Kwa observation yangu ndogo
Kuna watu wanapata wake bora kwa ajili yao ila si mama bora haswa kwenye kuwaongoza watoto katika njia ya kimafanikio
Na kuna wanaooa mama bora kwa watoto ila ni wake pasua kichwa
Na wachache sana wanaopata mke bora lakini pia ambaye ni mama bora.
Ninachomaanisha, hao wasomi wana exposure na uelewa wa dunia inapoelekea hivyo huwa na chance kubwa zaidi ya kuwaongoza watoto hata kama usipokuwepo. Wengine wa darasa la saba ambao ni submissive, wanaweza kuwasimamia watoto kimaadili zaidi ila kwingine huko itategemea spirit yake ya utafutaji
Ila ukioa darasa la nne C na mama wa nyumbani. Kula raha ya kuonekana mfalme ndani ya nyumba ila omba sana usije kufariki maana familia yako itaishia hapo maana mkeo hatokuwa na option nyingine zaidi ya kuolewa tena ili aishi mjini. Je, vipi kuhusu watoto wako mkuu?...
Hivyo unaweza tafuta msomi mwenye maadili maana wapo wengi tu kama vile ambavyo la pili C wapo wengi tu wamevurugwa.