Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Chloroform
Methane trichloride
Methyl trichloride
Methenyl trichloride
TCM
Freon 20
Refrigerant-20
R-20
UN 1888
Hayo ndo majina tofauti tofauti ya hiyo dawa inayotumiwa na hao wezi
Kazi yake nini ?
 
Kwa mujibu wa makala ya uchambuzi ya Fikrapevu.com

Je, unaifahamu Dawa ya usingizi inayotumiwa na wezi kuwapulizia watu kabla ya kuiba? Inaitwa Chloroform.

Kwa muda mrefu kumekithiri vitendo vya uhalifu unaohusisha wezi kuingia kwenye nyumba za watu nyakati za usiku na kuwapulizia dawa ya usingizi na kisha kuchukua chochote wanachokitaka ndani ya nyumba.


Baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha aina hiyo ya uhalifu na ushirikina lakini ukweli ni kwamba ipo dawa mojawapo ya usingizi ambayo hutumiwa na wezi wengi kutekeleza uhalifu huo. Dawa hiyo kitaalamu inaitwa Chloroform.

Dawa hiyo ina uwezo wa kumlegeza au kumzimisha mtu kiasi kwamba ashindwe kujitambua na kuhisi chochote na wahalifu wakafanya chochote wanachoweza kwa muda wa kutosha. Wataalamu wa afya huitumia katika shughuli za kitabibu hasa wakati wa upasuaji.

Ili kufahamu madhara na tahadhari ya kuchukua juu ya dawa hii inapotumika, soma zaidi makala hii kwa kina (na nyinginezo makini ambazo ungependa kuzifahamu) kupitia => Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?
 
hahaaaa umenikumbusha miaka hiyo advance, msimamizi wa biology pract akaivuta maana ilikuwa inatumika kuwafanya panya wazimie wakati wa dissection,yule jamaa alilala hadi pepa inaisha
Hahaha dadeki
 
Kwahiyo Huu uzi si utawafundisha vijana mambo ya wizi, ?
 
Sio mwanamke tu mkuu hata kidume wanaweza legeza marinda.ukiona wamesepa na zagazaga na wewe wamekuacha salama unscathed ni jambo la kushukuru mungu.
Kwa kweli.. Hahaha
 
Mmm tusipoangalia huu uzi unaenda kusajili wezi wapya nchini
 
Naam acha kabisa tech ya mwafrica hapana chezea kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…