Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Halafu Sijui huwa wanaambizanaga jamani…yani %98 kwenye mabasi huwezi kukosa movie za mkojan
Mm huwa nahisi wanaweka kwa dj mmoja[emoji1787][emoji1787],mfano mabasi yote ya Arusha Dar nyimbo zimefanana filamu aina moja,basi nililipanda nikaenjoy ,,,,,,[emoji23],hamuwezi amini nimelisahau jina,yaan nilienjoy kinoma walikuwa wanapiga miziki ya R&B na slow jam za maana,,,nimelikumbuka bus lenyewe ni Kidia One bus luxury saana
 
Daah manina back 2010 nilikuwa dodoma nikawa na safari ya haraka mida ya saa 8 mchana, chaap kurudi dar, sina gari binafsi nikazama kituoni pale nyuma ya shabiby nikakutana na chuma imetoka singida jamaa kanikatisha ticket mapema kashasepa

Baada ya gari kufika nimepanda kwa kweli nipata chafya pale pale, nkasema hapa natoboa hivi hivi, daah naenda kwenye siti yangu, konda akaniambia huku hamna cha mambo ya siti subiri mtu akishuka ukae, baada ya ku mind sana na kutaka kuleta ubabe abiria kadhaa wakasema wanashuka soon...

Lile gari lilikuwa linanuka harufu ya mavi ya kuku, na mbuzi, kelele mtindo mmoja, siti za chuma viti cushions zimezama kwa chini unazama ukikaa, aisee nilipata tabu sana mnaishi na kuku na mbuzi ndani ya bus, ilibidi niombe msaada kwa shangazi yangu pale gairo akanipa rav 4, yake nikawahi nilicholuwa ninawahi maana gari lenyewe lilizingua kabla hatujafika gairo namsikia konda anasema hapa mbombo ngafu[emoji28]...nkajua hii hatutoboi

Ya pili, nilitoka dsm kwenda dodoma 2009 nikapanda gari flani linaonekana Luxury sana hawa jamaa walikuwa na ma bus yao pale makonde mbezi beach ya kisasa wameyatoa ulaya, daah nilitumia masaa 17...kila baada ya kilometres kadhaa gari inachemsha [emoji23]

Kwa safari zangu za bus ni kilimanjaro na shabiby, i tried al saedy, dar lux na kidia ila hawa kwa sasa hivi nikikosa seat ni afadhali niruke na ungo
 
Mm huwa nahisi wanaweka kwa dj mmoja[emoji1787][emoji1787],mfano mabasi yote ya Arusha Dar nyimbo zimefanana filamu aina moja,basi nililipanda nikaenjoy ,,,,,,[emoji23],hamuwezi amini nimelisahau jina,yaan nilienjoy kinoma walikuwa wanapiga miziki ya R&B na slow jam za maana,,,nimelikumbuka bus lenyewe ni Kidia One bus luxury saana
Haujawahi kupanda mabasi ya mwanza ee😂😂movie za mkojani hazijawahi kukosekana.
Kwa mabasi niliyoyapanda kwangu yote ni mazuri kwa safari.
Tanzanite kabla hazijaamia mbeya,Ally’s no 1,Zuberi na mwisho ni Travel Partners yote haya kwangu ni mazuri sana tatizo ni movie za mkojani tu kha
 
Back
Top Bottom