Basi lenyewe linaitwa COMPLEX sijui kama bado yapo. Kisa chenyewe kilikua hivi, nilikua nimekata Green star miaka ya 2013 hapo, miaka hiyo ndo zamoto na ile luck star, bahati mbaya nikachelewa kufika ubungo nilikua natokea azizi Ali hapo ila nilikesha Bar na manzi nikarudi kulala saa tisa nikasema nijiegeshe kidogo, manzi akasema ataniamsha asubuhi aniwahishe ubungo na usafiri wake ...asalaleee ile nimeulaza nakuja kushtuka jua kali kinoma nikajua tu hii Lamasaba Kitan imetimia, nikashtuka bed, nacheki time saa moja unusu manzi anakoroma kishenzi moyoni nikajisemea huyu mlevi ndo alisema ataniamsha nikacheka tu mwenyewe. Basi mtu mzima nikajiweka sawa chap chap nikaita boda hadi ubungo nia yangu nidake champion ya Dom ile ya saa mbili nusu hadi saa tatu afu nikifika dom ningepata ya Mwanza kiconnection, ila MUNGU jaalia wakali wakaniambia kuna chuma ya Mwanza inaitwa complex ilitaga Mbagala inapopaki kwa hiyo kama niko tayari niidake saa sita makini tupo Mwanza,nikasema sio kesi sh ngap wakali wanataka 40 nikasema kwa basi hili 40 sitoi nikawachapa 30 nikakwea chuma. Picha linaanza mpaka saa nne ngoma haijachomoka Ubungi abilia ndo kusala mixer kuwaita matrafiki, jamaa wakatupooza kwamba kuna mkwaju wa krachi wanaweka sawa ngoma ikianza Mwanza nikugusa, huwezi amini tuliondoka Dar saa sita kasoro ***** kabla hatujaingia Dom ngoma ilitaga tena...Dom tuliingia Saa nne, usiku humo ndan hamlaliki gari ina kunguni afu uvundo kinoma.....Tulifika Shinyanga kesho saa mbili asubuhi sita sahau ilibidi nishuke nidake costa Mwanza nikaingia saa sita, mchongo ulikua saa saba niliuwahi ila nilijuta nilikua naumwa kila sehemu
Lile basi sitapanda hata kwa dawa