Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Kikubwa kufika salama,, uzuri nakerwa sana nikishuka yameisha ila km mliniudhi sana siwarudii,, sasa usiombe uwe unaenda vijijini ndani huko magari ya huko ndo balaa kamili acheni haya ya kupita barabara kuu na yanaoishia makao makuu ya mikoa,, Tanzania tuna shida nyingi sana acheni tu, nimezunguka mikoa mingi kiasi chake nchi hii, CCM Mungu anawaona aisee

Basi zuri na huduma nzuri ni Asante Rabi luxury Arusha-Mwanza,, sitawasahau hawa watu mkinisoma hapa msibadilike jameni,, safari yangu ile nilitamani tusifike yani ilikuwa raha juu ya raha, basi zuri na safi, lugha nzuri wahudumu wasafi mdada mzuri hana kitambi anaongea km anabembeleza, (ningekuwa dume ningetupa ndoano) mwendo poa, makulaji yao sasa full burudani, filamu za kijanja sio za kichina na mkojani
 
Iyo chuma ndio uifumanie siku iyo hAizingui mbona utakuwa unalipanda kila siku........masaa ya mbele iyo inaitwa
 
Kwasababu zakibiashara na huenda sasa hivi wamebadilika hivyo sitawataja, wanabrand ya rangi Blue na ofisi zao pale Shekilango..hawa watu walitutoa Ubungo saa sita mchana kwenda kahama badala ya saa 12 asubuhi.
Dar lux
 
Yoote kwa yote wakuu msije mkajikologa mkapandia njiani alafu upande bus lenye siti za 3/2 hapo umeingia njoo cha kiume fikoshi ni kampuni ambayo sitoisahau aisee gari ya mwanza.

Inaenda mbeya nilipandia misigiri konda alinipa ndoo nikalie kwa hasira nilikataa kukalia.....
Nilisamama nikaja kupatia siti dodoma bus kwanza
Linanuka maarufu ya ajabu ajabu siti zimeisha yani kama umekalia chuma tupu maana body lake..
Nilakuchongea joto kama lote tuliingia mbeya..

Saa 10 alfajiri tangu siku hiyo nimekoma kukatia
Ticket kwa wapiga debe ni heri nikalale stendi..
Asubui nipande bus la moja kwa moja.
 
Kuna saratoga DKB AKA sukari yao, dereva alikuwa anapiga mashine mpaka walimfungia

Sent from my CLT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Kampuni ya Sai baba bado nipo? Kwa kweli at their prime, ilikuwa ni kampuni nzuri na marcopolo zao zile wakati ule ndiyo fashion
Ipo mkuu imebakia moja nilipanda inatokea swanga - dar ila ndani siti zimechoka yani ukipanda ukifika dar lazima ukajikande mgongo Na diclopar iusike
 
Kwanza majinja body lake ni la kuchongea pia injini ni za scania mkuu[emoji16]
 
Arizona DAR - KIGOMA
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wanaolijua watanisaidia kuelezea sifa zake.
Dah hili bus nikiwahi kumpakia manzi yangu analudi kwake kahama si likazingua njiani[emoji81][emoji38] daah kahama walifika saa 8 usiku.
 
Luwinzo ..njombe ..dar humo tulipanda na bata mbuz na watu wamekaa kwenye vindoo Kama siti


Princess muro arusha ..dar sitasahau tulitoka arusha saa tatu dar tuliingia saa kumi alfajir
[emoji16][emoji75][emoji81]
 
[emoji16][emoji75] kuna bus ukiliona tu kwa nje unajisemea hapa hamna gari
 
Ally's Mwanza - Dar. Ile safari sitakaa niisahau, gari ilikua imepulizwa Manukato flani yaliyokua yanatoa harufu mbaya sana yani nilikereketwa mwanzo hadi mwisho wa safari, nilipata tabu sana, nilifika Dar nikiwa hoi bin tahabani
Allys star zinazotamba saivi ni mbili kuna allys nyuma imeandikwa last card na ile nyuma imeandikwa rockcity zinatoka dar kama unataka kuwahi kufika panda izo ni zinatembea balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…