Nahisi ilikua ni mwaka 2012 december. Natokea Moro naenda Moshi, hapo abiria wameanza kuwa wengi kama kawaida kwa kipindi hicho.
Mida ya saa moja kasoro naingia msamvu kwa madaha yote, ila hakuna hata mpiga debe anae hangaika na mimi maana basi zimejaza na wanajua wewe abiria ndo utawanyenyekea wakutafutie usafiri kwa gharama karibia mara mbili ya gharama halisi.
Kuhangaika kutafuta usafiri mle ndani tangu mida ya saa moja hadi saa tatu kasoro sija ambulia hata mlio wa gari inayoenda Moshi. Basi kuna mwana akanitonya pale kwamba kuna basi la 'Hood' ipo njiani kutokea Kilombero inaenda Arusha na pale msamvu ingepita saa tatu na nusu. Nikabonga nae pale akanipa ticket kwa elfu 35, kipigo cha kwanza hicho.
Nimekaa pale stendi kidogo tu kama saa tatu na robo chuma kimeingia kwa mbwembwe sana pale, nikajisemea kimoyo moyo "mambo si ndo hayo sasa, Mapema tu". Kumbe najidanganya mweeh. Tumetoka msamvu saa nne kamili kuanza kuitafuta kanda ya kaskazini. Kufika mikese nimeuchapa usingizi, chuma kinapepea tu, kufika msolwa njia panda ya msoga pale ngoma likazingua, likazima kabisa. Kidogo nasikia dereva anamwita jamaa alikua kakaa siti ya nyuma "oyaa uwanja wako dude limetaga hili', dah kumbe basi ndani linatembea na fundi! Jamaa alieitwa kaja pale mbele na mkoba wenye spana size zote. Abiria tumeshuka, basi likaanza pigwa spana mara nyundo mara lete kamba, funga hapa vuta kuelekea kule. Kwenye saa sita mchana, dereva katekenya switch, jino moja tu Scania ikanguruma kama simba dume. Dereva ame rev kwa mbwembwe za kutosha pale na ule mngurumo sie wapenda magari tukawa tunatabasamu tu, tukawa tumesahau kidogo muda tuliopoteza pale.
Safari ikaendelea basi linajivuta mdogo mdogo, mngurumo wa simba mwendo kama wa kobe, tabu tu. Kufika kabuku pale, moshi unatokea pale kwenye bonnet, tukajua disco limeingia mmasai na panga lake. Ikawekwa pembeni tukashuka mbio mbio wakina mama wameanza kukumbuka Mungu wao awasemehe maana walijua linawaka moto. Kumbe mzigo ulikua umeanza kuchemsha. Tukatulia marekebisho yakaendelea pale. Kwenye saa nane au tisa hivi tukaanza safari tena.
Mashine imetembezwa si mchezo. Kwa hesabu zangu nikajua Moshi saa nne usiku nashuka stendi pale. Kumbe najipa moyo tu. Tunapita pale liverpool Mombo saa 12 jioni, hakuna kuchimba wala kufukia dawa, ni mwendo kibati tu. Muda si muda giza limeshaingia, sie tulokaa mbele tukastuka mbona suka hawashi taa! Kumbe Scania letu haliwaki taa zinawaka kwa kujisikia bana dah. Zinawaka unatembea baada ya muda zinazima ghafla tu.
Dereva mbishi kinoma tumenyata mdogo mdogo, nimeingia Moshi saa nane usiku. Ndo mara ya mwisho nimepanda Hood.