Watu wa ajabu sana! Elf 8 au 7 kwa siku, Mtaji shilingi 2,400,000..
Hizi ni akili za kilemavu..
Muuza mishikaki anauza stick 100 kwa siku..
Bei ya stick moja ni 200.
Jiko ananunua 25,000
Nyavu 3000
Chumvi 500
Pilipili 1000.
Stick moja ya chuma 200.
Nyama 7,000.
Na anapata 20,000 kwa siku..
Ukitoa matumizi anabaki na 10,000 faida... Anazidi hiyo bodaboda kwa mtaji wa 40,0000 tu...
Aya tuje kwenye mayai ya kuchemsha.
Trei 6,500
Mkaa 1,000
Maji ya kuchemshia 100.
Chumvi 500.
Kwa uuzaji wa kutembeza mtu kiwango cha chini huuza trei 3mpaka 4 kwa siku..
Bei ya kuuzia 400.
Mapato kw trei 1 = 9,600
9,600×4= 38,400.
Mtaji 15,000
Faida 23,400...
Ukimlipa kijana 7000 au hata 10,000
Wewe unabaki 16,000-13,000..
Si faida ya pikipiki mbili hizo, na haiitaji service..
Cha ajabu, Mtaji haufiki 30,000... Mara 90% ya samani ya pikipiki na stress juu...
Kama na wewe unao mchanguo mwingine weka chini.. karibu..