Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapuuzi sanaNi bus linaitwa city boys ndo walifanyaga huu mchezo.
Hao allys juzi walikalishwa na jmcIla kiukweli usafiri mzuri na wa haraka dar to mwnza ni ally's star hawana mambo ya kupotezeana muda.. naipenda sana hiyo kampun nikikosa kwao kwenda rock city bora nihairishe.
Zile dragon zimebakia kupaa tu aisee zinatembea kweli kweli.
Najua kuna watu watakuja hapa kuongolea mambo ya kupata ajali kisa mwendo hayo ni ya kwenu ajali haina kinga .
La petroleum ni [emoji91][emoji91]Allys zamoto ni nyingi tuu
Kuna city hunter hii hadi ilipta ajali ikarudi kukaww na ginimbi pia enzi izo kulikuwaga na DRG aka La petrol hili ndo balaa, nyingine zinatambulika kwa nmba tuu achana n hizi DX Series
Nilishakutana nao wapuuzi sana nikapanda happy nation tukafika mbeya saa sita usikuWanafanya hivyo ili ulipie zaidi.
Ila kwanini sura kama jembe lakini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Happy nation ya mbeya jamani yani mnafika makambako saa 3 kuelekea 4 usiku dahKuna mabasi ya aina tofauti kutegemea umri yako ya vijana huenda spidi ya mwewe yako ya watu wa makamo na wazee
Hilo happy nation la Mbeya ni kwa ajili ya wazee ulijichanganya ungepanda Sauli
Kama wewe kijana panda happy nation ya kwenda Bukoba uone mziki wake ndio huwa la kwanza kufika Bukoba toka Dar
Yani kama daladala kila kituo konda anashuka chini ya gari kugonga gonga .majanga sanaHamna gari humo
Nilianza kupanda Asante Rabi mwaka 2018 baada ya kuwakimbia Mghamba Express, mghamba wana basi Lao lenye mlango katikati lilikuwa bovu sana.Kikubwa kufika salama,, uzuri nakerwa sana nikishuka yameisha ila km mliniudhi sana siwarudii,, sasa usiombe uwe unaenda vijijini ndani huko magari ya huko ndo balaa kamili acheni haya ya kupita barabara kuu na yanaoishia makao makuu ya mikoa,, Tanzania tuna shida nyingi sana acheni tu, nimezunguka mikoa mingi kiasi chake nchi hii, CCM Mungu anawaona aisee
Basi zuri na huduma nzuri ni Asante Rabi luxury Arusha-Mwanza,, sitawasahau hawa watu mkinisoma hapa msibadilike jameni,, safari yangu ile nilitamani tusifike yani ilikuwa raha juu ya raha, basi zuri na safi, lugha nzuri wahudumu wasafi mdada mzuri hana kitambi anaongea km anabembeleza, (ningekuwa dume ningetupa ndoano) mwendo poa, makulaji yao sasa full burudani, filamu za kijanja sio za kichina na mkojani
Wako vizuri mno yaniNilianza kupanda Asante Rabi mwaka 2018 baada ya kuwakimbia Mghamba Express, mghamba wana basi Lao lenye mlango katikati lilikuwa bovu sana.
Nikahamia Asante Rabi, kwa kweli hii kampuni kwenye customer care wanajitahidi kwa uzoefu wangu; Wanajitahidi kwenda na muda, Wana app kwenye simu ya kuchagua siti na kulipia sio lazima kwenda ofisini. Imagine nilikuwa nalipanda kila baada ya wiki tatu go and return kwa miaka 4.
Golden dragonMabus yao mengi bi higer
unachanganya facts...Kampuni unayoisema wewe inaitwa City Boy...enzi hizo Dar Kahama ndiyo gari zao ziligongana kwa huo mchezo wa kubadilishana lanes. City Boy au Super Video yupo mpaka leo hajabadili jina, for now anaenda Dar Karagwe, Kahama aliacha.Ivi kisbo sindo ili gali kipindi cha nyuma walikuwaga wakikutana salamu yao wanapishana wakulia anahamia kushoto kushoto anahamia kulia sasa siku moja akatokea alikuwa dereva ni mgeni hajui salamu za wenzie.
Jamaa kukalibiana dereva mzoefu akampigia..
Pass wapishane kama salamu yao ilivo kawaida yule dereva mgeni akaludisha pass akajua anasalimiwa maana kampuni ni moja kusalimiana muhimu sasa maana ya pass kwao ilikuwa wanamaanisha wa exchange njiaa dereva mzoefu akalileta kama kawa jamaa walikutana uso kwa uso babaaake jina la hii kampuni zamani sijui lilikuwa linaitwaje baada ya kukaa mda mrefu ndo wakabadili usajili wa jina wakaja na hii kisbo.
Nilichanganya mafileunachanganya facts...Kampuni unayoisema wewe inaitwa City Boy...enzi hizo Dar Kahama ndiyo gari zao ziligongana kwa huo mchezo wa kubadilishana lanes. City Boy au Super Video yupo mpaka leo hajabadili jina, for now anaenda Dar Karagwe, Kahama aliacha.
Kisbo wameanza kabla ya City boy hapo Kahama na wapo mpaka leo. Kisbo na City boy hazihusiani kibiashara.