Ni changamoto gani unaweza kutana nayo iwapo hutaripoti kwenye kituo cha kazi ulichopangiwa na TAMISEMI?

Nimepata dharula ambyo itanifanya niwe nje ya Tanzania kwa mwaka mzima.
Yaani ukae mwaka mzima ndio ukaripoti? Kisa nje ya nchi?

We endelea na mambo yako ya nje ya nchi usilete tamaa za kutaka huku na huku. Hebu waachie wenzio walio bongo na wasio na kazi wakafanye kazi hiyo.

Lakini hebu hata wewe jiulize, ingekuwa wewe ndio tamisemi ungefanya nini katika hii situation?
 
Kwenda nje ya nchi haimaanishi maisha yanakuwa yamekunyookea, nikirudi utanipa hela ya mboga na kodi.
 
Nashukuru mkuu nimeisoma nimekutan na hicho kipengele kinachoelezea athari za kutokuripoti bila sababu ya msingi.
 
Usitegemee kupangiwa kazi kwa levo hiyo tena.
 
Sijui ila nahisi mfumo utakuwa unakusoma kuwa huyu tayari alishapangiwa halmashauri x (kwahiyo arukwe)
 
Kwenda nje ya nchi haimaanishi maisha yanakuwa yamekunyookea, nikirudi utanipa hela ya mboga na kodi.
Sasa kama unajua yote hayo kwann unatusumbua, si usiende huko nje ya nchi ukaripoti ulikopangiwa
 
Nimepata dharula ambyo itanifanya niwe nje ya Tanzania kwa mwaka mzima.
Kama ulivyoomba ajira,kwa nini usiwasiliane na mwajiri wako huyo umueleze kiofisi.Zingatia neno "kiofisi" ili uondoe shaka ya kukutana na vizingiti mbeleni.
 
Niliona mahali wanasema usiporipoti hautowwza kuajiriwa tena na utumishi wa umma
 
Sheria za utumishi!
Kama sikusahau unapaswa kuripoti kituo cha kazi kabla ya wiki mbili kuisha!
Zaidi ya hapo toa maelezo!
 
Kama hujapata chek namba unaweza kuomba tena na hata kama ulishapata ukaacha kuna taratibu za kufuata.
 
Kila la kheri waliolamba asali Mungu awatangulie katika majukum yao mapya
 
Na hii likizo maximum ni muda gan? Na labda kama kuna probability yyt ya kukataliwa au kukubaliwa?
Not more than three years muhimu kuwa intouch na afisa utumishi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…