Ni baraka kwa introvert kujifahamu kuwa ni introvert na kuamua kuutumia uintrovert wake kwa manufaa!

Ni baraka kwa introvert kujifahamu kuwa ni introvert na kuamua kuutumia uintrovert wake kwa manufaa!

Mtu anasema yeye ni introvert halafu hapo hapo ana tabia hizi.
1. Yupo kwenye social media (Instagram, Twitter, Facebook, Whatsapp, JF) na kila siku anapost kuanzia story, picha kuhusu maisha yake au kile anachokiwaza.

2. Amefunga mziki mkubwa kwenye gari au nyumbani na anaupiga kwa sauti kubwa ili kila mtu asikie.

3. Anaishi kwa kutrend na fashion, kuanzia mavazi mpaka life style.

4. Mpenda sifa na umbea/udaku.

Kwa kifupi, watu wengi wanaojiona na kujitambulisha kuwa ni introvert sio maintrovert halisi, ni swaga tu.
 
Introvert wa JF mpoo! Unafahamu thamani ya uintrovert wako?

Kuwa introvert si ugonjwa. Nibaraka, lakini ukijitambua na kujikubali. Vinginevyo, unaweza ukawa sawa na mtu anayetaka kubadilishana kilo kumi za dhahabu kwa kuku kumi wa mayai! Hasara iliyoje!

Jamii yetu, kwa kutokufahamu, wamekuwa wakiwalaumu introvert kwa kutokuwa extrovert. Kuna wanaofikiria wana viburi,, wengine wanafikiri ni waoga, wengine wanawaona kama ni watu wanaojisikia, n.k. Hawajui kuwa wao ndiyo "wajinga", kwa kushindwa kujua utofauti wa maintrovert an extrovert.

Mungu, kwa nia njema kabisa, kaona vyema watu wawe na "personality" tofauti. Wewe unafikiri ingekuwaje kama dunia nzima ingekuwa ni ya maextrovert pekee? Au unafikiri ingekuwaje kama watu wote wangekuwa ni maintrovert?

Kama ambavyo Mungu kaamua kututofautisha, tuzikubali hizo tofauti na tuzitumie kwa manufaa. Wazazi wenye watoto maintrovert waache kuwalazamisha kuwa extrovert, badala yake wawasaidie kuvuna manufaa ya kuwa introvert.

Kwa wasiofahamu, kuwa introvert si ugonjwa. Ni namna ubongo unavyochakata taarifa zinazotumwa kwake. Kwamba, kiwango cha "dopamine" na muundo wa "dopamine receptors" kwenye ubongo ndiyo humtofautisha Introvert na Extrovert.

Tafiti za Kisayansi zinaonesha kuwa mtu anaweza kubainika kama ni introvert au extrovert akiwa na umri wa kuanzia miezi minne.

Kwa wasiojua, hizi ni baadhi ya tabia za Introverts:

~ Wakiamya

~ Wanapenda mazingira ya kuwa peke yao - hawafurahii mazingira ya mchanganyikeni

~ Wanapenda mazingira ya ukimya

~ Hufikiri kabla ya kuongea

~ Wana kawaida ya kuwa na marafiki wachache

~ Ni wasiri sana, n.k. (wengine wataongezea).

Baadhi ya watu maarufu ambao ni Introverts:
1. Warren Buffett
2. Mark Zuckerberg
3. Bill Gates
4. Steve Wozniak
5. Larry Page
6. Michael Jordan
7. Elon Musk
8. Charles Darwin
9. Mahtma Gandhi
10. Al Gore
11. Sir Isaac Newton
12. Rosa Parks
13. Eleanor Roosevelt
14. Abraham Lincoln
15. Barack Obama
16. Marissa Mayer
17. Guy Kuwasaki
18. Hilary Clinton
19.Michael Jackson
20. Brenda Barnes, e.t.c.

Nafikiri, na hawa Watanzania nao ni introvert: Dr. Mohammed Gharib Bilal, Dr. Ally Mohammed Shein, Dr. Philip Mpango, n.k.

Introvert, umebarikiwa kuwa introvert! Usitamani kuwa extrovert!

Extrovert, hakuna hasara kuwa Extrovert! Usiigize kuwa introvert!

Kila mmoja akae kwenye nafasi yake!!!
Mbona jina la Ally Kiba sijaliona hapo kwenye list ya introvert. Maana tunaambiwaga yeye hapendagi masifa na makiki!
 
Ni kweli kuna kasumba ya kuwachukia watu wanaojiita introverts hata kama wengine wanasema ukweli, ni kwa sababu introverts wengi husemekana wana akili sana na uwezo mkubwa wa kujenga hoja, kwahiyo tukiona mtu anajiita introvert moja kwa moja huwa tunahisi huyu anajaribu kutuambia kwamba ana akili na wabongo hatupendi kuona mtu anajisifia maana mtu wa aina hii tunamuona ni mjuaji

Mara nyingi wanaoitwa introvert ninawaonaga wajinga. Wasio na maarifa, wasiojua kujenga hoja, wasiojiamini,

Kwa sababu introvert Tabia yao kuu ni Ukimya.
 
Mara nyingi wanaoitwa introvert ninawaonaga wajinga. Wasio na maarifa, wasiojua kujenga hoja, wasiojiamini,

Kwa sababu introvert Tabia yao kuu ni Ukimya.
Introverts wako vizuri zaidi kwenye kuandika kuliko kuongea mkuu usisahau hilo na huko ndiko uwezo wao wa kujenga hoja unakoonekana

Wewe ndio unawaona wajinga kwa sababu ya chuki zako ulizonazo juu yao, ila wataalam wengi wa saikolojia wanasema introverts ndio wana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko extroverts, kundi la extroverts ndio lina wajinga wengi kuliko la introverts

Kuna mambo lazima tujifunze kuishi nayo na kukubaliana nayo, ukizingatia kwenye hii dunia kila character ina opposite yake dunia ina watu zaidi ya 8 Billion, hakuna character ambayo ni common kwa binadamu wote hawa na haitakuja kuwepo
 
👏👏👏🙏
 
Mara nyingi wanaoitwa introvert ninawaonaga wajinga. Wasio na maarifa, wasiojua kujenga hoja, wasiojiamini,

Kwa sababu introvert Tabia yao kuu ni Ukimya.
Ulichokosea ni kuishia kwenye mtazamo wako bila kufanya utafiti.

"Wenzako" huko "duniani" walianza na mtazamo kama wako, kisha wakachukua hatua ya kufanya utafiti hatimaye wakagundua kwamba mtazamo wao wa mwanzoni haukuwa sahihi.

Na kwa jinsi walivyo wakarimu, wameandika mpaka na vitabu ili kumsaidia kila "mjinga" anayetaka kuondokana na ujinga.

Inawezekana usiwe na muda wa kufanya utafiti, lakini hata kusoma utashindwa?

Si lazima ununue vitabu, unaweza kuvipakua mtandaoni "free of charge". Ni bando lako tu.
 
Umeandika kweli kabisaa,
Kuwa introvert au extrovert ni hali ya kiasili kabisa kama ilivyo kawaida kwa mwanaume kuota ndevu na mwanamke kuota maziwa.

Ni suala la kigenetic!

Umeshawahi kusoma kitabu chochote cha Kisaikolojia?

Nakushauri, fuata ushauri wa msomi fulani aliyesema, "no reference, no right to argue".

Kama umefanya utafiti ukagundua kuwa hao waliofanya utafiti wakagundua huo utofauti waliokosea, uiweke ushahidi wako humu. Humu kuna wanasaikolojia na wataalam wa ubongo.

Watachangia hoja yako kwa kujiunga mkono au kuipinga. Na kwa kuwa ni wasomi, hawataongea hisia zao, bali facts according to their findings.

Wanasema, "utafiti hupingwa kwa utafiti!" Hebu tuwekee na wewe wa kwako hapa.
 
Naona hapa unajisifia tu,unakuwaje Mwanasiasa halafu ni introvert.
Afu Elon Musk ana uintrovet gani au umeamua kuchukua matajili wote na kuwaweka katika hilo kundi.
1. Ninajisifia kwa lipi? Kuripoti kile wasomi wenye akili walichobaini kwenye tafiti zao? Mimi siyo neurosurgeon wala mwanasaikolojia, na wala sikushiriki kwa namna yo yote kwenye hizo tafiti zao, nina kipi cha kujisifia? Unaweza kuonesha chembe yo yote ya kujisifisu kwangu kwenye uzi husika?

2. Wasomi kadhaa wamethibitisha, si kwa maneno matupu bali kwa shahidi za kitafiti, kuwa wanasiasa kadhaa maarufu ni introvert. Miongoni mwao ni ABRAHAM LINCOLN, BARACK OBAMA, na HILLARY CLINTON. Wasomi waliosema hayo ni wa kule "duniani". Unaonaje na wewe ukitutoa Watanzania kimasomaso kwa kuwathibitishia kwa utafiti ulioufanya kuwa walikosea? Si unajua kuwa utafiti hupingwa kwa utafiti?

Fanya hivyo ili dunia ijue kuwa Tanzania ina wasomi wanaowazidi weledi Wazungu na Wahindi walioshindwa kujua kuwa introvert hawezi kuwa mwanasiasa, kama "ulivyogundua" wewe.

3. Si mimi niliyesema Elon Musk ni Introvert. Ni yeye mwenyewe, pamoja na wasomi kadhaa. Kwa kuwa wewe unamfahamu zaidi kumzidi yeye mwenyewe anavyojifahamu, na hao wasomi waliodai ni introvert, ulete na wewe matokeo ya utafiti wako (si maoni wala hisia), bali ya Kisayansi, ili kuwakosoa Kisayansi na si kwa maneno matupu.

4. Matajiri wote? Unamaanisha akina Dangote, Strive Masiyiwa, Mohammed Dewji, Bakressa, Rostam, na Manji?

Ili iweje? Itanisaidiaje?

Tafadhali usinihukumu kwa kuwa nimeandika ukweli kwa mujibu wa yaliyoandikwa.

Na wala sijasema kama mimi ni introvert au extrovert, na sina haja ya kusema. Kama wewe ni introvert, usikasirike kwa kuwa jina lako halijajumuishwa kwenye huu uzi. Labda mtu mwingine anaweza akakuandika na wewe wakati mwingine.

Na hata kama ni extrovert, usiwaonee wivu wale waliojaliwa kuwa introvert. Hawana ulicho nacho, kama ambavyo na wewe huna walicho nacho. Ridhika na ulichojaliwa🙏🙏🙏
 
Unaweza kukuta ile account zake za mitandaoni anaendesha mtu mwingne on behalf. Yeye yuko zake busy huko kwingne hana habari.
Very possible! Huenda hata ikawa inaendeshwa na marobot.

Inasemekana yupo busy sana, wakati mwingine analala ofisini kwake.
 
Ktk jamii za watanzania, introvert anapitia wakati mgumu Sana
Tangu akiwa mtoto wazazi wanamnyanyasa kwa kumuita lofa, zoba, kiburi na majina mengine

Shuleni wanafunzi wenzake wanamdharau Sana
Waalimu wanamdharau pia, wanamuona mtu aliyezubaa Sana!
Waalimu na wazazi wanampa pressure Sana,, "We vipi acha kuzubaa, changamka"

Kwenye kupendekeza uongozi, introvert ananyimwa kila posti,

Ila pamoja na hulka zao za upole, anapoonewa ikifika zaidi ya uvumilivu wake, Hawa jamaa wako vizuri kwenye kutoa vipigo kwa maextrovert!
Kuna ule msemo, watu wakimya usiwachokoze!

Hawanaga uwezo wa kujitetea kwa maneno!

Inapofika wakati wa kupata mke, Hawa jamaa wanapata tabu Sana, kwakuwa wanawake wengi hawawapendi watu wakimya,
Mara nyingi huishia kupata wanawake second class au third class

Hawa jamaa wanajua Sana kuvumilia maisha ya ndoa! Ni ngumu Sana kuwatupa wapenzi wao! Kwa mantiki hio Hawa si wazalishaji wa single mamaz!

Kwenye issue za kazi Hawa Ni wachapa kazi! Ingawa wanapigwa bao Sana na maextrovert kwenye interviews
Hawa wanatoboa vizuri kwenye issue za ufundi, kilimo, Sanaa, uandishi, sayansi na utafiti, kuliko maextrovert
Ukienda hospitali ukamkuta doctor Hana maneno mengi furahia
Ukienda garage ukamkuta fundi Hana maneno mengi furahia

Kiukweli Introvert Ni mtu na nusu Ila maisha yao yanapitia changamoto Sana hususani za kudharauliwa!
 
Mkuu, wanaoweza kuwadharau introvert ni "wajinga". Lakini wenye akili wanawathamini sana. Wanajua Wana hazina nzuri.
 
Introverts wako vizuri zaidi kwenye kuandika kuliko kuongea mkuu usisahau hilo na huko ndiko uwezo wao wa kujenga hoja unakoonekana

Wewe ndio unawaona wajinga kwa sababu ya chuki zako ulizonazo juu yao, ila wataalam wengi wa saikolojia wanasema introverts ndio wana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko extroverts, kundi la extroverts ndio lina wajinga wengi kuliko la introverts

Kuna mambo lazima tujifunze kuishi nayo na kukubaliana nayo, ukizingatia kwenye hii dunia kila character ina opposite yake dunia ina watu zaidi ya 8 Billion, hakuna character ambayo ni common kwa binadamu wote hawa na haitakuja kuwepo
Umemjibu vizuri sana..bila jazba wala maneno machafu kama aliyoyatumia yeye.
 
Tabia ya ukimya ipo kama ugonjwa na vingi ndani.......
Ukimya wa extrovert huhesabiwa kuwa ni hekima.

Lakini introvert kukaa kimya ni asili yake. Haimaanishi kuwa hawezi kuongea, hapana. Anaongea, tena sana tu, kukiwepo na uhitaji huo.

Introvert huongea kunapokuweko na uhitaji wa kuongea, na hukaa kimya kama hakuna sababu ya kuongea.
 
Back
Top Bottom