Ni gari gani ambayo kila unapoiona unajisemea ipo siku nitanunua yangu

Ni gari gani ambayo kila unapoiona unajisemea ipo siku nitanunua yangu

WhatsApp Image 2024-08-06 at 21.45.28.jpeg
 
Ndiyo maana Mimi huku kijijini napendelea kuwaambia wanakijiji kuwa mkiona niko bize na simu jueni niko kwenye kikao na matajiri wenzangu wa Jamiiforums maana kwa hizi gari mlizotaja asiwadanganye mtu lazima mpambane haswa .

Mimi kijijini hapa namiliki Corolla yangu Safi kabisa na ndiyo gari pendwa kwa kukodiwa kwenye maharusi yao na zaidi ni gari pendwa la diwani kuazima ili akague miradi kupitia mambo hayo kiukweli nimetokea kukupenda sana hili gari na vile hakali mafuta kaniachia hela ya ulanzi ni gari ambayo naikubali .

Kwahiyo nawiwa kusema nahisi hili gari la urithi limemaliza kiu ya Mimi kumiliki gari lingine na sijawahi kuwaza kubadili aisee .

Note :nakopesheka Mimi Kama mtumishi kwa hiyo hivyo vyuma mlivyotaja nikiamua naweza kuvipata Ila nimeridhika na Corolla yangu ,kiasi nimeamua kubandika number plate ya jina la ukoo wetu 😃
 
Kaka hicho kina kinaanzia 370+ kwa trim hiyo niliyoichagua, lakini inaweza kuzidi hadi kufika 450 huko, kuna features nikianza kuzielezea hapa itakua gazeti... Lakini zile editions zengine kama GX, GXR, VX, VXR n.k zinakua chini kidogo!
mi nikipata V8 VX inatosha hata kama ni ya mwaka 2005😌😌
 
Back
Top Bottom