Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Kufulia wanakuita kwa kimombo "Broke", kwa kinaijeria "sapaa", kusikiage tu!

Nakumbuka niliwahi kuwa na bajeti ya 200 kwa siku, nakula mhogo wa kuchemsha imeisha hio hadi kesho, pesa ikakata nikawa nafunga safari natembea lisaa ni nje ya mji kidogo naenda kukwea miti ya mapera, nakula na huo ndo unakuwa mlo wangu wa siku nzima. (shughuli ya uwani haikuwa ndogo)

Nilikuwa napenda sana mambo ya simu na niliweza kuzichambua vizuri kwenye camera, ram, ubora, chaji, n.k, hii ilifanya watu wawe wanakuja kuniomba ushauri kununua simu ipi kwa bajeti waliyonayo ila mimi nilikuwa na kitochi kimechoka.

Nilianza kuhesabu majina kwa simu huku nikisema nani anaweza kuniazima bila kuanza kunipa darasa la maisha ama kunitangaza.

Sendo yangu ilikatika upande moja nikawa naipiga msumali ijishike, baada ya siku 3 inaachia napigilia tena, ilijaa matundu kibao.

Nilikuwa natoa nguo zote kwenye tenga na kuanza kusachi moja moja kama ina hela naambulia patupu, kesho narudia nazikunguta kwa nguvu, lakini wapi.

Nikikuwa na Low Self Esteem.
 
Nilienda bush kumsalimia mjomba angu alikuwa ni mkulima amevuna mahindi mengi ya njano lakini anko aliishi kivyake hakuwa na mke dah alipika ugali mkubwa wa njano nikajua anko ameandaa mboga akatenga ugali kwenye chungu akatoa chupa ina mafuta ya ng'ombe (samli) yameganda akaipisha juu ya jiko ikayeyuka akamimina kwenye bakuli akaweka chumvi ikawa ndio mboga unamega tonge unatoezea kwenye mafuta unameza ugali
Tamu ile mbaya..
 
Ni vingi visa, ila nakumbuka mvua ina nyesha asubuhi had jioni na ndani hakuna chakula, mama alinipa mfuko wa sulphate kisha akasema nenda mwembe fulani ukaangue maembe ulete tulalie..

Nimetembea ndani ya mvua, nimekwea ule mwembe kunanyesha, nimevuna maembe robo kiloba kisha nikarejea nyumbani bado kunanyesha, tukajikusanya pamoja kama vile chakula tayari, kila mmoja anavuta embe anakula likiisha unarejea kwenye mfuko kuchukua lingine


Baada ya hapo mama akasem kunyweni maji mlale..
R.I.P hero Mom
Na hiki ni moja ya visanga/episode katika safar ya ufukara
Daaah! Jamaniii 😢
 
Huu uzi unarudisha hali ya ubinadamu poleni sana ndugu zangu mliopitia mazito nawaombea mpate faraja katika maisha yenu

Umasikini, ukata, kufuria, kukata ringi nyie kusikieni tu kwa wengine nimejikuta nimekosa cha kuandika nasoma comment tu

Kuna maisha wengine tulikua tunayaona ni ya kawaida sana ila kwa wengine yale maisha yalikua ni msoto

Mungu wasimamie watoto wote waliotoka vituo vya kulelea watoto yatima, na watoto yatima wote waliopo mitaani uwape amani mioyoni mwao,

Acha niwaombee amani ya moyo najua ndo dawa ya umasikini ambayo wengi hawaijui, nawaombea ndugu zangu wote mliopo kwenye misuko suko ya maisha mfurahi mkipata na muwe na amani mkikosa umasikini unauma sana pale unaposhindwa kukubali matokeo unaweza jikatia tamaa ya maisha
 
Mimi pia nimewahi kushindia kipande Cha mua Cha sh.100 na nilikinunua Kutoka Kwa akina ya sh.300 niliyokuwa nayo..

Pili nikiwa Dar nilipigika kiasi kwamba Chakula na makazi nilikuwa nakula Kwa mama wa rafiki yangu..

Siku Moja Jamaa alisema Kila mtu aondoke akapange ,hapo Sasa ndipo Kilio kichwa kilijaa gas,ilifika mahala nikaomba Msaada wa nauli Kwa broo Fulani ambae niliwahi soma nae O level,yule ndio alinisaidia nauli nikarudisha Mpira Kwa kipa mkoani ambako Nako maswaibu yaliendelea ikiwemo Hilo la kushindia Mua huku nasaka kazi za saidia fundi niweze ku survive..

Siku Moja nikiwa kwenye kazi za saidia fundi ukiacha kejeli vilaza wale mafundi Kwa vile walishajua mie ni msomi,nikapata demu huko huko basi wakaanza kumponda akanikacha,nikapata mwingine nikajiroga kumleta geto ,getoni Kulikuwa na jiko la Mkaa,ndoo 2 ndogo ya kuogea na ya kawaida na visufuria viiwili,godoro la wanafunzi nimetandika chini na geto ni single jirani na vyoo..

Demu alivyoingia nadhani alichoka ,akaomba atoke Nje uani,aisee alisepa maxima na akaniblock na Namba yangu [emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957]

Ila Maisha yanabadilika siku huko tena Mungu anawajali watu wake.Dar sikutoka Bure nilipata Mke.
We msenge kumbe ndo maana waichukia Dar, uliishindwa
 
Back
Top Bottom