Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

SAIBABA,
Nilikua nasafiri kutoka dar kwenda arusha kwaajili ya interview, safari jumapili interview jumatatu,

nilikata tiketi siku mbili kabla ya safari, siku ya safari nafika stand wananiambia gari yangu imeondoka wananipa gari nyingine ya saa mbili, kumbe gari halijaondoka ila lilikua halijajaza, nimekaa kwenye gari hadi saa8 mchana ndio inatoka wakasema ata kama saa6 usiku lazima tuingie arusha siku iyoiyo,
mwendo tuliokua tunaenda njiani kama msafara wa msiba wa malkin Elizabeth
Tunafika same saa6 usiku dereva na konda wakatuacha kwenye gari wakaenda kulala wanapojua wao wanarudi saa2 asubuhi jumatatu, tunaingia arusha saa6 mchana nikafika hadi sehemu tuliyotakiwa kufanya interview nimechelewa na watu wote wameondoka ilikua chuo cha uhasibu arusha.
Iyo safari sitaisahau na SAIBABA sitalisahau.
Saibaba washawahi kunikatisha tiketi kwenye basi lao zuriii chuma iko inaunguruma tunasubiria saa 12 ifike tuanze safari, mara tukashushwa wanasema dereva sijui hayupo, tukapelekwa kwenye saibaba lengine bovu lilikuwa sijui linaenda Songea aisee gari imejaa mende na kunguni, inapakia abiria kama daladala kila kituo inasimama, ndoo kama zote ndio nikajua kumbe hizi ndoo ni seats pia.

Kilichoniuma niliacha Chaula mpya nikasema nibadili upepo halafu kwa nauli ileile nikasafirishwa na gari bovuuu limejaa kunguni na hata pipi hatukupewa. Na bado niliposhushwa ilibidi nichukue boda tena mpaka nyumbani wakati ningepanda Chaula ingeniacha mahali ambapo ningetembea kwa mguu tu nisingeingia gharama za boda.

Na huo ndio ukawa mwisho wangu kupanda saibaba. Yani kuna makampuni nimeya blacklist ikiwemo saibaba.
 
Saibaba nzuri zimebaki 5 Tu nafikiri
 
Basi zote zinakuwaga nzuri mwezi wa 12 mwishoni na wa kwanza ile wiki ya kwanza. Hasa route ya kaskazini. Hata ile al hushoom ni nzuri kipindi hicho tu[emoji1]
Mkuu watu inabidi wafahamu hakuna mmiliki wa bas atakubali anunue brand new busses alafu aweke route ndefu mfano kigoma,bukoba nk angalia abood zile mpya alizo ingiza mwaka Jana zote kaziweka dar-moro hataki zichollke halaka Sasa zile choka mbaya ndo kapeleka maroute malefu tafuta route ndefu ndani ya nchi ukikuta kampuni Ina bus mpya luxury safi ni bahati
 
Mkuu watu inabidi wafahamu hakuna mmiliki was bas atakubali anunue brand new busses alafu aweke route ndefu mfano kigoma,bukoba nk anaglia abood zile mpya alizo ingiza mwaka Jana zote kaziweka dar-moro hataki zichollke halaka Sasa zile chiloka mbaya ndo kapeleka maroute malefu tafuta route ndefu ndani ya nchi ukikuta kampuni Ina bus mpya luxury safi ni bahati
Songea - Mwanza, Songea- Arusha & Songea- Dar (Super feo tena ni Zongtong)

Dar - Kigoma Aifola(Higer & kinglong mpya kabisa)!

Dar - Bukoba Travel partner, Frester & Happy nation wanapeleka magari mapya kabisa!!
 
Abood. Mwanza to Dar.

najuuuta kusafiri na hawa jamaa😅😅😅

Tuliondoka Mza Saa 12 asb tukafika Bongo kesho yake saa 11 alfajiri.

kipindi kile korona inaanza.

Nashukuru Mungu ndio nikapata nafasi ya Kumuona JIWE live pale Ubungo fly over na akapotea mazima kwenda Chato
 
Abood. Mwanza to Dar.

najuuuta kusafiri na hawa jamaa[emoji28][emoji28][emoji28]

Tuliondoka Mza Saa 12 asb tukafika Bongo kesho yake saa 11 alfajiri.

kipindi kile korona inaanza.

Nashukuru Mungu ndio nikapata nafasi ya Kumuona JIWE live pale Ubungo fly over na akapotea mazima kwenda Chato
Yani mmetumia siku Moja na saa 1
 
Basi lenyewe linaitwa COMPLEX sijui kama bado yapo. Kisa chenyewe kilikua hivi, nilikua nimekata Green star miaka ya 2013 hapo, miaka hiyo ndo zamoto na ile luck star, bahati mbaya nikachelewa kufika ubungo nilikua natokea azizi Ali hapo ila nilikesha Bar na manzi nikarudi kulala saa tisa nikasema nijiegeshe kidogo, manzi akasema ataniamsha asubuhi aniwahishe ubungo na usafiri wake ...asalaleee ile nimeulaza nakuja kushtuka jua kali kinoma nikajua tu hii Lamasaba Kitan imetimia, nikashtuka bed, nacheki time saa moja unusu manzi anakoroma kishenzi moyoni nikajisemea huyu mlevi ndo alisema ataniamsha nikacheka tu mwenyewe. Basi mtu mzima nikajiweka sawa chap chap nikaita boda hadi ubungo nia yangu nidake champion ya Dom ile ya saa mbili nusu hadi saa tatu afu nikifika dom ningepata ya Mwanza kiconnection, ila MUNGU jaalia wakali wakaniambia kuna chuma ya Mwanza inaitwa complex ilitaga Mbagala inapopaki kwa hiyo kama niko tayari niidake saa sita makini tupo Mwanza,nikasema sio kesi sh ngap wakali wanataka 40 nikasema kwa basi hili 40 sitoi nikawachapa 30 nikakwea chuma. Picha linaanza mpaka saa nne ngoma haijachomoka Ubungi abilia ndo kusala mixer kuwaita matrafiki, jamaa wakatupooza kwamba kuna mkwaju wa krachi wanaweka sawa ngoma ikianza Mwanza nikugusa, huwezi amini tuliondoka Dar saa sita kasoro ***** kabla hatujaingia Dom ngoma ilitaga tena...Dom tuliingia Saa nne, usiku humo ndan hamlaliki gari ina kunguni afu uvundo kinoma.....Tulifika Shinyanga kesho saa mbili asubuhi sita sahau ilibidi nishuke nidake costa Mwanza nikaingia saa sita, mchongo ulikua saa saba niliuwahi ila nilijuta nilikua naumwa kila sehemu

Lile basi sitapanda hata kwa dawa
 
Mkuu watu inabidi wafahamu hakuna mmiliki was bas atakubali anunue brand new busses alafu aweke route ndefu mfano kigoma,bukoba nk anaglia abood zile mpya alizo ingiza mwaka Jana zote kaziweka dar-moro hataki zichollke halaka Sasa zile chiloka mbaya ndo kapeleka maroute malefu tafuta route ndefu ndani ya nchi ukikuta kampuni Ina bus mpya luxury safi ni bahati

Inategemea na nature ya route Na biashara yake. Happy nation ananunua bus na anapeleka dar bukoba ni mbali zaidi. Baraka classic anapeleka mpya dodoma mtwara
 
Basi lenyewe linaitwa COMPLEX sijui kama bado yapo. Kisa chenyewe kilikua hivi, nilikua nimekata Green star miaka ya 2013 hapo, miaka hiyo ndo zamoto na ile luck star, bahati mbaya nikachelewa kufika ubungo nilikua natokea azizi Ali hapo ila nilikesha Bar na manzi nikarudi kulala saa tisa nikasema nijiegeshe kidogo, manzi akasema ataniamsha asubuhi aniwahishe ubungo na usafiri wake ...asalaleee ile nimeulaza nakuja kushtuka jua kali kinoma nikajua tu hii Lamasaba Kitan imetimia, nikashtuka bed, nacheki time saa moja unusu manzi anakoroma kishenzi moyoni nikajisemea huyu mlevi ndo alisema ataniamsha nikacheka tu mwenyewe. Basi mtu mzima nikajiweka sawa chap chap nikaita boda hadi ubungo nia yangu nidake champion ya Dom ile ya saa mbili nusu hadi saa tatu afu nikifika dom ningepata ya Mwanza kiconnection, ila MUNGU jaalia wakali wakaniambia kuna chuma ya Mwanza inaitwa complex ilitaga Mbagala inapopaki kwa hiyo kama niko tayari niidake saa sita makini tupo Mwanza,nikasema sio kesi sh ngap wakali wanataka 40 nikasema kwa basi hili 40 sitoi nikawachapa 30 nikakwea chuma. Picha linaanza mpaka saa nne ngoma haijachomoka Ubungi abilia ndo kusala mixer kuwaita matrafiki, jamaa wakatupooza kwamba kuna mkwaju wa krachi wanaweka sawa ngoma ikianza Mwanza nikugusa, huwezi amini tuliondoka Dar saa sita kasoro ***** kabla hatujaingia Dom ngoma ilitaga tena...Dom tuliingia Saa nne, usiku humo ndan hamlaliki gari ina kunguni afu uvundo kinoma.....Tulifika Shinyanga kesho saa mbili asubuhi sita sahau ilibidi nishuke nidake costa Mwanza nikaingia saa sita, mchongo ulikua saa saba niliuwahi ila nilijuta nilikua naumwa kila sehemu

Lile basi sitapanda hata kwa dawa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] daaaah noma
 
Back
Top Bottom