Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Kiongozi, hivi kati ya Allex na Runx kuna tofauti yoyote mbali na majina yao?
Kama ipo tofauti yoyote itanisaidia kufanya decision niagize gari ipi muda ukifika.
Oii hivi vidude vinafanana vitu vingi kasoro badge tu.

Sehemu nyingi ukisoma, watasema tofauti ni mbili kuu, mosi ni size na pili ni fuel consumption.

Inasemekana Allex ina nafasi zaidi kuliko Runx, ingawa ni tofauti ndogo sana, na pia Allex kidogo ni rafiki kwenye mafuta kuliko Runx, kidogo sana tofauti. Nilioana mahala 15km/L Allex kwa 12km/L Runx.

Pia, Runx ni sport version ya Corolla wakati Allex ni family car. Kwenye sport hapo utaona suspension za Runx ni tiff wakati Allex iko soft. Pia nahamini Runx ina option ya 1.5L na 1.8L wakati Allex yeye ana 1.5L tu.
 
Big up sana.
Mpaka hapo nishajua nataka nini
Allex for life.
 
Tufafanulie hiyo 1.5L na 1.8L ndo imekaaje na option imekaaje?
 
Hivi hizo gari zina chngamoto gani hasa, juzi nilikuwa naendeshaa hiyo gen 2 ni ya ndugu yangu haikunisumbua hata kidogo nimekaa nayo almost mwezi mzima
Hizo gari nzuri sana, madalali wa Tanzania ndio wanazisagia kunguni.
Mimi nimetumia first generation miaka 5 bila shida.
 
Kama maisha ya kuunga unga nitamkataza haya:

BMW

BMW

BMW

BMW

BMW
Mkuu BMW ina shida gani kwani...
Mimi nilikuwa na 530i nimedumu nayo miaka 3 na nilikuwa naenda nayo trip za dar to mwanza. Mbali na service ya kawaida haikuwahi nisumbua chochote. Mwisho nikamuuzia msukuma fulani aliipenda
 
Nisan X-Trail
 
Hii gari ni toleo la mwaka gani ?
 
Mkuu BMW ina shida gani kwani...
Mimi nilikuwa na 530i nimedumu nayo miaka 3 na nilikuwa naenda nayo trip za dar to mwanza. Mbali na service ya kawaida haikuwahi nisumbua chochote. Mwisho nikamuuzia msukuma fulani aliipenda
Mode gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…