Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Rais wa Jamhuri ana uhuru wa kufanya mkutano na kikundi chochote ikulu wakati wowote atakao.

Swali kama hili linakuwa na mantiki pale mkutano ufanyike ikulu alafu Rais asiwepo... lakini maadamu yupo utaambiwa na wana-usalama kwamba waliona Lumbumba sio salama sasa utasema je? na ofisi yake na makao yake yako Ikulu.

Kwa hali hiyo hata vikao vya harusi anaweza kufanyia humo humo?

Amandla........
 
Hivi na mweshimiwa chenge ni mjumbe? au ni macho yangu tu? Haya kwa wale wanaofikiria kuwa ktk chama cha Mapinduzi kutatokea mabadiliko miaka ya karibuni wameliwa.

Unadhani wameanza kuliwa leo? walianza tangu kipindi kileeeeeeeeeeeeeee Muungwana alipoanza na aliposhiriki kikamilifu kuileta IPTL.

Mzi
 
wakubwa Kama katiba isipobadika nchi hii hayo mambo ni ya kawaida. Hivi mlitegema wafanye kitu gani? serikali ni CCM nchi hii!
 
Si HALALI hata kwa chembe moja. Kwani Ikulu ni ya CCM nadhani Ikulu ni mali ya watanzania wote. Kama ni halali basi vyama vyote vya siasa ruksa kufanya mikutano yenu kwenye nyumba ya ufalme. Hii ni tatizo la kuongozwa na watu wasiofikiria mbali. Sasa wamegeuza Ikulu ni mali ya CCM kazi kweli kweli.
 
- Si Usalama wa Taifa ndio wanaamua Rais afanyie wapi mkutano, au aende wapi na asiende wapi, au? na kwamba kwenye hili la usalama wa viongozi wa juu wa taifa hakuna compromise wala negotiations na yeyote yule au?

Respect.


FMEs!
 
Unafahamu mzee cost ya kumpeleka Rais wa Jamhuri Dodoma na Kurudi. au unadhani Rais atalipiwa na chama... safari zote za Rais zinalipiwa na Serikali mkuu... they are the one responsible kwa usalama wake.

Samahani kama nimekukwaza hivi Rais wenu safari hii anaenda kutembelea nchi gani vile??
 
- Si Usalama wa Taifa ndio wanaamua Rais afanyie wapi mkutano, au aende wapi na asiende wapi, au? na kwamba kwenye hili la usalama wa viongozi wa juu wa taifa hakuna compromise wala negotiations na yeyote yule

Wanasema ati bongo hakuna UWT wapo wapo tu
 
Yes, But until when... kwa sasa yuko ndani ya mstari mkuu, na huwezi kulaumu kabisa.

Furthermore, kwa utaratibu wa sasa alivyofanya mkutano Magogoni it is cost effective kwetu taifa na kwa CCM kuliko angeupeleka Dodoma.

Ukifuatilia kwa makini CCM pia wanaogopa mzigo wa kusafirisha wajumbe wao ndio maana mara nyingi sana NEC inakutana wakati wa Bunge sessions.


Lumumba kuna ofisi ndogo na nafikiri ni 'cost effective' zaidi. Naona kama kuna hitilafu katika hili
 
uko ndio kutimiza ilani ya ccm, walishasema unapochagua ccm ina maana serikali itayoundwa itakua ya ccm kwa iyo yote yatayofanywa na ccm ndio ya serikali na ya serikali ndio ya ccm kwa iyo ndio ivyo tena vyama vya upinzani kuchukua nchi ni ngumu, we unadhani seif, mrema na cheyo kusalimisha njaa zao wajinga, washaona hamna nchi watayochukua
 
Hivi mtoto wa rais akiolewa send-off atafanyia wapi?

Mkuu Safari ni Safari,

Najua unapoelekea. Suala la kumtoa binti ni la kijamii na Rais ambaye makazi yake ni Ikulu anaweza kufanya hiyo shughuli hapo Ikulu, lakini kwa kutumia gharama zake binafsi[ingawa hili jamaa wanaweza kulipindisha chini ya zuria kwani huwajibikaji bado mdogo au haupo]. Upande wa Pili, Kuendesha shughuli za Kichama kwa manufaa ya chama kimoja katika majengo na gharama za Serikali ni kinyume na taratibu za nchi[sijui kama sheria ya vyama inalizungumzia hili].
 
Unajuwa ndio maana tunasema katiba ibadilishwe ili iendane na mfumo wa vyama vingi, kwani bado CCM wanadhani ni sawa na wameruhusu vyama vingi ili kukidhi masharti ya IMF/WB etc. uongo mwingi bado, mfano Labor uingereza wanaweza kumhoji PM Gordon Brown kuhusu matumizi mabaya ya fedha na madaraka lakini bongo mhh!!!
 
Yes, But until when... kwa sasa yuko ndani ya mstari mkuu, na huwezi kulaumu kabisa.

Furthermore, kwa utaratibu wa sasa alivyofanya mkutano Magogoni it is cost effective kwetu taifa na kwa CCM kuliko angeupeleka Dodoma.

Ukifuatilia kwa makini CCM pia wanaogopa mzigo wa kusafirisha wajumbe wao ndio maana mara nyingi sana NEC inakutana wakati wa Bunge sessions.

Huwezi kulaumu kwa sababu gani? Nani alisema Rais lazima awe mwenyekiti? Huo ni utaratibu wao na siyo katiba ya nchi. Kama kuna gharama awalilie CCM huko huko!

Kwa utaratibu wa sasa, upi huo? hatuna utaratibu wa aina hiyo ktk nchi hii.
 
Ni jambo linalokera lakini watu wako Kimya. Hivi hawa CCM wana haki gani ya kuendeshea vikao vya Kamati Kuu ya Chama chao kwenye Ofisi ya Umma. Ikulu nayo ni Ofisi ya CCM?

Gharama za kuendeshea vikao vya CCM Ikulu, inalipwa na nani. Na jee kama CHADEMA nao wakitaka kuendeshea vikao vyao Ikulu (kabla ya kushika Dola) wataruhusiwa na kama watakazwa ni kwa mantiki gani?
 
Ni jambo linalokera lakini watu wako Kimya. Hivi hawa CCM wana haki gani ya kuendeshea vikao vya Kamati Kuu ya Chama chao kwenye Ofisi ya Umma. Ikulu nayo ni Ofisi ya CCM?

Gharama za kuendeshea vikao vya CCM Ikulu, inalipwa na nani. Na jee kama CHADEMA nao wakitaka kuendeshea vikao vyao Ikulu (kabla ya kushika Dola) wataruhusiwa na kama watakazwa ni kwa mantiki gani?

The greatest mistake JK did is not to die in the office!
 
JK amejiruhusu kuwa rais rojorojo, ambae amezungukwa na watu dhaifu ambao hawamsaidii, hata kuliona hilo na lenyewe ni jambo lakuhitaji ushauri wa Bana.
kweli tutaona mengi mpaka huyu Mkwere atakapoondoka Ikulu.
 
Katiba yetu inamapungufu ya ajabu na ni makubwa mno. Umeshawahi kuona wapi, waziri anagombea ubunge, muda huo huo yuko anafanya kazi za kiserikali, mchana yuko kweny kampeni, huu uchuro si wa kuuachia uendelee.
 
Back
Top Bottom