Tehe tehe tehe hayo majamaa yaliyokunywa mpaka chai ni 'noma', ukweli lazima tuyapongeze kwa umafia walioufanya kwa sababu huwezi kwenda kwenye nyumba ya mtu kuiba halafu ukanywa mpaka chai ni 'noma'.
Nakumbuka wakati naishi Kunduchi, jirani yetu mmoja alikuwa mfugaji wa bata. Alikuwa na bata wengi kama utitiri. Kumbe basi wazee wa kazi siku nyingi walikuwa wanawamezea mate wale bata.
Siku ya siku wazee wa kazi wakatia 'maguu', nafikiri walitumia hiyo dawa ya usingizi kwa maana siku hiyo usingizi ulikuwa mtamu balaa! Wazee wa kazi kama kawaida yao, wakachukua bata wote hawakuacha hata manyoa...watu tunaamka asubuhi tunakuta banda leupe, dah siku hiyo nilicheka sana kwa sauti ya chini chini kwa sababu wazee wa kazi walikuja na 'kiroliroli'... tuliona tu alama za matairi ya gari, yani wazee wa kazi kwa jeuri walikuja mpaka na gari, ule mngurumo wa gari watu hatukusikia tunakoroma tu, ha ha haa ni 'noma!'