Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Kwa hiyo ni bora kikao kingefanyika Dodoma Rais akachukua ndege akajaza mafuta na kuruka hadi Dodoma! Tatizo ni kwamba wakati gani JK anakoma kuwa Rais na kubaki kuwa MWenyekiti wa CCM? Kutenganisha hapa inakuwa vigumu kweli. Rais analindwa na serikali kwa gharama za serikali na hakuna wakati ambapo watasema kuwa sasa Rais anafanya kazi za Chama hivyo alindwe na Chama! Hakuna wakati ambapo anauvua Uamiri Jeshi Mkuu. Kuondoa tatizo hili inawezekana tu endapo uongozi wa chama na Urais vitatofautishwa japokuwa bado Rais atakuwa akitumia vyombo va serikali wakati akihudhuria mikutano lakini itaondoa mikutano kufanyika Ikulu.

Mkuu hapa hoja wa si kusafiri mpaka Dodoma tu kwani hata Dar ccm wana ofisi na pia wanapewa fungu kutoka serikalini kama ruzuku kwa ajili ya kugharamia shughuli cha chama kwahiyo wangeweza hata kukodi ukumbi wa mkutano popote pale wanapoona panafaa na si kutumia ikulu kwa shughuli za chama.

Hebu tujiulize leo mfano mkurugenzi wa wilaya ambae ni mpenzi wa chadema au meya katika halmashauri yoyote ile ambae ametokana na chadema naye akaamua kutumia ofisi aliokabidhiwa na serikali kwa shughuli za chama chake itakuwaje?
 
ukumbi wa mikutano wa ikulu unakodishwa, so inawezekana ccm walikodi na wamepewa risiti ili wafanyie kikao chao! hata CHAUMA nao wakitaka kufanya mkutano wao next week ruksa!

Acha kutudanganya watu wazima.Chadema au CAF wakikodisha watakubaliwa au kupigwa mizengwe tu?
 
ni ujinga tu. Kwani Obama anapofanya kampeni kurudi ikulu , anahama ikulu na kukaa home kwake? Rais anaendelea kuwa mkuu wa nchi hata anapofanya shughuli za chama. ni aibu kwa great thinker kuwa narrow thinker.
 
ni ujinga tu. Kwani Obama anapofanya kampeni kurudi ikulu , anahama ikulu na kukaa home kwake? Rais anaendelea kuwa mkuu wa nchi hata anapofanya shughuli za chama. ni aibu kwa great thinker kuwa narrow thinker.

Ni aibu kwa chama tawala kubebwa na serikali kwa shughuli za chama.
 
ukumbi wa mikutano wa ikulu unakodishwa, so inawezekana ccm walikodi na wamepewa risiti ili wafanyie kikao chao! hata CHAUMA nao wakitaka kufanya mkutano wao next week ruksa!

...Huu ndo uongo tusioutaka. Kukodisha ukumbi wa Ikulu ni kushusha hadhi na kuhatarisha usalama wa taifa letu. Leo "wamekodi" NEC ya CCM, kesho nakodi kwa ajili ya harusi yangu! Ni uhuni mtupu.
 
Mkuu, naomba nikiwa nikufahamishe kuwa sina personal issue na mtu yeyote, na uandishi wangu hautawaliwi na hizo. Kama umesoma vizuri nimeuliza swali la kimsingi kuhusu kufanyia vikao vya chama tawala ikulu. Nakumbuka kuanzia enzi za TANU (ndiyo, nakumbuka vizuri sana) vikao vya chama vilifanyika katika ofisi za chama, hata wakati wa Chama kiliposhika hatamu, ndio kwanza makao makuu ya CCM Lumumba street, yakapata hadhi zaidi. Je kumekuwa na mabadiliko rasmi mapya yaliyotokea ambapo chama tawala kimeshika hatamu tena

:banplease::frusty:Hiro rijamaa rako rinatetea vikao vya CCM kufanyikia ikulu na wakati CCM wanayo bajeti itokanayo na ruzuku wanayopata kila mwezi,mara nyingi vikao vya CCM havijadili maendeleo ya watanzania, hapo walipo ni Ikulu iliyojengwa kwa kodi zetu wavuja jasho wa TZ,cha zaidi hapo wanajadili namna ya kumdhibiti Lema na Dr.Slaa na CHADEMA kwa ujumla.
1.Hawapo hapo kuwajadili wale Majangili waliotorosha Twiga kwa ndege ya jeshi la waarabu,
2.Hapo walipo pia hawajadili namna mafisadi walioficha pesa za rusha ya rada,Kagoda,
3.Wala hapo hawawezi kujadili pesa za rushwa ya mikataba ya uchimbaji madini,pesa ambazo zimebainika kufichwa nchini Uswisi.
4.Hapo pia hawajadili namna ambavyo watafanya ili kumrudisha wale mijusi (Dinosours) waliyemuuza kwa wakoloni wa kijerumani,wanaogopa watanyimwa mikopo na misaa ndani ya miaka 51 ya uhuru.

Hapo walipo wanajadili maslahi ya Chama zaIdi na si ya watanzania wa CHADEMA au wale wasio na vyama vya siasa.
:clap2: :focus::A S thumbs_down:..................................................................................................................................
 
Naomba kufahamishwa na wale wenye kufahamu zaidi, hivi ni sawa vikao vya CCM kufanyika Ikulu? Ninavyotambua Ikulu huwasikilisha serikali ikiwa ni pamoja na jamii nzima ya Tanzania.

Hivi CUF, TLP au Chadema wanaweza kufanyia mikutano yao Ikulu au katika sehemu zingine kama hizo?

Hiki ndicho chanzo cha swali langu:

ccm-ikulu.jpg


Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ikulu jijini Dar es Salaam (Photo by Freddy Maro).

Hawana uhalali wa kuwa hapo kwa mwamvuli wa siasa,hapo ni mahali patakatifu lakini cha ajabu wanajadili namna ya kuidhibiti nguvu ya umma,Hapo wanakula bata hakuna lolote,isipokuwa wanajadili namna ya kukabidhi madaraka ya uongozi wa nchi kwa CHADEMA.
 
Naomba kufahamishwa na wale wenye kufahamu zaidi, hivi ni sawa vikao vya CCM kufanyika Ikulu? Ninavyotambua Ikulu huwasikilisha serikali ikiwa ni pamoja na jamii nzima ya Tanzania.

Hivi CUF, TLP au Chadema wanaweza kufanyia mikutano yao Ikulu au katika sehemu zingine kama hizo?

Hiki ndicho chanzo cha swali langu:

ccm-ikulu.jpg


Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ikulu jijini Dar es Salaam (Photo by Freddy Maro).

Wastani wa umri wa magwiji wa magamba ni miaka kama 68 hivi, angalieni hapo juu wote karibu ni wastaafu sasa unataka kupata nini hapo????? Waachieni vijana jamani
 
CCM kufanyia vikao ikulu si halali ni matumizi mabaya ya madaraka na pesa za umma. Hii ni kwa hoja tu kuwa ikulu yote inalipiwa na serikali na hivyo haifai vyama kimoja kimoja kutumia umeme, maji, viti n.k kwa kuwa ni kodi za watanzania wote. Tunawashauri wawe na ofisi kule Mabwepande itawasaidia kwa vikao ambavyo hawataki watu kuingia kwani hakuna atakayewafuata huko, na ukiwafuata huko yakikukuta ya Ulimboka usilalamike!!!
 
mmesahau maneno ya katibu mkuu mstaafu kwamba kila kitu kilichopo nchini ni mali ya CCM, sasa sina uhakika inawezekana hata sisi wenyewe ni mali yao -- ha ha ha
 
Acha kutudanganya watu wazima.Chadema au CAF wakikodisha watakubaliwa au kupigwa mizengwe tu?

sikudanganyi mkuu, ila haiingii akilini kwa watu wazima kupageuza ikulu kuwa pango la vikao vya wanyang'anyi, haya ni matumizi mabaya ya mali ya umma. ni sawa na kugeuza benzi la ikulu daladala. its not fair kwa nyinyiemu kufanyia vikao ikulu!
 
mkutano hauna shida, tatizo ni kutumia hela, magari ya serikali kwa ajiri ya kazi za chama
 
hawa watu kwa sababu ccm na ye mwenyewe wamekuwa wakiwatumia waislamu kwa manufaa ya ccm sasa anogopa siri kuwekwa hadharani tumeone waislamu wengi viongozi mzee mwinyi aliwadhibiti akina ponda mzee makamba aliwadhibiti pale magomeni sasa kikwete kwa nini tusikuone wewe ni swahiba na unawafurahia kwa sababu wanafanya kazi abayo ndani ya moyo wako unachekelea lakini kumnuka vita ya kidini haitamuacha salma ridhiwani wala ndugu yako yeyote acha udini ongoza nchi nyerere aliyuonya watanzania kukuchagua sasa tunaona faida zake
 
sikudanganyi mkuu, ila haiingii akilini kwa watu wazima kupageuza ikulu kuwa pango la vikao vya wanyang'anyi, haya ni matumizi mabaya ya mali ya umma. ni sawa na kugeuza benzi la ikulu daladala. its not fair kwa nyinyiemu kufanyia vikao ikulu!

Mkuu hapo sawa kama nawe unaunga mkono hao nyinyiemu nao kutofanya vikao ikulu.Na siamini kama kweli wanalipia ukumbi na ninaomba wanasheria wawafungulie mashitaka.Hata kama kesi itafanywa kisanii kwasababu wao wameshika mihimili yote ila itakuwa ni aibu tosha kwao na kwa maneno mengine tunasemai takuwa message sent.
 
Ilianza taratibu pale CCM ilipoanza kufanya mikutano yake Ikulu. Tukapiga sana kelele hapa lakini watu wengi wakiwemo Chadema hawakusema chochote.

Wengi tulijua nini kitafuata. Na kweli kimetokea. Sio tuu CCM inatumia zana za umma kwa faida za chama bali pia watumishi wa umma.

Na wake zenu watatumiwa hivi soon.
 
Tatizo la kufanyia kikao ikulu ni kutumia fedha zetu Watanzania ambazo sio za CCM.
 
Haya mawazo ya kitoto.kama sisim wanatawala wanayo haki ya kufanya vikao popote. Ngojeni nanyi mkishapewa dhamana hiyo mfanye sio kulalama
 
Back
Top Bottom