Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ndomaana kila siku tunasema tatizo la Nchi yetu ni Mkuu wa kaya hata akibadili mawaziri kila wiki bila ye mwenyewe kukiri Nchi imemshinda nakustep down ni sawa na kukausha bahari kwa kizibo cha soda.

Anataka kumuiga Farao kwa kuwa na moyo mgumu. Hajui hizi ni nyakati tofauti....
 
Sisi ni watawala huwezi kutupangia sehemu ya kufanyia kikao. FUNGA DOMO LAKO
 
Unadhani????? Hivi ndugu zangu tutaishi kwenye zama za kudhani hadi lini? Je hatuna kanuni zinazotuongoza katika hili na masuala mengine kati ya vyama vya siasa na serikali....?

Hawa Jamaa wa Deep Green walishajimiulikisha kabisa hii nchi kama vile walivyoamua kujimilikisha Viwanja vya mipira huko mikoani

KIukweli kaka umesema kitu cha msingi sana... nafikiri Ikulu ni moja kati ya mali muhimu sana ya serikali na sio chama na kila kitu kipo wazi juu ya matumizi yake kwamba kitu kinapofanyikia ikulu ni kitu cha kitaifa sio cha kiitikadi sasa.... hata wale mnaotetea hili swala kaeni mkijua hakuna sehemu inaruhusu vikao vya chama ndani ya jumba lile... huu ni ubabe tu coz no body will question him but will come a time for him to pay what he is doing now
 
Hivi ni kwa nini vyombo vya habari hata havihoji vikao vya CCM kufanyika Ikulu?
Jana tena kikao cha CCM kimefanyika Ikulu.

Kikao cha jana 27 April 2010

CC1.jpg



CC2.jpg
 
Je ni haki Chadema kuingia ikulu na magwanda Kama ni haki, kuna athari gani wana CCM kumfuata mwenyekiti wao ikulu ambako anaendesha serikali inayoongozwa na CCM . Pengine una tatizo la wivu usiokuwa na maana.
 
Kwaufupi ni kwamba tz imeoza katika Nyanja zote so what is needed ni kuunda upya katika ya nchi yetu, Honestly this time hatuna Raisi Kabisa ila ndio hivyo. Kuhusu vikao kufanyika Ikulu kisheria Raisi anaweza huo ila visiwe vikao vya chama kwa kuwa Ikulu ni Mali ya TANZANIA, vikao vya chama vinafanyika makao makuu ya chama husika.
 
Tatizo kila kitu ccm wanaamini cha kwao,ikulu ni yetu sote bila kujali chama. Vikao vya chama vilipe pango kwa serikali!
 
labda si vibaya kwa mkulu kuwaalika ikulu CC, lakini mahali stahiki ilikuwa kwenyw makao yao pale Lumumba!
 
Hakuna tatizo vikao vya chama tawala kufanyika Ikulu maana Ikulu ni makazi na ofisi ya rais. Tatizo wana CDM mnakariri sana hata nyinyi mkienda Ikulu ruksa kufanya vikao vya chama ila marufuku kunywa soda za Ikulu nadhan mmenipata
 
Yep, imejirudia tena and probably inaonekana ni practice fulani inajengeka.

Nyumba ya baba yangu imegeuzwa kuwa pango la majangili na vibaka.

Jamani tuamke nakuikataa hii,mazoea itageuzwa utaratibu.
 
Naomba kujuzwa....Je ni halali kuendesha shughuli za Chama cha siasa ndani ya IKULU au haya pia ni mapungufu yaliyomo ndani ya Katiba yetu ya sasa?? Hivi vyama si vinakuwa na ofisi zake kwa shughuli zake sasa iweje CCM mara kadhaa vikao vyao wanavifanyia IKULU.....Vikao vyao hivyo vinagharimiwa kwa fedha za chama au kwa fedha za Watanzania????

Wana haki zote hata ya kutoa malazi CCM ni chama dume nyie majike tumeshawapiga mimba wote!
 
Ikulu ishakuwa kijiwe longtime,au hamsikilizi hotuba za marehemu Kambarage,ule utakatifu wa ikulu kwishney kuanzia enzi za Mzee Ruksa
 
Inategemea kikao kinazungumzia nini. Kama kile kikao kingekuwa kinazungumzia maswala ya kichama ningelalama ila kilikuwa kinazungumzia kashfa ya baadhi ya Mawaziri kwa hiyo yalikuwa na maswala ya Serikali.
 
Juzi raisi kikwete aliongoza kikao cha kamati kuu ya ccm kilichofanyika ikulu na kufanya uteuzi wa mgombea wa ccm kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mdogo wa kupata mwakilishi wa jimbo moja huko Zanzibar.Bila shaka hii si mara ya kwanza kwa vikao vya chama kufanyikia ikulu bali hali hii imekuwa kama utaratibu wa kawaida.

Hivi kweli ktk mfumo wa saiasa wa vyama vingi ni halali kwa vikao vya chama kufanyikia ikulu?Kikao cha chama kufanyikia ikulu kuna tofauti gani na kitendo cha viongozi wengine wa serikali kama mawaziri kutumia magari ya serikali kwa shughuli za chama?Vitendo kama hivi vimekuwa vikipingwa na wanasiasa kama ni moja ya matumizi mabaya ya madaraka.Matumizi ya mali za serikali kwa ajili ya kuendeshea shughuli za chama ni jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele sana.Sasa ikulu si ni ofisi ya serikali kwa ajili ya shughuli za serikali na si chama?Wadau wenye uelewa wa mambo hayo tunaomba mtupe ufafanuzi wa jambo hili.

Gharama za kikao cha chama kinachopewa ruzuku ili kuendesha shughuli zake kinapofanyikia ikulu kinagharamiwa na nani?Serikali kupitia ikulu au ni chama chenyewe?Na kama ni serikali je ni sahihi?Nini maana ya chama kupewa ruzuku?Je hayo si matumizi mabaya ya madaraka?

Mwisho kama huu ni utaratibu wa kawaida naona wakati umefika kupitia katiba mpya kupiga marufuku jambo hili.Hii ikulu leo wako ccm kesho chadema na keshokutwa CAF na pia vyama vingine na kwahivyo ni bora ipitishwe sheria kuzuia jambo hili ili lisiendelee kwa siku zijazo hata kama ccm watakuwa wametoka madarakani.
 
Kwa kufanyia kikao cha CCM ikulu Kikwete ameonyesha anavyovunja kanuni za utawala bora. Ikulu si mali ya CCM ni mali ya watanzania wote. Hata hivyo kumlaumu Kikwete ni kutomtendea haki. Maana jamaa ni mweupe kweli kweli. Hata mfumo wenyewe ni wa kulaumiwa. Hamuoni tulivyojazana na kupe wanaoitwa wakuu wa wilaya na mikoa na wabunge wa viti maalumu?
 
Kwa hiyo ni bora kikao kingefanyika Dodoma Rais akachukua ndege akajaza mafuta na kuruka hadi Dodoma! Tatizo ni kwamba wakati gani JK anakoma kuwa Rais na kubaki kuwa MWenyekiti wa CCM? Kutenganisha hapa inakuwa vigumu kweli. Rais analindwa na serikali kwa gharama za serikali na hakuna wakati ambapo watasema kuwa sasa Rais anafanya kazi za Chama hivyo alindwe na Chama! Hakuna wakati ambapo anauvua Uamiri Jeshi Mkuu. Kuondoa tatizo hili inawezekana tu endapo uongozi wa chama na Urais vitatofautishwa japokuwa bado Rais atakuwa akitumia vyombo va serikali wakati akihudhuria mikutano lakini itaondoa mikutano kufanyika Ikulu.
 
ukumbi wa mikutano wa ikulu unakodishwa, so inawezekana ccm walikodi na wamepewa risiti ili wafanyie kikao chao! hata CHAUMA nao wakitaka kufanya mkutano wao next week ruksa!
 
Back
Top Bottom