Ni biashara gani ndugu zangu inaweza kuniingizia elfu saba kwa siku?

Kuna biashara ya samaki wakavu
Soko lake linapatikana kwa kutembeza mtaani au tafuta maeneo yaliyochangamka kama stendi na maeneo yaliyochangamka uswahilini, hutakaa sana na mzigo.
Kwakuwa ni wakavu wanakaa muda mrefu bila kuharibika na kama eneo la biashara litakua zuri unaweza maliza mzigo wa 150,000 ndani ya siku 4 ,
Faida kwa kawaida hukaribia bei ya manunuzi ya mzigo .
Mfano mzigo wa 150,000 unaweza kupata faida ya 90,000 - 120,000 kama tu unasehemu nzuri ya biashara(nakazia).
 
Aiseee
 
Zipo nyingi kwa mtaji Wa laki 200k - 300k
I/nunua gunia 3 za mkaa uza rejareja
ii/uza matunda ya kukata kata kwenye visahan na uuze kila plate elfu 1 plate 20 uta kuwa umepata faida na hela ya mtaji imerud
iii/fungus banda LA chips na vinywaji
iv/km upo dar uza kachor, ngisi na pweza
v/nguo za wadada zinalipa sana tengeneza kibanda kwenye mzunguko Wa warembo wengi nenda mchikichini nunua top, skin jeans,vimini na viatu Anza Kuuza.
vi/ beti kila Siku mikeka ya elfu 5 kaa subiri matokeo
 
Umeanza vizuuuri... Sasa hapo vi/
 
Uza hao samaki ikiwezekana agiza hata tanga au maeneo unajua utapata rahic me nipo tanga bei ya huku ni nzuri tofauti na dar #wakaange mwenyewe wafuate mwenyewe
 
Jitahidi ufungue filling station,hutajuta,tafuta eneo maeneo ya ocean road au posta
 
Halafu ndiyo nakula hizo Viewers au!
Ofcourse not, channel yako ikikua na kufikia vigezo unajiunga na adsense, kisha unapata vijisenti, 7000 hiyo kwa siku hukosi kabisa, ila upiga kazi hasa na kizalisha vipindi vizuri vyenye kuvutia watazamaji wengi, ili matangazo ya biashara yakiwekwa kwenye video zako yaonwe na watu wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…