Ni bora kuamini Mungu yupo umkose kuliko kuamini hayupo umkute?

NI bora kila mtu awe na Mungu wake
 
Naamini mungu yupo, ila mateso yasiyo na mwisho ni uongo.
Mateso yapo lakini yenye mwisho , mateso yasiyo kuwa na mwisho ni mafundisho ya uongo.
 
Ivi mtumishi maji ya uzima yana maana gani???
Mkuu unazungumzia maji gani? kuna maji ya uzima ambayo ni YESU alitumia kama mfano kwa mwanamke msamaria ili aeleweke kirahisi... kulingana na eneo husika!
 
Alitufia msalabani wanadamu ili tusipotee milele na kwa jina lake YESU tunaomba naye anatujibu haja zetu mkuu! Zerock
Endelea kuamini unachokiamini,ila soma sana ili ufahamu na siyo kukariri.
Hakuna mtu atakufa kwa ajili ya dhambi za mtu mwingine
 
lazima utarajie na imani inaumba anayeamini Mungu yupo atamkuta na pia asiyeamini Mungu hatamkuta , sasa hatujui atakuta kitu gani inategemea na imani yake na matarajio .
 
Mkuu unazungumzia maji gani? kuna maji ya uzima ambayo ni YESU alitumia kama mfano kwa mwanamke msamaria ili aeleweke kirahisi... kulingana na eneo husika!
Ndio hayo hayo maji ya uzima aliyotumia Yesu elezea maana yake hapa kwasababu biblia imeandikwa kwa mafumbo nataka ufumbue fumbo hapa ili nijue kama umekomaa kiimani
 
Ni Mungu yupi huyo anayeongelewa?………………maana kuna Miungu zaidi ya 1000 Duniani kote, inategemea tu na umezaliwa, kukulia na kulelewa kwenye mazingira yapi
 
Ndio hayo hayo maji ya uzima aliyotumia Yesu elezea maana yake hapa kwasababu biblia imeandikwa kwa mafumbo nataka ufumbue fumbo hapa ili nijue kama umekomaa kiimani
mkuu mimi sina experience sana na mafumbo ya biblia maana kwa age yangu na miaka niliyoanza kumwamini MUNGU indeed haifiki hata mitatu, bado naendelea kujifunza zaidi.
 
mkuu mimi sina experience sana na mafumbo ya biblia maana kwa age yangu na miaka niliyoanza kumwamini MUNGU indeed haifiki hata mitatu, bado naendelea kujifunza zaidi.
Ahsante kwa kuongea ukweli shida ipo kwa wachungaji (wanazuoni) wanaitafsiri biblia kwa maslahi yao.
 
Unafikiri Mungu akijua kuwa hujamuamini kweli ila umebeti tu atafurahi?
 
Yani uwekeze maisha yako yote kama dhamana ya kubeti tu habari za kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu.
Kwani ukichagua moja nani atakuchapa?
Tuseme hayupo nini kimetokea au yupo kuna nini kimetokea?
Well said mkuu.

Kila mtu akae chini kwa utashi wake achague kunyoa au kusuka.
 
Tatizo dini zinahubiri ama vitisho au ahadi kedekede za pasipojulikana.

Binadamu tuna hofu ya tusichokijua (fear of unknown). Mungu anaishi ndani yetu na ana sauti ya utulivu sana. Anasema nasi ila tunampuuza, hutaka tufanye yaliyo mema. Mwili ukiwa dhaifu, roho hupata nguvu na sauti ya Mungu husikika dhahiri. Hakika Mungu yupo.

Maisha ya duniani huisha na maisha mengine huanza. Maisha ya mwanadamu hayana ukomo. Mwili utakufa ila roho itaishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…