Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwa hiyo ni bora kikao kingefanyika Dodoma Rais akachukua ndege akajaza mafuta na kuruka hadi Dodoma! Tatizo ni kwamba wakati gani JK anakoma kuwa Rais na kubaki kuwa MWenyekiti wa CCM? Kutenganisha hapa inakuwa vigumu kweli. Rais analindwa na serikali kwa gharama za serikali na hakuna wakati ambapo watasema kuwa sasa Rais anafanya kazi za Chama hivyo alindwe na Chama! Hakuna wakati ambapo anauvua Uamiri Jeshi Mkuu. Kuondoa tatizo hili inawezekana tu endapo uongozi wa chama na Urais vitatofautishwa japokuwa bado Rais atakuwa akitumia vyombo va serikali wakati akihudhuria mikutano lakini itaondoa mikutano kufanyika Ikulu.
Mkuu hapa hoja wa si kusafiri mpaka Dodoma tu kwani hata Dar ccm wana ofisi na pia wanapewa fungu kutoka serikalini kama ruzuku kwa ajili ya kugharamia shughuli cha chama kwahiyo wangeweza hata kukodi ukumbi wa mkutano popote pale wanapoona panafaa na si kutumia ikulu kwa shughuli za chama.
Hebu tujiulize leo mfano mkurugenzi wa wilaya ambae ni mpenzi wa chadema au meya katika halmashauri yoyote ile ambae ametokana na chadema naye akaamua kutumia ofisi aliokabidhiwa na serikali kwa shughuli za chama chake itakuwaje?