Salaam jf.
Nilikuwa naomba uzoefu wenu wana jf, hasa katika hizi dawa wa wanazotumia wezi kuwaibia raia wema kuwapulizia madirishani wakati wa usiku wanapolala, kwanza nilikuwa nataka kufahamu jina lake na pili wapi wanapozipata lengo si kwa ajiri ya matumizi binafsi lengo ni kufahamu. Sababu wizi wa kuvunjiwa milango na madirisha umekithiri kibaya zaidi wezi wanathubutu kuwaibia walala hoi hadi maafisa wa serikali wenye silaha, juzi kati mh. Fulani ambaye anacheo kikubwa tu serikalini alipigwa vitu vyake vyote sebureni na mwengine kasafishwa sebure yote na watoto wa mjini, akiwemo pia mwanajeshi mstaafu nae alivunjiwa nyumba na wezi kusafisha sebure lakini kabla ya kuiba wezi walikunywa chai iliyokuwa sebureni na kuondoka. Inavyooshesha hii dawa inawapa kiburi sana, usishangae hadi usalama huwa wanapigwa.