Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Absolutely true! Mungu huwa hachelewi anakuja kwa wakati sahihi tu. Nashukuru Mungu kilikuwa kipindi kifupi kigumu saana lakini nilijifunza mengi saana.

Kwa vile nilikuwa na pesa awali hata kuomba msaada nilishindwa maana nilikuwa nawaza watu watanicheka na Mama yangu hakuwahi kujua maana nilijua nitampa mawazo tu kumwambia whole situation. So I fought this battle all alone.

Triumphantly, nilipita Salama lile bonde la dhiki kuu. Usiombe kukosa pesa wakati awali ulikuwa nazo unaweza kuwa mwehu maana unaona aibu kufanya kazi mbovu sababu ulikuwa nazo mwanzoni.

Mungu ni mwema, nimerudi barabarani na technically wewe ni miongoni mwa marafiki zangu wa hapa JF I wish hata siku moja tuonane tu.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Mungu ni mwema sana sana Humble...Nafurahi kuona ulipita katika lile bonde la uvuli wa mauti salama

Sasa ni nini? Ukiwa mjini nichek tu Rafiki yangu..Nipo available napambana...

Karibu.
 
Wanawake hawajifikiriagi mara mbili hao watu sijui waliongea nini na shetani, swala la tunda nadhani lilikua topic ya mwisho kabisa
 
Kweli kabisa ndugu.
 
Mungu amlaze mahala pema Hakika Alikuwa mwenye Utu Sana, Kama huyo mkewe yupo usiache kumtembelea
 
Wanawake hawajifikiriagi mara mbili hao watu sijui waliongea nini na shetani, swala la tunda nadhani lilikua topic ya mwisho kabisa
Kuna vitu vinafanyika ili kutimiza unabii, sasa kwa vile haikusemwa tuwalaumu wanawake kwa kosa la pale Eden au tuwachukie wanawake basi inawezekana ni unabii ulitimizwa, Sasa tunakiwa twende na kauli mbiu yetu ya kufanya kazi kwa jasho ili tupate riziki.
 
Mungu amlaze mahala pema Hakika Alikuwa mwenye Utu Sana, Kama huyo mkewe yupo usiache kumtembelea
Unajua shida nyingi zinatupata wanadamu hasa Afrika kwa kuyakataa maarifa, imagine tumeambiwa tusaidiane sisi kwa sisi lakini watu hata yule anayejua huyu anashida kweli nimsaidie yeye anakwepa, na waliofanya sisi tuharibikiwe tunyimane misaada ni wale waliotumia misaada ya wenzao vibaya mfano kubweteka tu unaposaidiwa au kuomba na vya ziada bila kupewa hawa watu wabaya wanatakiwa waundiwe kikao Cha kukemewa kila pande za nchi.
 
Hakika Mkuu
 
Sitasahau nilivyoanza kukopa hela kwenye applications za mikopo nilizokuwa nazidharau nikiona matangazo yangu Facebook. Sasa picha linaanza kuna siku nataka kukopa TENI kwenye Moja ya application za MIKOPO wakaomba picha yangu ya kuscan nilikuwa bar then nakimbia toilet kupiga picha kwa Siri ghafla umeme ukakata daah ilikuwa noma sana wakuu. Chanzo Cha yote hayo ni kupitia ugumu wa kuichumi usiombe yakukute[emoji23]
 
Nimesoma comments zoote
Kwa hakika maisha ni tough
Neno moja lisikauke kinywani ni AHSANTE MUNGU
binafsi sikuwahi kupitia maisha magumu hata kidogo
Kwetu tupo 6
Ila mshua alipambana kadri ya alivyoweza kuweka mambo level nyumbani
Leo wa tatu kati ya sisi sita tunaweza kusema tunajitegemea

Wazazi wanapambana sana sana Sanaa kujenga tabasamu kwetu
Thus mama au mzee wanapotaka chochote hua sisiti kutoa pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…