Ni chakula, tunda au kinywaji gani unaona kipo overrated/underrated?

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Kwa upande wangu,

Underrated

Makande: Nimekuwa nikiona watu wakiyadharau sana makande eti kwamba ni chakula cha ajabu ila kwa mimi naona makande hayapewi heshima inayostahili. Jamii zote za makande kama; makande njugu, makande maharage zina mabalaa yake. Halafu itokee siku hiyo likachanganuwa na nyama na pak choi (Chainizi) kwa pembeni. Acheni wakuu, makande matamu bwana.

Zambarau:
Huwa najisikia vibaya sana pale haya matunda yanapokuwa hayapewi thamani yake. Ni nadra sana kukuta sehemu panauzwa zambarau. Yaani huwa nikipita njiani naona mazambarau yamedondoka tu na watu hawana hata time nayo huwa najiuliza kwani haya matunda yaliwakosea nini wadau. Haya matunda yametukuza, yametutoa mbali sana.
Zambarau uliweke kwa kipoozeo liwe la bariiidi, aah, acheni aisee!

Overrated

Pizza:
Hiiiiii, haya mavitu sijui hata watu wanayapendea nini! Kuna siku nikaamua kujitoa kimasomaso nikanunua pizza bwana ili nami niliburudishe tumbo kimamtoni, aisee. Nilijutia sana hela yangu.

Mafenesi: Kwanza sijui ndo jina lake hilo! Madude flani matunda yake makuubwa yana mavipelevipele, vile vinyama flani vya ndani ndo vinaliwa. Haya matunda ni maarufu sana Dar, utayakuta wauzaji wameyaweka pembeni mwa barabara. Kuna siku nami nikaamua kuyajaribu, aisee ile harufu tu ilinishinda. Buku langu likawa limeenda bure maana nikipofika gheto nikayatupa kwenye mfuko wa taka.

Ma-apple: Haya madude yanaishi kistaa sana hapa mjini maana bei ya apple moja unanunua sahani ya wali. Haya madude yananitesa maana kuna kadada nisipokanunulia basi lazima itokee vita ya majimaji. Ila ladha yake ni sawa na mapeasi tu. Yaani kiufupi ma-apple ni mapeasi yaliyochangamka. Figure tu ndo inayapa kiki hapa mjini vinginevyo yanyekuwa yanauzwa fungu mia kama mapera.

Vipi kwa upande wako?
 
Mtoa mada umeudhihirishia uma kuwa wew ni wa mkoani..

We komaa na kande zako tu mkuu...mi nikiziangalia tu meno yanapata ukakasi

Wew hata urojo utauweza kwel..au mchuz wa oweza...au biriyan + mandi...we wa mkoan ndugu yangu hzo mambo waachie wenyew...ushawai kula mandi ya kuku wa kienyeji halaf kuku nusu..upate na ndizi mbivu..aiseeeeeee
 
Ukiwa na njaa huwezi kuchagua chakula,issue ya kuchagua vyakula inakuja pale vyakula ni vingi na unakua na option,kama ni sehemu yenye njaa huo ujasiri wakuchagua vyakula unautoa wapi?
Yeye mwenyewe hajazungumzia mambo ya njaa.
 
Kwa upande wangu,

Underrated

Makande: Nimekuwa nikiona watu wakiyadharau sana makande eti kwamba ni chakula cha ajabu ila kwa mimi naona makande hayapewi heshima inayostahili. Jamii zote za makande kama; makande njugu, makande maharage zina mabalaa yake. Halafu itokee siku hiyo likachanganuwa na nyama na pak choi (Chainizi) kwa pembeni. Acheni wakuu, makande matamu bwana.
YES
Zambarau: Huwa najisikia vibaya sana pale haya matunda yanapokuwa hayapewi thamani yake. Ni nadra sana kukuta sehemu panauzwa zambarau. Yaani huwa nikipita njiani naona mazambarau yamedondoka tu na watu hawana hata time nayo huwa najiuliza kwani haya matunda yaliwakosea nini wadau. Haya matunda yametukuza, yametutoa mbali sana.
Zambarau uliweke kwa kipoozeo liwe la bariiidi, aah, acheni aisee!
Somehow
Overrated

Pizza:
Hiiiiii, haya mavitu sijui hata watu wanayapendea nini! Kuna siku nikaamua kujitoa kimasomaso nikanunua pizza bwana ili nami niliburudishe tumbo kimamtoni, aisee. Nilijutia sana hela yangu.
Pizza zipo aina nyingi ulikula ipi
Mafenesi: Kwanza sijui ndo jina lake hilo! Madude flani matunda yake makuubwa yana mavipelevipele, vile vinyama flani vya ndani ndo vinaliwa. Haya matunda ni maarufu sana Dar, utayakuta wauzaji wameyaweka pembeni mwa barabara. Kuna siku nami nikaamua kuyajaribu, aisee ile harufu tu ilinishinda. Buku langu likawa limeenda bure maana nikipofika gheto nikayatupa kwenye mfuko wa taka.
NO...alafu tangu mtoto uwe ujawai kula fenesi acha ujinga
Ma-apple: Haya madude yanaishi kistaa sana hapa mjini maana bei ya apple moja unanunua sahani ya wali. Haya madude yananitesa maana kuna kadada nisipokanunulia basi lazima itokee vita ya majimaji. Ila ladha yake ni sawa na mapeasi tu. Yaani kiufupi ma-apple ni mapeasi yaliyochangamka. Figure tu ndo inayapa kiki hapa mjini vinginevyo yanyekuwa yanauzwa fungu mia kama mapera.

Vipi kwa upande wako?
Apple ni tunda Luxury/Brand Shape yake
 
Mtoa mada umeudhihirishia uma kuwa wew ni wa mkoani..

We komaa na kande zako tu mkuu...mi nikiziangalia tu meno yanapata ukakasi

Wew hata urojo utauweza kwel..au mchuz wa oweza...au biriyan + mandi...we wa mkoan ndugu yangu hzo mambo waachie wenyew...ushawai kula mandi ya kuku wa kienyeji halaf kuku nusu..upate na ndizi mbivu..aiseeeeeee
Urojo sijawahi kula, nitautest.

Mchuzi wa pweza uko overrated sana,
 
We Muhaya kaa kwenu Muleba tu hizi food code huwez elewa kabisa.
 
Back
Top Bottom