Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Sijui niandike nini lakini mapito kwa mwanadamu ni sehemu ya kumjenga. Kwa wasioelewa vizuri neno umasikini ni hali ya kushindwa kupata chakula, mavazi ,makazi. Umasikini ni kuumwa na kushindwa kupata huduma, ni kupoteza matumaini ya kuishi kesho. Ni kukosa kazi ya kufanya, ni kukosa elimu, kushindwa kusoma, kuwa na nguvu lakini huna chakufanya.

Ukiwa na pesa changamana na wenye pesa, masikini ni mtu hatari sana usichangamane nae kwenye starehe. Sijasema usimsaidie bali usijenge mazoea na masikini kama wewe una kipato cha kati au juu chagua mnaoendana kipato.

Wasalimie masikini lakini usikubali wakuzoee, naongea kama masikini wa mali na tajiri wa fikra. Masikini masikini wacha akae na masikini mwenzake.

Nimewahi kupitia mengi mazito tena nikiwa na familia yangu lakini akili iliendelea kuwa imara zaidi na zaidi. Mpaka sasa naheshimu sana pesa.

Namwelewaga sana Mwana FA wanaosema pesa sio kila kitu umasikini unanunua nini??mimi kwa akili zangu bila kulazimishwa na mtu nakiri pesa kwangu ndio kila kitu. Sio tu sipendi masikini, umasikini pia sipendi mtu anaependa kuongelea shida, anaependa kuongelea negative, huwezi kuwa rafiki yangu kama wewe ni masikini wa fikra.

Naamni kwenye kujituma na kuwekeza juhudi, naamini kuna kushikwa mkono na kujiongezea urefu. Naamini kuna bahati na kuna fursa na kuna mipango ya muweza wa yote na pia kuna kuna kuna bahati mbaya.

Namini ili ufanikiwe zaidi inakubidi kuwa tofauti, naamini matajiri ni watu jasiri na masikini ni waoga na wana upole wa kuonewa huruma.
Naamini akili + nguvu + siasa + tajahudi/meditation + ubunifu = lazima uzipate pesa chafu na safi.

Naamini binadamu anauwezo mkubwa sana kama akiweza kutumia ubongo wake vizuri. Naamini mitandao inapotosha na kushape thinking tone ya binadamu wa sasa.

Ukishakuwa na pesa jifunze namna ya kuzilinda na zifundishe pesa zako namna ya kuita pesa zingine zije zenyewe tena zije kwa mafungu zisije moja moja tena jifunze kuziamuru pesa zako zisipende kukaa mbali sana na wewe sio mpaka uzitafute ndio uzione.

Utajiri ni Science na ukiimudu utaitwa majina yote mazuri na ya kuogopesha. Utajiri una marafiki wengi sana. Masikini hata ndugu wa damu wanamkimbia sio tu kumtenga. Ukweli haupendwi sana ngoja nikomee apa muhimu masikini sio mtu wa kuonea huruma na unapomsaidia masikini msaidie kwa kutumia akili.
 
Mlijengwa kwenye msingi mzuri, wababa wengi wa Sasa hawajui mamlaka Yao na jukumu lao kwa kizazi Chao kiasi Cha kulaaniwa bila wao kujua, unakuta baba kijana kabisa hajengi msingi wa watoto wake ila na muda mwingine watoto wamekuwa kidogo na hawana msingi mzuri anashinda kuomba hela kama mtu asiye na nguvu na watu wanashangilia, ila baba wa hivyo huwa ananya'gwa mamlaka yake na Mungu na uzee wake huwa mbaya sana tena wa kuomba omba kama ombaomba, ila baba aliyesimama kwenye msingi wake huku anamkumbusha Mungu ambariki ili asimamie majukumu yake vizuri hata watoto wakiondoka wote Bado Mungu huwa anampa watu wa kumuhudumia nyakati za uzee.
Sasa hapo Umeandika nini!
 
Kufulia wanakuita kwa kimombo "Broke", kwa kinaijeria "sapaa", kusikiage tu!

Nakumbuka niliwahi kuwa na bajeti ya 200 kwa siku, nakula mhogo wa kuchemsha imeisha hio hadi kesho, pesa ikakata nikawa nafunga safari natembea lisaa ni nje ya mji kidogo naenda kukwea miti ya mapera, nakula na huo ndo unakuwa mlo wangu wa siku nzima. (shughuli ya uwani haikuwa ndogo)

Nilikuwa napenda sana mambo ya simu na niliweza kuzichambua vizuri kwenye camera, ram, ubora, chaji, n.k, hii ilifanya watu wawe wanakuja kuniomba ushauri kununua simu ipi kwa bajeti waliyonayo ila mimi nilikuwa na kitochi kimechoka.

Nilianza kuhesabu majina kwa simu huku nikisema nani anaweza kuniazima bila kuanza kunipa darasa la maisha ama kunitangaza.

Sendo yangu ilikatika upande moja nikawa naipiga msumali ijishike, baada ya siku 3 inaachia napigilia tena, ilijaa matundu kibao.

Nilikuwa natoa nguo zote kwenye tenga na kuanza kusachi moja moja kama ina hela naambulia patupu, kesho narudia nazikunguta kwa nguvu, lakini wapi.
Daahhh,inachekesha sana hii story ila inaukweli aiseee
 
Niliwahi kufulia miaka hiyo ikafika hatua mtoto wangu wa miaka 2 akiona chakula ni kama kaona almasi. Anafukia sahani nzima ya wali wa buku jero nilionunua Kwa mama lishe! Acha kabisa. Sasa hivi mambo sio mabaya dogo yupo shule hajui aliyoyapitia......
 
Niliwahi kufulia miaka hiyo ikafika hatua mtoto wangu wa miaka 2 akiona chakula ni kama kaona almasi. Anafukia sahani nzima ya wali wa buku jero nilionunua Kwa mama lishe! Acha kabisa. Sasa hivi mambo sio mabaya dogo yupo shule hajui aliyoyapitia......
"""mtoto wangu wa miaka 2 akiona chakula ni kama kaona almasi."""
Nimecheka japo yanahudhunisha 😂😂🙌🙌🙌🙌🙌
Lika la hivo watoto huwa wana kula hatareee
 
"""mtoto wangu wa miaka 2 akiona chakula ni kama kaona almasi."""
Nimecheka japo yanahudhunisha 😂😂🙌🙌🙌🙌🙌
Lika la hivo watoto huwa wana kula hatareee
Acha tu siwezi kusahau! Ilikua nikileta msosi mtoto anaurukia ..... Maana utakuta asubuhi hajapata uji hakuna gesi hakuna mkaa... Ila mama watoto na mapungufu yako yote chukua maua yako! Ulinivumilia Kwa mengi....
 
Mkuu kwanza hongera kwa kuleta mada kama hii.

Umaskini kufulia bati kali nilishapitia japo sikukosa chakula kabisa ila niliishi kimasimango sana. Ila Mungu ana njia zake kipindi hicho hicho cha kufulia nilikua na mwanangu nakaa nae geto alikua anapiga kazi mjini cha ajabu akirudi kila siku analalamika hana hela na hata kodi nilikua simshirikishi ila yeye hela hana kila siku.
nilikua naweka buku kwamba juice ya 500 na sambusa za viazi za 500 kila siku jioni na alikua anakuja tunagawana na sijawahi jisikia vibaya mpaka nahisi alijistukia. Mbaya zaidi alikua ananunua kitimoto anakula mwenyewe akirudi anacheua unaskia kabisa mapocho pocho ila hata kusema leo mwanangu naye afaidi hakuna hiyo.
Siku moja nilimuomba msaada kigo ila asubuhi nikakuta maneno mtaani basi nikapiga moyo konde japo nilikua naweza rudisha mpira kwa kipa muda wowote ila niliamua kupambana nikijua ipo siku itakua stori tu
 
Acha tu siwezi kusahau! Ilikua nikileta msosi mtoto anaurukia ..... Maana utakuta asubuhi hajapata uji hakuna gesi hakuna mkaa... Ila mama watoto na mapungufu yako yote chukua maua yako! Ulinivumilia Kwa mengi....
Hongera kwako...
🤝🤝🙌🙌🙌 Mama ni mama....
 
Back
Top Bottom