Ni biashara gani ambayo huelewi faida wanapata vipi?

Ni biashara gani ambayo huelewi faida wanapata vipi?

Madereva TAKS hapa Town poster mpaka feri , hivi muna pata faida Gani, maana muda mwingi huwa muna piga story, alafu wengi wenu ni wazee ukiuliza alikuwa mjeda amesfaafu,
AU ni wazee wa kitengo [emoji23]
Wale wengi wana wateja wao. Anaweza kufanya trip mbili kwa siku akaingiza 50 au 60 akafunga kazi saa 9 akaenda kulala.
Kuna jamaa mmoja ana wateja wake kama 10 hivi so kwa siku akibeba wawili kamaliza. Mmoja mdada ni mhasibu wa kampuni flan namfahamu akienda bank na kumrudisha 30k kuna nn tena hapo.
 
Anatakiwa kupata FAIDA? 😳
Hatimaye umejitpkeza mkuu.

Kuna umuhimu wa kujua jinsi unatengeneza faida.Inaweza Kuna Kizazi kipya Chenye mawazo ya initiative kama hii au zaidi ya jamii forums, wanajiuiliza watafanikishaje ndoto zake.

Mana mwisho wa siku lazima mkono uende kichwani,lazima mwili ufunikwe na namba na lazima kichwa kilale kwenye mto.
 
Ujenzi wa maghorofa makubwa ya biashara na ofisi,wanapataje faida...?
-Ujenzi una gharimu mabilioni.
-uendshaji wa Majengo unahitaji mamilioni
-Kodi zao zipo juu
-Majengo mengi hata nusu ya floor zote zipo wazi.
Kuna biashara ni nzuri kufanyia kufichia au kutakatisha pesa, sio kila biashara za watu ni kwa ajili ya kupata faida katika kipindi cha muda mfupi.
 
Biashara ya mama/baba ntilie wanapataje faida hii biashara siielewi mfano mdogo tu wa mboga, samaki ukienda sokoni ni elfu 5 mpaka elfu 10 lakini kwa mama/baba ntilie wali samaki unakuta elfu 2 au 3 wanapataje faida? Hapo haujapigia hesabu ya mafuta na viungo pamoja na mboga mboga
 
Nakazia hapa , Kuna rafiki yangu alifungua biashara ya nguo zile classic.yaani kwa week anaweza asiuze hata nguo moja na Kodi ya frame ni laki 2 ,mwisho wa siku alifunga biashara akaanza kuvaa mwenyewe.
Mie rafiki angu ana frem kkoo, ni zile ndogo ndogo, anauza vyupi, boxa vest.....anaenda kufata mzigo kule maduka ya jumla ambako vyupi 3 ni 9000 ye anauza 10000. Faida 1000

Ndo najiuliza hapo apate kodi laki na nusu, mshahara wa muuzaji laki na nusu, nauli ya kuja shop, msosi.....na mambo mengine 🤔🤔
Na kuna kipindi aliunganisha frem mbili kodi laki tatu

Niseme tu biashara zina siri
 
Back
Top Bottom