Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Kufulia wanakuita kwa kimombo "Broke", kwa kinaijeria "sapaa", kusikiage tu!

Nakumbuka niliwahi kuwa na bajeti ya 200 kwa siku, nakula mhogo wa kuchemsha imeisha hio hadi kessho, pesa ikakata nikawa nafunga safari natembea lisaa ni nje ya mji kidogo naenda kukwea miti ya mapera, nakula na huo ndo unakuwa mlo wangu wa siku nzima. (shughuli ya uwani haikuwa ndogo)

Nilikuwa napenda sana mambo ya simu na niliweza kuzichambua vizuri kwenye camera, ram, ubora, chaji, n.k, hii ilifanya watu wawe wanakuja kuniomba ushauri kununua simu ipi kwa bajet waliyonayo ila mimi nilikuwa na kitochi kimechoka.

Nilianza kuhesabu majina kwa simu huku nikisema nani anaweza kuniazima bila kuanza kunipa darasa la maisha ama kunitangaza.

Sendo yangu ilikatika upande moja nikawa naipiga msumali ijishike, baada ya siku 3 inaachia napigilia tena, ilijaa matundu kibao.

Nilikuwa natoa nguo zote kwenye tenga na kuanza kusachi moja moja kama ina hela naambulia patupu, kesho narudia nazikunguta kwa nguvu, lakini wapi.
Mkuu,
Sasa mbona umeandika Uzi ambao nilitamani kuanzisha......

Uzi wa kuutupia mawe umaskini......yaan unajua UMASKINI 🤓 unafananaje hasa ukikosa mapenzi ya wazazi 😊 marafiki wakakutenga na ndugu wakakimbia na mpenzi akisema hakutaki (umwache) ......

#MAPISHI YA UPENDO
 
Mama yangu alikuwa mpika na muuza gongo kule Gongo la mboto mapolisi waliweka informer kila tukiwa tunaenda kupiga gongo wanakuja wanamkamata mama analia tukiwa mapolini kule kinyerezi(enzi hizo kinyerezi kulikuwa pori la kukamata hadi sungura na digi digi kabisa) sasa mama alikamatwa mfuluzo mbaya zaidi wakati mahita anatawazwa kuwa IGP si akapitisha opereshen maalum ambayo mama akabebwa na ma pipa na mtambo wa gongo mpaka kituoni akatuacha mimi na wadogo zangu watatu.Mimi niliachwa kwa sababu ni mdogo ikabidi mimi nikabidhiwe jezi na mchezo sijauelewa hivyo nikajikuta nina majukumu ya kulisha wadogo zangu na kumtafutia mama chakula ili ale kule lock up kwa sababu ndugu tulikuwa nao wachache pale Dar ambao kama vile walitutenga kwa sababu ya umasikini.Dingi ameshasepaga muda kakimbia familia sababu ni hiyo hiyo umasikini.
Ikanibidi niwe naenda matembezini na kiroba kwapani huko kutafuta mashamba ya watu mfano wa mashamba nilikuwa nayaonea ni ya miogo na viazi na minazi na mapera kule ulongoni enzi hizo hata TANESCO hawajaweka umeme hata nyumba moja.
Huwezi amini nilijua hadi kupandia minazi ili niibe madafu usiku anyway tu cut the story nilikuwa naondoka na kiroba kitupu nawaacha madogolas wamejikunyata nikirudi wanabidi wapokeee chochote ntachokuja nacho kwenye kiroba kuna siku nilikimbizwa na mwenye shamba ambae lilikuwa na miogo mitamu kumbe aliweka lindo baada ya kuona katikati ya shamba lake nimelaza mashina yote aisee.
KUMBE kitendo cha kuwa namletea miogo kila siku maza mapolisi wakawa wananichora na kunidiscuss siku moja nilikosa miogo nikapeleka madafu mawili mama aliachiwa tuongee nae nje ya kituo si akaanza kulia na kuniambukiza kilio na mimi kumbe ile ilikuwa pona yake si mkuu wa kituo akazipata zile habari maana kumbe watu wanapewa dhamana mimi sijui taratibu wakaniuliza eti kesho nije na mkubwa tumdhamini kwa vile ndugu walishatutenga ikabidi nikamchukue MAMA SALAWALA(sijui yupo wapi) ambae huwa tunamuuziaga gongo anaishi mzambarauni Gongo la mboto.
Mama akatoka mtaji ukawa umefilisiwa maana walibeba mtambo wa gongo na mapipa yote ikabidi mama awe raia mwema akaanza kuazima shamba tukawa tunalima huku tunashindia maembe
Anyway njaa ni noma inakosesha hadi ladha ya maisha
Sitaki kueleza mengi at the end nikafaulu mtaa mzima kwenda shule ya AZABOY nikaona shida zinazidi nyumbani hata nauli nikakosa ikabidi niende kujipendekeza kwa madogo wa dogo dogo center Mabibo karibia na shule ya loyola walipangishiwa nyumba na wadhamini wao wazungu.
Story ni ndefu ila acheni nijiite Billie humu JF kwa sababu hata mama yangu kwa sasa nimuanzishia biashara anaishi kwenye nyumba nzuri na kuna flame za kupangisha 8 na ana nyumba za wapangaji 5.
Upande wa mimi now nilivyo sitaki kusema ila nipo na familia ambayo watoto kula mpaka uwashikie fimbo au uwawekee katuni na almost kila kitu ndani hadi vyakula vinaharibika.SIJITAPI NAONGEA UKWELI TUPU NIMEJIFUNZA SHIDA NI ELIMU NZURI SANA KAMA UKIWEZA KUZITOROKA.
Mkuu ulisoma aza boi enzi za mchwa mpaka nini???¿? Yule ticha mpenda fimbo
 
Ajue maisha sio rahisi namna hiyo, lakini pia akumbuke privilege aliyonayo na familia yake kuna wengine hata hayo makombo wanayatamani.

Nasikitika tu kuwa wapo wanawake hawajui kupima chakula, ni hawawezi.
Sio hawawezi wanafanya makusudi kwa kuwa hela ni ya mume.
Wakitumiaga hela zao huoni wakitupa chakula
 
Overpopulation ndio imechangaia kwa kiasi kikubwa ufukara wa kutisha. Idadi ya ukuaji wa watu ni muhimu kudhibitiwa ili kupambana na umaskini.
Nilichojifunza kuwa overpopulation ni nzuri kama hiyo popularion ina characteristics za high IQ(check wachina) ila kama sisi masikini tunazaliana hovyo na ubongo wetu hautoshi kwenye kupambana na nature ndo hayo yanatukuta.
 
matatizo ndo hufanya akili zetu kuwa aggressive kwenye kutafuta fursa.

siku zote mwanaume usikubali kuwa na maamuzi yatakayoplekea familia yako ilazimike kwenda kulia kwa familia ingine ili ipate chakula, nguo ama malazi. (allocate your income wisely)
Vingine vya magari hivyo na mijengo sita sita ni majaaliwa.
 
Baada ya kusoma comments zote, nimegundua wazazi wa kiume ni wachache sana wanaoonekana walitoa mchango kwa watoto wao either iwe ni ukweli au kwa watoto kutokujua

Japo mimi sikupitia magumu kiasi hicho kama wenzangu lakini mpaka leo nakiri mshua wangu alikua Master sana, na mama kwa upande wake alijitahidi

Wazazi wa kiume turekebishe hapo penye mapungufu,

japo ni ngumu kumridhisha mtoto na kumfanya aamini nawe unamsaidia kama hauishi nae au hauko nae karibu sana, Credits zote atapewa mama
 
Ili kuimarika kuna mapitio mengine ni muhimu kuyapitia ili yawe ukumbusho wa kukosa pale ukipata.

Ila kiukweli kabisa hakuna faraja kwenye ufukara.

Nakumbuka kuna kipindi nilipigika ikawa natembelea washkaji mida ya misosi kiasi cha kujua ratiba ya mlo wa masela wote.

Kuna msela wangu (Mungu amlaze mahala pema) ilikuwa ikifika jioni ananipigia simu kuniita tukapige story, kumbe alishajua hali yangu na ule wito ulikuwa ni msaada indirectly maana alihakikisha nakula ndio naondoka.

Na kila nikiondoka mkewe ananipa kikontena cha msosi ananiambia shem naona chakula cha leo umekipenda beba na hiki utakula baadae.

Hawakujua jinsi gani walikuwa wakinisevu.
Maisha aya
 
Daaaah acheni mikasa ni mingi lakn nakumbuka tu wakat nimeenda kuripoti chuo,,hela ya kuungaunga ile usajili ikakataa sikua hata mia,,,nilikaa siku mbili bila kula hadi vidonda vilitoka kooni aiseeee haya maisha. Lkn hali ile ilinitia uchungi nilijiapiza Mungu akiendelea kunijaalia uhai iwe mvua iwe jua kamwe wanangu wasije kupitia yale maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kusoma comments zote, nimegundua wazazi wa kiume ni wachache sana wanaoonekana walitoa mchango kwa watoto wao either iwe ni ukweli au kwa watoto kutokujua

Japo mimi sikupitia magumu kiasi hicho kama wenzangu lakini mpaka leo nakiri mshua wangu alikua Master sana, na mama kwa upande wake alijitahidi

Wazazi wa kiume turekebishe hapo penye mapungufu,

japo ni ngumu kumridhisha mtoto na kumfanya aamini nawe unamsaidia kama hauishi nae au hauko nae karibu sana, Credits zote atapewa mama

Kuna kitu hujanote unajua umasikin Upo tu lkn baba akiwa si mtu wa familia Yaan mlev malaya mvivu mbinafsi aisee apo ndo umasikin uwa unazid mara dufu mkuu
 
Back
Top Bottom