Ni bora kununua gari yenye kilometa 200,000 kutoka Japan kuliko kununua gari yenye kilometa 50,000 Tanzania.

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Madalali wa magari nchini Tanzania kila siku wamekuwa wakiharibu biashara ya magari ya mkononi kwa kukosa elimu ya biashara.

Uaminifu, ukweli na uwazi ni msingi MKUBWA sana kwenye ukuaji wa biashara yoyote ndio maana kwa kulijua hilo, wenzetu wa nje hawarudishi nyuma kilometa ambazo zinasoma kwenye odometer, umbali ambao Gari imetembea.

Gari ambayo imeingia nchini ikiwa imetembea kilometa 102,005, wauzaji watailazimisha Gari hiyo isomeke kwamba imetembea kilometa 35,000 kitu ambacho ni uhuni na kukosa weledi.

Soko la ndani la magari linaharibiwa na wauza magari wenyewe.
 
Ukitaka kujua kuwa kilomita zimerudishwa nyuma unafanyaje mkuu...?
 
Ukitaka kujua kuwa kilomita zimerudishwa nyuma unafanyaje mkuu...?

  1. Unusually low mileage for vehicle's age. ...
  2. Wear and tear don't match odometer. ...
  3. Dashboard shows signs of tampering. ...sio kwa magari yote
  4. Electrical issues. ...
  5. Mileage doesn't match the car's history report. ...na mara nyingi wauza magari doesn't provide this file kwako
  6. Suspiciously low price. ...
  7. Get a pre-purchase inspection. ...
  8. Take a test drive.
 
Kama hilo gari walinunua Toyota Tz pre owned nunua, ila kwa Kina Doto usinunue maana zile gari wanazichukua pale Jan Japanese zina 120Kkm wanaenda zishusha
Hawa kina Doto magari ndo waharibifu wenyewe. Pia show rooms nao wanarudisha sana kilometa.

Jan Japan wako very real wanakupa hadi docs za mnada na service history file
 
Kwa mfano zile mileage zinasoma kidijitali nilisoma inawezwa badilishwa kwenye dashboard ila ukichomeka mashine ya kusona error codes unaweza kuona mileage halisi maana inakuwa kwenye memory ya conp ya gari
 
Kwa mfano zile mileage zinasoma kidijitali nilisoma inawezwa badilishwa kwenye dashboard ila ukichomeka mashine ya kusona error codes unaweza kuona mileage halisi maana inakuwa kwenye memory ya conp ya gari
Wauza magari hawataki kabisa uende na diagnosis machine wakati wa MANUNUZI, utasikia huyu hana hela, hamna biashara hapa
 
Ukinunua mkononi ni kwa ajili ya shambani tu
 
Gari imetengenezwa 2002 halafu dalali anaonyesha imetembea 60,000 KM.

Tufanye haikupata mteja mpaka 2005.

So imetumika kuanzia 2005 mpaka 2024. Imekua barabarani kwa miaka 19. Kwa KM 60,000 hii ni kusema kila mwaka ilitembea 3157 KM.

Ikimaanisha kwamba hii gari tangu 2005 mpaka 2024 ilikua inatembea wastani wa 8 KM kwa siku.

Na hii ni kumaanisha huyu ni first user na wewe utakua second.

Mwisho inakua tatizo la umeme la gari lina tatizo jingine ambalo inabidi wewe na fundi wako mkatafute fundi mwingine.
 
Vitu vingine kutojitambua Kwa mnunua gari, wewe unakuta gari Lina zaidi ya miaka 15 mileage inasoma chini ya 100,000 inamaana Hilo gari lilikuwa bovu au?
Pili wewe mnunuzi lazima ujiridhishe na historia ya gari unalolinunua, mfano ipo mitandao ukiingiza chasis numba TU historia ya gari unaipata kipindi likiwa Japan eg lilikuwa registered lini, kilometer ilizo uzwa nalo, grade ya gari, accident histori
Hivyo kama hujitambua hata ununue Japan utapigwa TU kwasababu hata huko magari yanauzwa Kwa grade hivyo utauziwa grade R Kwa Bei ya grade 4.5
 
Shukrani sana kwa inputs hizi. Unaweza share link/platform ya kuingiza chasis number na kupata historia ya gari husika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…