Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Hiyo ilitukuta morogoro mazimbu tulikuwa tumelala wanaume kama watatu mana chumba chetu kilikuwa kikubwa vitanda viwili vinatosha na ukitucheki tulikuwa mbavu balaa jamaa walizoa kila kitu visimu sory radio kubwa,tv samsung asubuh tunaamka mlango upo wazi tunashangaa nani alitoka hajafunga mlango kauacha wazi yani wanafungua mlango wote kuchak mali hazipo alooo hii kitu mbaya sana.

Watoto wa Dark city hao.. Mngeenda pale mkatangaza dau mngevipata.
 
image.jpeg
image.jpeg


Hii nimeiona kwenye Group la WhatsApp,imetokea mitaa ya Segerea Dsm...Jamaa walikuja usiku wa kiza kinene,wakapiga dawa dirishani wakaanza kupakuwa kitu kimoja baada ya kingine!!Chumbani walishindwa kuingia ikabidi watumie hilo "jaro" kupakuwa simu kitandani.

Wakazungukia kwa wapangaji wengine wakakomba kila kitu.Wakapakuwa kiporo cha ubwabwa wa kipaimara wakala,wakafungua friji wakanywa juice yote na matunda.Wakaenda na bafani wakaoga na kujisaidia bila kuflash ...wakafungua TV ukutani ya nchi 32 na mziki sebuleni...baada ya hapo wakakojolea kwenye vikombe na masufulia,ajabu ni kuwa haya yote yanatokea hakuna hata aliyeamka.

Walioibiwa wamekuja kuamshwa saa tano asubuhi,maana gari ya shule "school bus" ilikuja kuwabeba watoto ikapiga sana honi bila mafanikio...aliyekuja kustua majirani ni Mama msaidizi wa kazi ambaye huwa anasidia kazi na kurudi nyumbani.Watoto wamelazwa chini jamaa wamebeba mashuka na mito.

Hivi hawa jamaa dawa yao nini??Maana imekuwa kero sana kwa sasa....Yaani wameiba na kumpaka mtu white dent eneo la "mtaro wa maji machafu" halafu wakatoweka....sio haki kabisaaaaaa
 
Huwa nashangaa sana! Hawa watu hawajaenda shule lakini wana akili sana!
 
Huu uwizi wa designed hii ilianziaga msisiri,Kinondoni Wezi walikuwa maarufu kwa Jina la Jordan....
dawa Yao ni majirani waji organise kisiri na kufanya lindooo......dawa nyingine ni kumkamata mmoja wao na kumfanyia kitu mbaya.....ili ujumbe uwaendee wengine
 
Nimecheka sana Asee....Utafikiri mazuri!!Kweli JF never boring
 
Hizo dawa noma kijichi jamaa walikuja na fuso...jirani mmoja akirudi toka night shift akaona makochi yanapakizwa akajua jirani wanahama,akaona asiwasemeshe akaenda lala kwake ....dah familiya nzima ilikutwa haijitambui mnamo SAA 5-6 wakiwa wamelazwa chini saafuni!kila kitu makabati, hadi mapazia walibeba!
 
Unafahamu spray wanazozitumia kuwapurizia ndani?
Point yangu ni kuwa hao wezi walikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo yao mpaka kuwa na confidence ya kuamua waoge kabisa.

Wezi mara nyingi wanakuwa wanafanya mambo yao halafu wanapotea haraka eneo la tukio, ila hawa waliamua waoge kabisa
 
Point yangu ni kuwa hao wezi walikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo yao mpaka kuwa na confidence ya kuamua waoge kabisa.

Wezi mara nyingi wanakuwa wanafanya mambo yao halafu wanapotea haraka eneo la tukio, ila hawa waliamua waoge kabisa
Swali linasimama palepale unzijuwa spray wanazotumia?
 
Back
Top Bottom