Wew achana na nyie wakishua ambao mmekulia maisha mazuri hamuzijui shida wala umasikini.
Jf wengi wanaFake maisha lkn kwa Ground ukweli mnaujua[emoji23].
Mim nakumbuka niliwai pigwa na maisha mpaka nikafanya kama alichokifanya mtoa mada yaan kusachi nguo nikaambulia vumbi tupu[emoji23][emoji23], kiufupi niliambulia patupu kwa hasira nilizikusanya nguo zote nikawabeep washikaji waje wajichagulie kwa bei nafuu, maajabu na washikaji nao walipokuja wakaishia kunikopa nikaambulia buku3 ya kula siku moja.
Nishawai shindia pipi ivory na maji mengii siku nzima mpaka ukitembea tumbo linanguruma ule mlio wa maji kujaa tumbonii[emoji23][emoji23].
Shaenda mpaka kwa sangoma aloge nipate pesa kibahati nilipe madeni ya watu lakin mjinga yule nae akaanza masharti ya kijinga huyo nikatimka[emoji23][emoji23]
Kiufupi ukiwa ktk kipind kigumu kuna njia unazoamini zitasaidia kujikwamua lkn maajabu hizo njia ndio zinakuzamisha ktk mateso zaidi[emoji23].
JF watu wakiacha kuigiza maisha na kueleza uhalisia wao watasaidika humu kuna wengi tu wana Roho nzuri za kusaidia hata mimi kwa niliyoyapitia sipendi kuona mwingine anayapitia, lkn kwa hii Trend ya wanaJF kufake maisha basi acha wote tuonekane tuna magari na manyumba.