Hii inaweza kuwasaidia
Kwa hustler yeyote ukiingia kwenye mji au nchi yoyote ambao ww ni mgeni huna pa kufikia wala hujui utapata wapi kibarua, cha kufanya uliza mwenyeji yeyote akuelekeze mahali Soko kubwa la mji lilipo.
Amini nakwambia hutolala njaa pindi ukifika sokoni na hutakosa kazi ya kufanya hata kubeba mzigo utabeba na pesa utapata.
Why Sokoni na si mahala pengine? Sokoni ndio sehemu ambapo kuna mzunguko mkubwa wa pesa katika mji au kitongoji husika. Baada ya hapo sasa utaweza kuangalia ufanyaje ili utoke kimaisha.
Sehemu nyingine ambayo inaweza kukuokoa ni Migahawani au Hotelini. Hii sehemu inaweza kukuokoa usilale na njaa na pia unaweza kupata ujira mdogo. Ukifika maeneo hayo omba kazi ya kufanya usafi na hata kuosha vyombo. Hii itakusaidia sana kupata ujira mdogo na chakula pia.
Mwisho kabisa ni nyumba za ibada iwe msikitini au kanisani. Huku kunaweza kukupa fursa ya kukutana na watu wenye hofu na kumjua Mungu hivyo ni mara chache sana kwa wewe mgeni kukosa hifadhi au chakula, na ukiwa nao vizuri unaweza ukapatiwa connection ya kazi.
Kikubwa ukifika sehemu yoyote jiepushe sana kuomba Fedha bali omba kibarua /kazi ,hii itakuwezesha upate pesa ya kujikimu na vilevile kukuepusha dhidi ya fedheha na udhalili wa kuombaomba. Kumbuka mwanadamu hapendi kuombwa pesa.
Katika kutafuta pesa epuka kitu kinachoitwa kuona aibu, watu watakuchukuliaje nk. Mwanaume hachagui kazi as long as kazi hiyo ni ya halali na haimuondolei utu wake.