Ni haki kweli kumlipia mpenzi wako mahari ng'ombe 40?

Usukumani Tena wamempunguzia sana ni kawaida sana wangemwanzia ng'ombe 80 wao wamesema 40 wanaweza punguza mpaka 30 lkn kama ni vzr aombe alipe za miguu kama 10 hivi zingine athamanishe fedha hapo atakuwa kapunguza

Tena wanyatunzu wanadharau kuliko kawaida

Hafu ni watafutaji pita kawaida

Deni kwao ni kama wachaga

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Nina mshkaji wangu, homeboy wangu kabisa ana mpenzi wake ambaye wamedumu naye kwenye mahusiano kwa takribani miaka 2.

Mwana akaamua ampeleke mtoto kwa wazazi wake huko Tanga kwanjeka. Wazazi wa mwana wakamwelewa na kumkubali huyo demu kiroho safi, sasa ikawa zamu ya demu kwao ni Simiyu maeneo ya Itilima ni mnyantuzu.

Kufika huko wazazi wa demu wakamkomalia mshkaji wangu alipe ng'ombe 40 kama mahari ya demu haswa ukizingatia wamemsomesha kwa gharama. Mshkaji aliponiomba ushauri juu ya hili swala, mi nikamshauri atoe kama kweli anampenda demu, ila wazazi wa mwana wamemwambia hawamtaki tena huyo demu wake nakwamba atafte mwingine.

Sasa kwanini wazazi wanaweka mahari za kukomoa watu? Na hapo si kama amemfanya mwanae kuwa kitega uchumi? Ni aibu sana tena sana!
Mkuu 40 ni nyingi sana. mimi jamaa yangu alikaziwa ngombe kumi mamake hatari.. ikabidi tubadilishe tusiongee kuhusu ngombe tuwaweke kwenye mfumo wa pesa ndo ikawa pona yetu.

Na hapo bado walikuwa wanasema ngombe wa kushibaa bei ni laki 5 so kwa 40 mkuu nashauri apige mimba tu alale hivi
 
Kwenye kikao tulikubaliana tunaweka mimba alafu tunapotea msituni huyo mshkaji wako kwan hakuhudhuria kikao
 
Ng'ombe 40? Kama jamaa anamihela atoe Tu maybe wanemkadiria kulingana na life lake
 
Kumbe rahisi hivi hauwezi kosa m8 aisee mimi nilipiga ng'ombe moja laki 8 hadi milioni so nikaona m 34 hadi m 40 parefu mno
Wewe unadhani watu wote wana uwezo wa kutoa milioni 8? Halafu mahari yote hiyo ya nini?
 
Nina mshkaji wangu, homeboy wangu kabisa ana mpenzi wake ambaye wamedumu naye kwenye mahusiano kwa takribani miaka 2.

Mwana akaamua ampeleke mtoto kwa wazazi wake huko Tanga kwanjeka. Wazazi wa mwana wakamwelewa na kumkubali huyo demu kiroho safi, sasa ikawa zamu ya demu kwao ni Simiyu maeneo ya Itilima ni mnyantuzu.

Kufika huko wazazi wa demu wakamkomalia mshkaji wangu alipe ng'ombe 40 kama mahari ya demu haswa ukizingatia wamemsomesha kwa gharama. Mshkaji aliponiomba ushauri juu ya hili swala, mi nikamshauri atoe kama kweli anampenda demu, ila wazazi wa mwana wamemwambia hawamtaki tena huyo demu wake nakwamba atafte mwingine.

Sasa kwanini wazazi wanaweka mahari za kukomoa watu? Na hapo si kama amemfanya mwanae kuwa kitega uchumi? Ni aibu sana tena sana!
Mahari za watoto kanda ya ziwa rangi nyeupe huwa ndio iko hivyo, wanyantuzu ni jamii ya wasukuma
 
Apo mahari inayotakiwa m2 nabado anaweza kuomba kupunguziwa,
Unadhani jamaa ataswaga ng'ombe awapeleke? Zamani ilikuwa ilikuwa inawezekana familia nyingi zilikuwa zakifugaji na walikua wanatoa kweli.
Niliwahi kuskia story kwamba zamani ikitajwa ng'ombe mahari ya mnyama yaani ni kwamba wakwe wanakuja kuchagua wenyewe zizini sasa wanachukua yale yenye afya kweli kweli halafu wanawaachia wale waliokonda.

Unaambiwa wajanja walikuwa wanakubaliana kesho mapema wanyama waje kuchukuliwa ila usiku usiku wanahamisha wale wooote wenye afya na mimba kisha wanaacha wale waliodhoofu na wazee 😂😂😂.

Mkija mnaambiwa haya ingia zizini tu mjichagulie hapo mtabahatisha bahatisha mkiondoka tu wanarudisha wote 😂😂.
 
Nina mshkaji wangu, homeboy wangu kabisa ana mpenzi wake ambaye wamedumu naye kwenye mahusiano kwa takribani miaka 2.

Mwana akaamua ampeleke mtoto kwa wazazi wake huko Tanga kwanjeka. Wazazi wa mwana wakamwelewa na kumkubali huyo demu kiroho safi, sasa ikawa zamu ya demu kwao ni Simiyu maeneo ya Itilima ni mnyantuzu.

Kufika huko wazazi wa demu wakamkomalia mshkaji wangu alipe ng'ombe 40 kama mahari ya demu haswa ukizingatia wamemsomesha kwa gharama. Mshkaji aliponiomba ushauri juu ya hili swala, mi nikamshauri atoe kama kweli anampenda demu, ila wazazi wa mwana wamemwambia hawamtaki tena huyo demu wake nakwamba atafte mwingine.

Sasa kwanini wazazi wanaweka mahari za kukomoa watu? Na hapo si kama amemfanya mwanae kuwa kitega uchumi? Ni aibu sana tena sana!
Jamaa atakuwa kila akiona ng'ombe, anashikwa na presha. Kapigwa kitu cha Emotional Damage.
 
Bibi yangu aliniambia hata mahari ya milioni 3 nisikubali sembuse ng'ombe 40. Kipindi hata kabla hamjatambulishana unakuta binti yao umemgharamikia mpaka basi huku wakijua binti yao anajiweza. Wachague, kusubiri ng'ombe 40 au binti yeye azalishwe na mtu baki halafu waanze kumlaumu. Uchumi wenyewe ni waajabu muda huu, halafu uchezee mafanikio yako kwa mtu ambaye anaweza kubadilika muda wowote. Kipindi cha chuoni watu wamechezeana wee, leo uniambie anadegree. Kwani degree yake itaniongezea nini kwenye standard ya maisha yangu. Halafu actually mimi nitaendelea kuwasaidia wao huku wamekula pesa yangu mwanzoni.
 
Back
Top Bottom