Kikubwa kufika salama,, uzuri nakerwa sana nikishuka yameisha ila km mliniudhi sana siwarudii,, sasa usiombe uwe unaenda vijijini ndani huko magari ya huko ndo balaa kamili acheni haya ya kupita barabara kuu na yanaoishia makao makuu ya mikoa,, Tanzania tuna shida nyingi sana acheni tu, nimezunguka mikoa mingi kiasi chake nchi hii, CCM Mungu anawaona aisee
Basi zuri na huduma nzuri ni Asante Rabi luxury Arusha-Mwanza,, sitawasahau hawa watu mkinisoma hapa msibadilike jameni,, safari yangu ile nilitamani tusifike yani ilikuwa raha juu ya raha, basi zuri na safi, lugha nzuri wahudumu wasafi mdada mzuri hana kitambi anaongea km anabembeleza, (ningekuwa dume ningetupa ndoano) mwendo poa, makulaji yao sasa full burudani, filamu za kijanja sio za kichina na mkojani