ya kujisifisu kwangu kwenye uzi husika?Naona hapa unajisifia tu,unakuwaje Mwanasiasa halafu ni introvert.
Afu Elon Musk ana uintrovet gani au umeamua kuchukua matajili wote na kuwaweka katika hilo kundi.
Very possible! Huenda hata ikawa inaendeshwa na marobot.Unaweza kukuta ile account zake za mitandaoni anaendesha mtu mwingne on behalf. Yeye yuko zake busy huko kwingne hana habari.
Mkuu, wanaoweza kuwadharau introvert ni "wajinga". Lakini wenye akili wanawathamini sana. Wanajua Wana hazina nzuri.Ktk jamii za watanzania, introvert anapitia wakati mgumu Sana
Tangu akiwa mtoto wazazi wanamnyanyasa kwa kumuita lofa, zoba, kiburi na majina mengine
Shuleni wanafunzi wenzake wanamdharau Sana
Waalimu wanamdharau pia, wanamuona mtu aliyezubaa Sana!
Waalimu na wazazi wanampa pressure Sana,, "We vipi acha kuzubaa, changamka"
Kwenye kupendekeza uongozi, introvert ananyimwa kila posti,
Ila pamoja na hulka zao za upole, anapoonewa ikifika zaidi ya uvumilivu wake, Hawa jamaa wako vizuri kwenye kutoa vipigo kwa maextrovert!
Kuna ule msemo, watu wakimya usiwachokoze!
Hawanaga uwezo wa kujitetea kwa maneno!
Inapofika wakati wa kupata mke, Hawa jamaa wanapata tabu Sana, kwakuwa wanawake wengi hawawapendi watu wakimya,
Mara nyingi huishia kupata wanawake second class au third class
Hawa jamaa wanajua Sana kuvumilia maisha ya ndoa! Ni ngumu Sana kuwatupa wapenzi wao! Kwa mantiki hio Hawa si wazalishaji wa single mamaz!
Kwenye issue za kazi Hawa Ni wachapa kazi! Ingawa wanapigwa bao Sana na maextrovert kwenye interviews
Hawa wanatoboa vizuri kwenye issue za ufundi, kilimo, Sanaa, uandishi, sayansi na utafiti, kuliko maextrovert
Ukienda hospitali ukamkuta doctor Hana maneno mengi furahia
Ukienda garage ukamkuta fundi Hana maneno mengi furahia
Kiukweli Introvert Ni mtu na nusu Ila maisha yao yanapitia changamoto Sana hususani za kudharauliwa!
Umemjibu vizuri sana..bila jazba wala maneno machafu kama aliyoyatumia yeye.Introverts wako vizuri zaidi kwenye kuandika kuliko kuongea mkuu usisahau hilo na huko ndiko uwezo wao wa kujenga hoja unakoonekana
Wewe ndio unawaona wajinga kwa sababu ya chuki zako ulizonazo juu yao, ila wataalam wengi wa saikolojia wanasema introverts ndio wana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko extroverts, kundi la extroverts ndio lina wajinga wengi kuliko la introverts
Kuna mambo lazima tujifunze kuishi nayo na kukubaliana nayo, ukizingatia kwenye hii dunia kila character ina opposite yake dunia ina watu zaidi ya 8 Billion, hakuna character ambayo ni common kwa binadamu wote hawa na haitakuja kuwepo
Ukimya wa extrovert huhesabiwa kuwa ni hekima.Tabia ya ukimya ipo kama ugonjwa na vingi ndani.......
✅🙏🙏🙏Umemjibu vizuri sana..bila jazba wala maneno machafu kama aliyoyatumia yeye.
mimi mwenyewe ni introvert nayajua mateso yake bro usiombe ukiwa introvert kuchizika ni rahisiSiyo kweli mamlukii