Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

ma'ccm wanafanyia vikao vyao ikulu maana ndipo wanapopanga mikakati yao yakufilisi inji hii
 
Wana najisi ikulu yetu mwezi mtukufu! Ikulu ni mahala patakatifu ila inatumiwa na wmakafir wa kimaadili!
 
Naomba kufahamishwa na wale wenye kufahamu zaidi, hivi ni sawa vikao vya CCM kufanyika Ikulu? Ninavyotambua Ikulu huwasikilisha serikali ikiwa ni pamoja na jamii nzima ya Tanzania.

Hivi CUF, TLP au Chadema wanaweza kufanyia mikutano yao Ikulu au katika sehemu zingine kama hizo?

Hiki ndicho chanzo cha swali langu:

ccm-ikulu.jpg


Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ikulu jijini Dar es Salaam (Photo by Freddy Maro).
Ikulu palikuwa mahali pa takatifu wakati wa urais wa Nyerere tu. Walipoingia dot com wakapageuza pango la wanyang'anyi. Hapo ndipo dili za wizi wa EPA, ugawanaji wa nyumba za serikali ullipoppangwa na kutekelezwa bila aibu. Hapo ndipo sasa utashangaa mtu aliyeitapeli serikali na RICHMOND yake akifika hapo na kupokelewa kwa heshima zote tena na makamu wa rais. Madudu ni mengi! You name it! Ingekuwa wakati wa Nyerere baadhi ya unaowaona katika picha hapo wasingenusa hapo. Wakati ule tuhuma tu ilitosha kukudisqualify. Lakini sasa mtu hata akituhumiwa kusafirisha pembe za ndovu au wanyama wetu anatinga ikulu kiulaiiiiini!!
 
Ikulu ni mahala patakatifu.

Ikulu haina chama cha siasa

kama mnataka ukumbi wa kufanyia mikutano yenu ya fitna na majungu nendeni kwenye makao makuu ya chama chenu
 
tena wakome kabisa viwanja vya michezo walitunyang'anya wakajimilikisha,majengo yenye ofisi zao tulio jenga nayo wakayatwaa kiubabe leo na ikulu wanataka
 
Utakatifu wa Ikulu ulishakufa siku nyingi Mkuu pale fisadi Mkapa alipoamua kufanya biashara na ufisadi akiwa ndani ya Ikulu. Ikulu yetu si mahali patakatifu tena.

Ikulu ni mahala patakatifu.

Ikulu haina chama cha siasa

kama mnataka ukumbi wa kufanyia mikutano yenu ya fitna na majungu nendeni kwenye makao makuu ya chama chenu
 
Back
Top Bottom