stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,216
- 26,225
Niliwahi kupanda Bus moja lilikuwa linaitwa Buffalo hili lilikuwa lina kwenda kama sio Arusha ilikuwa Moshi maana nilipandia Dar kwa kushukia Hedaru,lile basi lilikuwa linakimbia ajabu na ukichukulia miaka ile kulikuwa hakuna speed govenor ilikuwa ni hatari,nakumbuka kwenye makona lilikuwa linalala mpaka unasikia kama kuna bolt na nuts zinakatika,kufika maeneo ya Mombo ile basi likaacha njia tukaingia kwenye mashamba ya katani,bahati yetu lile eneo lilikuwa ni tambarare hakuna aliyepatwa na umauti zaidi ya majeraha madogo madogo...